Kesi ya Masheikh: Mawakili wa Jamhuri waomba muda kuongeza nguvu

Sep 19, 2019
43
383
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

KESI YA MASHEIKH LEO TEREHE 20.05.2021: UPANDE WA JAMHURI UMETOA UDHURU

Shauri la Masheikh lililomalizika jana katika Mahakama ya Rufani Tanzania, leo limerudishwa Mahakama Kuu kwaajili ya kusikilizwa. Shauri hilo sasa litasikilizwa mashtaka 11, baada ya 14, kufutwa.

Katika shauri la Mahakama ya Rufaa upande wa Jamhuri ulishindwa baada ya majaji watatu kukubaliana na hoja za mawakili wanaowatetea Masheikh.

Katika hali isiyotarajiwa mawakili 10, wa upande wa Jamhuri leo Mahakamani wameomba shauri hilo liakhirishwe na kupangiwa siku nyingine.

Mawakili hao waliwasilisha ombi hilo kwa madai kuwa kiongozi wao DPP Biswalo ameondolewa katika mamlaka hayo na hivyo wanataka DPP mpya aliyeapishwa juzi aje kuwasaidia kuongeza nguvu.

Walimwambia Jaji kuwa tayari Rais Samia Suhu Hassn kamteuwa DPP mpya lakini hajajipanga kwaajili ya kuhudhuria katika shauri hilo.

Wakati mawakili wa serikali wakito udhuru wa kumkosa DPP kwa upande wao, jopo la Mawakili 9, wanaowatetea Masheikh lilikuwa tulivu Mahakamani likisubiri amri ya Jaji ya kuendelea na shauri.

Jopo hilo likizungumza mbele ya Jaji lilipinga udhuru uliotolewa na upande wa Jamhuri likisema kuwa Mawakili 10, wa upande wa Jamhuri wanatosha kuendesha shauri bila ya DPP.

Katika mashauri haya jopo la Mawakili wa Masheikh wamekuwa wakijenga hoja nzito za kisheria na kujijengea taswira ya ukakamavu wa Kisheria Mahakamani.

Hata hivyo Jaji alizingatia ombi la upande wa Jamhuri na kuwakubalia ombi lao. Shauri limeakhirishwa mpaka jumatano tarehe 27.05.2021.

Ust. Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura.
0713118812
 
Kuwatoa hao Mashekhe ni kuliingiza Taifa katika UGAIDI, hao ni wapinzani wa Waislam, Wakristo na Taifa kwa ujumla...labda kama hujawafuatilia vizuri tangu matukio yao ya Mombasa na Zanzibar ufukweni

Ni Magaidi waliokomaa.
 
nasikia bakwata wamekemea ya palestina?,ila ya al shabab,alkaida,syria,congo,msumbiji,ccm,huamsho sio tija.
 
Back
Top Bottom