Kesi ya Liyumba: Naibu Gavana aibua mambo mazito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Liyumba: Naibu Gavana aibua mambo mazito

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mundele, Jan 27, 2010.

 1. mundele

  mundele Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAIBU Gavana wa Benki Kuu (BoT), Juma Reli (54), ameshindwa kuithibitishia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuhusu hasara iliyopatikana katika mradi wa ujenzi wa minara pacha kwa sababu hadi sasa ripoti ya mwisho ya matumuzi ya fedha za mradi huo haijakamilika.

  Sambamba na hilo, katika hali isiyotarajiwa, upande wa mashitaka katika kesi hiyo umesema unakusudia kupunguza idadi ya mashahidi wake kutoka 15.

  Naibu Gavana huyo ambaye ni shahidi wa nane wa upande wa mashitaka katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221, alitoa maelezo hayo jana mbele ya kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa baada ya wakili wa utetezi, Majura Magafu na Hudson Ndusyepo kutaka ufafanuzi.

  Kesi hiyo ya matumizi mabaya katika ofisi ya umma inamkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa benki hiyo, Amatus Liyumba,.

  Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano baina ya mawakili wa utetezi na shahidi huyo:

  Wakili: Lini umeajiriwa BoT?

  Shahidi: Niliteuliwa kuwa Naibu Gavana Februari 2005 na ndipo nilipoanza rasmi kufanya kazi katika BoT.

  Wakili: Unajua mradi huu wa ujenzi wa minara pacha ulianza lini?

  Shahidi:
  Sikumbuki sawa sawa.

  Wakili: Utakubaliana nami kimsingi wakati unaanza kufanya kazi hapo, mradi huo ulikuwa umefikia hatua za mwisho?

  Shahidi: Ni kweli mradi niliukuta katikati.

  Wakili: Utakubaliana na mimi hayo mabadiliko ya nyongeza yanazolalamikiwa na upande wa mashitaka, hilo zoezi lilikuwa limeishapita?

  Shahidi: Hapana.

  Wakili: Ni mabadiliko ya nyongeza katika mradi huo yalifanyika wakati wewe upo BoT, unayajua?

  Shahidi: Mradi huo ni mkubwa, siwezi kukumbuka.

  Wakili: Ni nani alikuwa na maamuzi ya mwisho ya hili lifanyike au hili lisifanyike?

  Shahidi: Gavana.

  Wakili: Nani alikuwa na maamuzi ya mwisho ya kuidhinisha mabadiliko ya mradi na fedha?

  Shahidi: Ni bodi ya wakurugenzi ambayo mwenyekiti wake ni gavana.

  Wakili: Je, mkurugenzi wa idara zozote pale BoT anaweza kutoa maamuzi bila gavana na bodi kujua?

  Shahidi: Hapana.

  Wakili: Kuna kipindi chochote wakati mradi huu unaendelea Liyumba aliwahi kuandika maombi ambayo hayaendani na matakwa ya menejimeti?

  Shahidi: Sikumbuki.

  Wakili: Kuna kipindi chochote wakati wewe ukiwa Naibu Gavana, wewe binafsi na gavana mliwahi kupeleka maombi kwenye bodi yakakataliwa?

  Shahidi: Hatujawahi kupeleka.

  Wakili: Kwa hiyo Liyumba alikuwa anapata maelekezo ya ujenzi kutoka kwa Meneja Mradi Deogratius Kweka?

  Shahidi: Ndiyo.

  Wakili: Kuna siku Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo aliwahi kulalamikia matumizi mabaya ya fedha katika huo mradi?

  Shahidi: Sikumbuki (watu wakaangua vicheko).

  Wakili: Nyie kama BoT, huu mradi umeleta madhara kwenu?

  Shahidi: Haujaleta madhara kabisa.

  Wakili: Hadi hapa tulipofikia kuna hasara yoyote imepatikana kutokana na ujenzi wa mradi huo?

  Shahidi: Siwezi kusema wala kuthibitisha hasara eti imetokea katika mradi huo kwa sababu hadi hivi sasa ninapotoa ushahidi ripoti ya mwisho ya matumizi ya fedha za ujenzi wa mradi huo ‘Finacial Account’ haijakamilika. (watu wakaangua vicheko).

  Mahojiano kati ya Hakimu Mkazi na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:

  Hakimu: Shahidi kumbuka mshitakiwa (Liyumba) ameshitakiwa kwa kesi ya kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221, sasa mahakama hii tunatafuta uthibitisho wa kiasi hicho kutoka pande zote mbili za kesi hii?

  Shahidi: Sipendi kudanganya ila ukweli ni kwamba hatuwezi kuthibitisha hasara kwa sababu Financial Account haijakamilika.

  Hakimu: Ulisema mradi huu haukupitia kwenye menejimenti, ulipitia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi, ieleze mahakama ulifikajefikaje kwenye bodi na ni Liyumba yeye kama yeye ndiye aliupeleka?

  Shahidi:
  Kama nilivyokwishaeleza, gavana ana nguvu za kisheria. Jambo linaweza kutoka idara fulani akalipitisha bila ya kuwepo kwa wajumbe wengine wa bodi au menejimenti na kisheria anaruhusiwa.

  Baada ya shahidi kumaliza kutoa ushahidi wake, Wakili wa Serikali, Juma Mzarau, aliiomba mahakama hiyo iahirishe kesi hiyo hadi Februari 4-5 mwaka huu, kwani wanatarajia kupunguza idadi ya mashahidi kutoka mashahidi 15.

  Aliieleza mahakama kwamba kuna shahidi wanayemtegemea kutoka nchini Singapore na waliihakikishia mahakama kuwa katika siku hizo wataleta mashahidi watu wa mwisho.

  Hata hivyo wakili wa utetezi, Magafu alidai upande wa mashitaka haupo makini na kazi yao na kuongeza kuwa kama watakubaliana na kesi hiyo ikiahirishwa hadi tarehe hiyo, basi uhakikishe unawaleta mashahidi hao bila kukosa, la sivyo siku hiyo wafunge kesi yao.

  Aidha, Kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Edson Mkasimongwa, alikubaliana na ombi hilo na kwa mujibu wa ratiba ilipangwa itaanza kusikilizwa mfululizo kuanzia jana hadi Februari 5, mwaka huu.

  Aidha, aliamuru upande wa utetezi upewe nakala ya mwenendo mzima wa kesi ili waweze kujiandaa kwa ajili ya kujibu hoja kama mshitakiwa ana kesi ya kujibu au la.

  Liyumba alifikishwa mahakamani hapo Januari 26, mwaka jana akikabiliwa na makosa mawili ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

  Hadi sasa Liyumba yupo rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.


  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nchi ya wanasarakasi.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  hapo Liyumba hana kesi!
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,104
  Trophy Points: 280
  Kwanini hapewi dhamana wakati kweka alikuwa na kesi moja na liyumba lakini yuko kitaa akikata bia kwa kwenda mbele?
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mfumo wa kufunga mahesabu baada ya mradi husika kukamilika hupaswa kuchukua muda gani kisheria?
  Hapa tunaomba wataalamu wa miradi ya ujenzi wa nyumba za serikali na wataalamu wa mambo ya mahesabu watujuvye kuhusu hili, isijekuwa tunatengeneza kosa juu ya kosa.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,104
  Trophy Points: 280
  kesho ya nyani unataka kumpa tumbili?
   
 7. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapa kuna changa la macho. Kama ripoti ya ujenzi wa majengo pacha haijakamilika je hiyo hasara ambayo serikali inadai imepata ilikokotolewa kwa njia gani na kutoka wapi? Na je Liyumba anashitakiwa kwa kosa gani wakati BOT wenyewe kupitia kwa Naibu Gavana Juma Reli wamesema BOT haikupata hasara kwa sasa kwa sababu final financial report haijakamilika. Ieleweke kwamba simtetei mtu hapa. Nashindwa kuelewa credibility ya serikali mpaka inapeleka kesi mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kutosha. Ikumbukwe kuwa fedha zinazotumiwa kuendesha hiyo kesi ni ya walipa kodi wa Tanzania, ilitokea Liyumba kweli hana kosa serikali itatuambia nini? Kwamba wametumia mamilioni ya walipa kodi kuendesha kesi isiyo na ushahidi uliojitosheleza na hatimaye kushindwa?
  Mungu ibariki Tanzania yetu
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Yaaani mie nimeangalia jana nikabakia kushangaa ..kama Gavana hajui lolote huyo Liumba wamemuweka ndani kwa nini??
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  From the face of it , Lyiumba is a free man.
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  mlitegemea nini kama naibu gavana ni kilaza....kwa credential zake ..advance diploma na MBA ....hazitoshi kumfanya awe naibu gavana..ni AHSANTE MUUNGANO!!!...ilibidi naibu gavana atoke zanzibar....walipochagua BOT walimtaka jamaa mmoja anatoka PEMBA ...ni Phd holder...serikali ya zanzibar ikamkataa....wakampendekeza RELI
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Naibu Gavana Juma Reli (54) wa Benki Kuu Tanzania (BoT), ameiambia Mahakama kwamba Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo haikufurahishwa na ombi la kuidhinisha malipo ya fedha za matumizi ya mradi wa majengo pacha ya benki ambazo tayari zilishafanyiwa malipo.

  Reli ambaye ni shahidi wa nane katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.1 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi, Amatus Liyumba, alidai pia maombi hayo yaliwasilishwa kwenye bodi hiyo kupitia Idara ya Utumishi na Utawala iliyokuwa chini ya mshtakiwa huyo.

  Naibu Gavana huyo alitoa madai hayo mbele ya jopo la mahakimu watatu Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Muingwe wanaosikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Akiongozwa na wakili wa serikali, Juma Ramadhani, shahidi huyo alidai kuwa kitaaluma ni mhasibu ambapo aliteuliwa na Rais kushika wadhifa huo Februari, mwaka 2005.

  Alidai kuwa mabadiliko ya mradi hayakuwahi kujadiliwa na Bodi ya Wakurugenzi isipokuwa iliombwa kibali cha kuidhinisha matumizi wakati tayari malipo yameshafanyika.

  "Baada ya bodi kupokea maombi ya kuomba kuidhinisha matumizi ambayo yameshafanyika, Bodi haikufurahia utaratibu wa kuomba idhini ya matumizi ya fedha zilizokwishakutumika," alidai shahidi.

  Sehemu ya mahojiano kati ya wakili wa serikali na shahidi yalikuwa kama ifuatavyo:-

  Wakili: Shahidi umekuwa na wadhifa wa Naibu Gavana tangu lini?

  Shahidi: Niliteuliwa na Mheshimiwa Rais Februari, 2005.

  Wakili: Shughuli zako ni zipi kwa nafasi uliyonayo?

  Shahidi: Ni kumsaidia Gavana kazi mbalimbali, kuhudhuria vikao vya Bodi pamoja na kufanya kazi za kila siku za BoT.

  Wakili: Kuna aina ngapi za matumizi ya fedha za BoT?

  Shahidi: Kuna aina mbili ya matumizi ya kawaida ya kila siku na matumizi ya maendeleo.

  Wakili: Je, uidhinishwaji wa matumizi ya maendeleo uko vipi?

  Shahidi: Huanza kupitia idara ya utumishi na uendeshaji ambapo hupelekwa katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo kupata idhini ya matumizi. Ikishatolewa idhini ni kazi ya uongozi kufanya matumizi ambayo yametolewa na bodi. Pia matumizi ya kawaida hayana tofauti na yale ya maendeleo utaratibu uko sawa.

  Wakili: Bodi inamshauri nani?

  Shahidi: Inamshauri gavana na manaibu wake.

  Wakili: Gavana ana uwezo wa kutoa maamuzi yoyote BoT?

  Shahidi: Ndiyo kwa BoT, gavana ana uwezo wa kutoa uamuzi na naibu gavana pia lakini katika maeneo yake.

  Wakili: Umewahi kufuatilia mradi wa majengo pacha wa BoT?

  Shahidi: Ndiyo, majengo pacha na Gulioni Zanzibar.

  Wakili: Mradi huo ulikuwa chini ya idara gani?

  Shahidi: Idara ya Utumishi ya benki hiyo.

  Wakili: Ulikuwa ukiidhinisha mabadiliko ya mradi kama naibu gavana?

  Shahidi: Hapana.

  Wakili: Ulipokuwa mjumbe wa bodi hiyo, suala la mabadiliko ya mradi liliwahi kujadiliwa?

  Shahidi: Ndiyo.

  Wakili: Je, nini kilijadiliwa?

  Shahidi: Tulijadili ombi la malipo ambayo yalikuwa yamefanyika ambapo bodi ilitakiwa kuhalalisha matumizi yaliyofanyika ya mradi huo.

  Wakili: Hoja ya kufanya mabadiliko ya mradi ilijadiliwa wakati gani?

  Shahidi: Haikujadiliwa bali ilikuja pamoja wakati tayari mabadiliko na malipo yameshafanyika.

  Wakili: Bodi ilikuwa na uamuzi gani kuhusu hilo?

  Shahidi: Bodi haikufurahia utaratibu huo wa kuomba idhini wakati tayari matumizi yameshafanyika.

  Naye wakili wa utetezi Majura Magafu, alimhoji shahidi kama hivi:

  Wakili: Kabla ya kwenda BoT, ulikuwa unafanya kazi wapi?

  Shahidi: Nilikuwa Mkurugenzi Chuo cha Fedha Zanzibar.

  Wakili: Unaweza kujua mradi ulianza lini?

  Shahidi: Nilipoteuliwa nilikuta mradi unaendelea.

  Wakili: Je, mabadiliko gani yalifanyika ukiwa pale unayajua?

  Shahidi: Nafahamu maombi ya mabadiliko yalifanyika.

  Wakili; Nani alikuwa na mamlaka ya mwisho katika maamuzi BoT?

  Shahidi: Maamuzi ya mwisho ya mradi huo yalikuwa ni ya bodi ya wakurugenzi.

  Wakili: Nani alihusika kusimamia mradi huo?

  Shahidi: Mbali na Liyumba kulikuwa na Meneja Mradi Deogratius Kweka.

  Wakili: Kweka jukumu lake kubwa lilikuwa ni nini?

  Shahidi: Kusimamia mradi kwa kuwasiliana na mhandisi pamoja na kuushauri uongozi wa juu wa BoT kuhusu hali ya mradi na ulipofikia, lakini meneja mradi hana mamlaka ya kufanya kitu chochote.

  Wakili: Je, mradi umeleta madhara kwa BoT?

  Shahidi: Umeleta faida haukuleta madhara yoyote.

  Hakimu Mlacha alimhoji shahidi huyo kama hadi sasa benki hiyo imepata hasara ya kiasi gani?

  Shahidi: Hadi sasa BoT bado haijapokea majumuisho ya mahesabu ya mradi hivyo hatujui kama kuna hasara kiasi gani au la.

  Kesi hiyo itaendelea kusikiliza shahidi wa tisa Februari 4 na 5, mwaka huu ambapo ushahidi wa shahidi wa tisa wa upande wa mashitaka.

  Katika kesi hiyo, Liyumba anadaiwa kuwa akiwa kama Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, alipindisha mkataba wa BoT kuhusu mradi wa ujenzi wa maghorofa pacha na hivyo kuongeza kiasi cha fedha zilizokuwa zikihitajika katika ujenzi.

  Ilidaiwa kuwa kutokana na Liyumba kupindisha mkataba huo, aliisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 153,077,715.71 ambazo ni sawa na Sh. 221,197,299,200.96 kwa sasa.

  CHANZO: NIPASHE


  Maswali matatu hapa! Nani anasauti ya mwisho ndani ya bodi gavana au mwenyeketi wa Bodi.
  Kama ni gavana nini kazi ya bodi ya wakurugenzi kwenda kunywa chai au kujadili maswala nyeti???
  Mwisho kabisa kama hawajui kama BOT imepata hasara au la ina maana hawakuwa na strategic plan kabla ya ujenzi??? If not ina maana ujenzi umefanyika kiholela kwa maana utajengaje jengo such a huge investment bila kuangalia faida na hasara zake???
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Madhara na hasara wapi na wapi? Nadhani kinachozungumziwa hapa ni Final Accounts na siyo Financial Accounts. Sasa kama hakuna madhara, ikiwa ina maana defect liability period imepita bila matatizo kwa nini wanachelewa kukamilisha final accounts? Hawaoni kuwa wanajiweka wazi kwa madai kutoka kwa mkandarasi kwa kumcheleweshea pesa yake?

  Amandla.......
   
 13. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Pole,naona umehuzunika sana Liyumba kuendelea kuwekwa ndani! Atatoka.
   
 14. mundele

  mundele Member

  #14
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania yetu Inateketea...Hivi unawezaje kumuajiri Naibu Gavana Mbumbumbu kama Reli kwenye kitengo muhimu kama hiki? yani ni kama pale BOT haelewi chochote kinachoendelea.....Tusisahau Mtu huyo huyo ndiyo mmojawapo wa magavana waliojengewa majumba ya mabilioni. Je, msaada wake katika kulijenga taifa uko wapi? mtu kama huyo ni wa kumstahafisha kwa maslahi ya Taifa. Na kesi hii ya Liumba mwisho wake naanza kuuona, Hii kesi imegeuzwa kabisa na kuimaliza kwa kutumia kivuli cha Gavana ambaye ni marehemu na idhinisho zote zilizopitishwa zitatupiwa kwake...By the end of time LIUMBA will be Free kwakuwa mabadiliko ya project hiyo yaliidhinishwa na Marehemu Gavana.

  Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Africa.
   
 15. mundele

  mundele Member

  #15
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gavana wa BOT ndiyo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi...umeona mambo hayo
   
 16. GY

  GY JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  kweli neno ni toka kwa mtoa neno, likishaenda mbele zaidi, neno huhama toka kwenye uhalisia wake

  Taarifa hiyo hiyo, imenukuliwa na vyombo viwili vya habari, lakini ina tofauti kubwa sana
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani angekuwa huyo mwenye PhD ndiye deputy gavana hiyo hasara angeijuaje wakati ripoti bado haijakamilika?
   
 18. N

  Nanu JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mradi bado haujakamilika as we talk now! bado kuna mambo yanaendelea kidogokidogo!
  Kwa ushahidi wa Reli kama vile Liyumba hana kesi ya kujibu............
  Uongozi huu wa visasi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!taabu kwelikweli.
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kaka si useme tu Dr Mohamed wa IFM na yule jamaa angelienda BOT angeliifuma kwani at least ana ufahamu wa good governance ni nini. Unategemea nini na siasa za kulindana????
   
 20. N

  Nanu JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kesi hii ilifunguliwa baada ya kifo cha Gavana. Halafu Reli si mbumbu anasema anachokielewa, ujue kuwa yupo mahakamani na anatakiwa aseme ukweli na ambao anaweza kuutetea akiwekwa kwenye kona. Ukweli ni kwamba bodi ilipitisha mabadiliko na ndiyo maana yaliendelea. Kama bado haikuridhika basi aliyeruhsu matumizi bila adhini angechukuliwa hatua. inaonekana kila kitu hapo BoT kilfuata process na hat TZS1.2billion za nyumba ya gavana ilifuata process hiyo hiyo....
   
Loading...