Kesi ya Lundenga Sept. 23 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Lundenga Sept. 23

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 4, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,491
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Lundenga Sept. 23

  na Vumilia Kondo
  Tanzania Daima~Sauti ya watu

  KESI ya madai inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency International, waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga, itaanza kusikilizwa rasmi Septemba 23 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Jagalile Mwaseba.

  Kesi hiyo iliyofunguliwa Agosti 5 mwaka huu na mke wa Lundenga ,Twigi Hashimu Lundenga, mlalamikaji anataka kugawana mali walizochuma pamoja na mumewe huyo baada ya kumtelekeza na familia.

  Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo jana, Ritha Tarimo, alimtaka mwanasheria wa mlalamikaji (Twigi), kuwa anatakiwa kuwasilisha pingamizi la majibu yaliyoletwa na wakili wa Lundenga, Audax Kahendaguza, hadi ifikapo Septemba 19.

  Licha ya kuwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Lundenga, pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga.

  Licha ya dini ya Kiislamu kumruhusu Lundenga kuwa na mke zaidi ya mmoja, kinacholalamikiwa mahakamani hapo ni madai ya Lundenga kuitelekeza familia ya mke wake wa kwanza, baada ya kuoa mwanamke mwingine, aliyewahi kuwa mmoja wa Miss Tanga mwaka 1997.

  Inadaiwa kuwa, baada ya Lundenga kumwoa mwanamke huyo wa Kitanga, alihamia katika nyumba mpya iliyoko Sinza, ambayo aliijenga akiwa na mke wa kwanza, huku akiitelekeza familia ya mke wa kwanza, hivyo mwanamke huyo anataka wagawane mali.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani wanawake wa Tanga si mchezo Lundenga sikulaumu ila kumbuka watoto!1
   
Loading...