Kesi ya Maxence Melo yaahirishwa baada ya Wakili wa Serikali kuomba muda wa kujipanga

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
647dea92-215e-4173-9d57-08593d235d5e.jpg


Habari wanaJF,

Kesi namba 457 inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Ndg Maxence Mubyazi Melo na mwenzake Mike William imeahirishwa tena baada ya Wakili wa Serikali Bwana Salum kuomba muda wa kujipanga kwakuwa ametoka likizo.

Aidha kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 13 March 2017 itakapoanza kusikilizwa rasmi kwakuwa upelelezi umekamilika.

Ndugu Maxence Melo amewakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya(Kiongozi wa jopo hilo), Wakili Peter Kibatala na Wakili Omar Msemo.

Katika kesi namba 457, ilielezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwambapa kwamba, katika siku na tarehe tofauti kati ya Mei 10, 2016 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni ndani ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Melo akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media Co. Ltd ambayo inaendesha mtandao wa JamiiForums, wakati akijua kwamba Jeshi la Polisi Tanzania linafanya upelelezi wa jinai kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa kwenye mtandao wake, kwa nia ya kuvuruga uchunguzi, alikaidi kwa makusudi amri ya kutoa taarifa ambazo alikuwa nazo, kinyume na kifungu cha 22(2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber Crimes Law) namba 14 ya mwaka 2015.
 
Naona kama anaona hapo hakuna kesi,maana polisi walisema hawajamaliza uchunguzi,leo wakili hajajipanga ,mh!!!!!!!!!!!!!!!.Na yule Wakili wa Mello amejitoa kuogopa fagio la mwenye nyumba
 
Kila wakili ni msomi, Ulipaswa kuandika wabobezi, Nguli, Neno wasomi linaleta taswira habari yako ipo kishabiki.
 
Mawakili wa serikali wakati mwingine nawaonea huruma sana wanawapotezea tuu muda Maxence Melo mwisho wa siku watashindwa kesi kila siku wa naomba kuongezewa muda walifungua kesi kwa kukurupuka wanasogeza muda wakishindwa waonekana hata walipambana
 
View attachment 472238

Habari wanaJF,

Kesi namba 457 inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Ndg Maxence Mubyazi Melo imeahirishwa tena baada ya Wakili wa Serikali Bwana Salumu kuomba muda wa kujipanga kwakuwa ametoka likizo.

Aidha kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 13 March 2017 itakapoanza kusikilizwa rasmi kwakuwa upelelezi umekamilika.

Ndugu Maxence Melo amewakilishwa na Mawakili wasomi, Wakili Jeremiah Mtobesya(Kiongozi wa jopo hilo), Wakili Peter Kibatala na Wakili Omar Msemo.
wapoteza muda wa watu tu hawa na kesi zao uchwara
 
Sasa huku ni kupoteza pesa za walipa kodi. Criminal justice system OVERVIEW OF CRIMINAL JUSTICE SYSTEM IN PAKISTAN inaanza Polisi wakimkamata mtuhumiwa jalada hupelekwa DPP kujiridhisha kisheria kuna kesi ya kupelekwa mahakamani. Hapo mawakili wa serikali na mwendesha mashtaka wa serikali na mfumo w criminal justice system unazidi kuonesha udhaifu wa kitaaluma / ujuzi /weledi wao.
 
Jamani muda wote huo bado anajipanga? Au anamaanisha kusubiri maelekezo?
 
Back
Top Bottom