Kesi ya kupinga matokeo ya Godless Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kupinga matokeo ya Godless Lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Sep 5, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ile kesi ya kupinga matokea ya ubunge wa Arusha mjini iliyofunguliwa na Musa mkangaa na wenzanke zidi ya kamanda Godbless Lema, mkurungezi wa manispaa ya Arusha na mwanasheria itaanza kuunguruma leo...Katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana, Lema, alimbwaga kwa kura nyingi aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian. Lema alipata kura 56,196 na Dk. Burian aliambulia kura 37.460......nitawajuza zaidi kinachoendelea


  ====
  Kesi inaendelea tena leo tarehe 06.02.2012
  CCM imejaza mabausa sijaelewa kazi ni kwanini...
  nitawajuza zaidi...
  ====
  Ushahidi waanza kutolewa

  Na Queen Lema, Arusha

  KESI ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, imeanza kusikilizwa jana.

  Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji, Bw. Musa Mkangaa, aliieleza Mahakama jinsi Bw. Lema alivyotumia maneno kumdharirisha aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Batilda Buriani.

  Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2010, inasikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Jaji Mfawidhi, Gabriel Rwakibarila, kutoka Mahakama ya Sumbawanga.

  Bw. Mkangaa alidai kuwa yeye binafsi alifanikiwa kutembelea sehemu nne za mikutano ya kampeni ya Bw. Lema, ambapo mbali na kutoa ahadi, mbunge huyo alimkashifu Dkt. Buriani.

  Alidai kuwa Agosti 312010, katika eneo la Kwa Muorombo, Kata ya Terrat, Bw. Lema aliwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kuwa wanaume katika makabila ya Wachaga na Waarusha, hawawezi kutawaliwa na mwanamke.

  Alisema kauli hiyo kwa mujibu wa sheria ni kinyume cha taratibu na kudai kuwa, mbali ya kuwakataza wananchi kutompa kura Bi. Buriani pia aliwataka kujiadhari na watu wanaovaa vitambaa katika vichwa vyao, kwani huenda ni miongoni mwa makundi ya kigaidi.

  "Mimi nilimsikia Bw. Lema akiwaambia wananchi wasimchague Dkt. Buriani kwa kuwa anavaa vitambaa na kufunika kichwa kila mara hivyo si kiongozi bora," alisema.

  Katika hatua nyingine, shahidi huyo alisema Septembe 18,2010, saa sita mchana katika eneo la Mbauda, Bw. Lema, akiwa na viongozi wa chama chake waliendelea kurudia maneno hayo.
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Sijui kwanini kuna watu hawana kasumba ya kukubali matokeo.
  Uchaguzi umeisha na sasa ni wakati wa kufanya kazi.
  mtu unapitwa kura 18736 na bado wapinga matokeo...huwezi kuwa na akili timamu.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mkuu Crashwise.

  Asante kwa taarifa lakini chonde chonde weka ushabiki pembeni tujuze kinachoendelea hata kama kamanda wako kaminywa sema tu hii ndiyo starehe ya JF.Habari za Lema kashinda kwa kura nyingi hazina msingi kwasababu kinachopingwa si kukosewa kwa hesaba tu.


   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkuu kuna mengine zaidi ya hesabu?
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hebu ni kumbushe nilini nililipoti kwa kuweka ushabiki zaidi.....
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mkuu yapo mengine zaidi ya hesabu nitakujulisha baadaye kuna jamaa zangu wapo hapo mahakamani kumtegemea Crashwise pekee yake ni kujidanganya mchana kweupe.Crashwise yuko kwaajili ya Lema na CDM akiona kaminywa hakika usitegemee atatujuza sana sana atatafuta visingizio kama kawaida yake.


   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu umeshasahau kesi ya madiwani ulivyowahukumu kabla ya mahakama haijatoa hukumu.Kwanza ulishawabatiza wasaliti ebu jiweke wewe ndiyo hakimu madiwani wangetendewa haki ?.

   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu usipate shida na huyu mtani wa jadi, we endelea kutujuza kinachojiri huko mahakamani.

  Hivi huyo Mussa Mkangaa aliyefungua kesi ya kupinga matokeo ni wa chama gani?
   
 9. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Maisha kutafuta sio kutafutana.
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sasa kama kuna jamaa zako hapo mahakamani kwanini kumlalamikia Crashwise huku at the same time ukimtegemea?

  Na hayo mengine kumbe huyajui pamoja na kukaa arusha na kujivika usemaji wa anti-Lema, unasubiri jamaa yako ndo akufahamishe? Mara zote huwa unakuwa mjuvi wa mambo yanayomhusu Lema, sasa hili imekuwaje likakupita kushoto?
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mussa Mkangaa ni diwani wa zamani CCM sijui siku hizi ana wadhifa gani ndani ya chama cha Magamba.

   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  M Maranya

  kesi ya kupinga ubunge wa Lema awali ilifunguliwa na watu wengine baadaye wakajitoa sasa sijui kwa hakika kama mashitaka ni yale yale ila ninachojua kuna vipengele zaidi ya vitano vinavyobishaniwa pia muda umeshapita sana unajua mimi si kama Crashwise hana shughuli nyingine zaidi ya CDM na Lema.

  Kitakachojadiliwa mahakamani hakika nitakijua muda huu jamaa zangu wapo ndani nadhani unajua taratibu za kimahakama lazima simu zote zizimwe.Habari atakazoleta Crashwise lazima niziverify upo mwita.


   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ngongo amesaini contract ya kumtafutia mabaya Lema kwa hali na mali. Kwake yeye kumtafuta Lema ndo maisha.
   
 14. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ngongo heshima kwako!kuna watu wanashinda wakicheza bao kuanzia asubuhi hadi jioni,nafamila zao ziko vizuri,swala la kusema kuwa crashwise hana shuguli nyingine zaidi ya lema na chadema sio haki,kwasababu uwezi kumpangia mtu shuguli ya kufanya ukizingatia aumlishi wala kumvisha,inaonesha unachuki tu binafsi na crashwise na sio kitu kingine,maisha ni kutafuta sio kutafutana.
   
 15. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwita huu ndio ujinga ambao tunaufanya watanzania,na siku zote mwisho wa ubaya ni aibu,Inaonesha Ng'ongo ni kama alivyo FF yaani wanamchukia mtu tu bila sababu ya msingi,FF ukimuuliza sababu ya kumchukia Nyerere anajikanyaga kanyaga tu,sasa hili swala na liona kwa ng'ongo.
  Tufanya kazi watanzania tuache majungu na kutafutana pasipo na sababu.
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi cjaona anacholenga Ngongo mpk muda huu! Crashwise,huyu Ngongo Mi naona ni sawa na kelele ya chura haimnyimi ng'ombe kunywa maji. Crashwise 2nakutegemea Kamanda.
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ha ha haa, Ngongo bana heshima kwako mkuu.

  Haya mkuu nasubiri kusoma verified information toka kwa watu wako.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ndo maana mimi huwa nashindwa kumuelewa Ngongo.

  Mwanzoni alipoanza kumshambulia Lema nilidhani ni siasa za uchaguzi tu, baada ya uchaguzi mashambulizi yangeisha lakini wapi bwana Ngongo anaendelea kutupa mawe.

  Mkuu ngongo badilika, inaonekana kama una kisasi na Lema, kwa maana hii yako sasa imevuka kiwango cha chuki.
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mzee wa Lushoto upo? mbona umekuwa adimu kiasi hicho arife?
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  nimechelewa kufika lakini kinachobishaniwa sasa ni juu ya maneno aliyoyatumia lema kwenye kampeni kuwa yalikuwa yana mkashifu mgombea wa ccm..wanaulizwa yaliwaathiri vipi waliofungua kesi
   
Loading...