Kesi ya kumpa Mimba mwanafunzi

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Wadau mimi naishi na mtoto wa dada yangu, kwasababu dada yangu hana uwezo nilichukua jukumu la kumsomesha huyu mtoto, kwasasa yupo form four, jana kafukuzwa shule baada ya kugundulika ni mjamzito wa miezi mitano. Kwasababu sifahamu vema sheria zinazosimamia hili swala naomba kufahamu yafuatayo:-

1. Je ni sahihi huyu mtoto kufukuzwa shule hasa ukichukulia nimelipa ada mpaka siku atakapomaliza masomo yake?

2. Kijana aliyempatia uja uzito anakili kufanya hivyo ila anajibu jeuri sana kwamba nisimfuatefuate. Je ni hatua gani za kisheria naweza kumchukulia huyu kijana hasa ukichukulia huyu bint yetu ana umri wa zaidi ya miaka kumi na nane yaani ana miaka18 na miezi7 hivyo alikutana naye kimwili akiwa ana umri zaidi ya miaka18.
 
Peleka shitaka polisi, watakupa wongozo kamili kuitafuta haki ya upande wenu.
 
Mtunze huyo binti, akijaliwa kujifungua salama na mtoto wake akikua au wakati anaendelea kunyonyesha anaweza kuendelea na masomo kama private candidate, achana na kesi ambazo zitakugarimu muda na fedha na hauwezi kubadilisha yaliyotokea, onyesha upendo kwa huyo binti, amepata mimba kwa bahati mbaya au kutokana na kukosa elimu ya uzazi, yeye kuwa na mahusiano ni haki yake na ni mahitaji muhimu ya akili na mwili, ni bahati mbaya aliyempata hafai/amemwacha solemba, kitu ambacho kinamtesa kisaikolojia pia.
 
Ahsante Mkuu Visenti mwenyewe nilikuwa nafikiria kitu kama hicho kwamba ikiwezekana kwasababu mimba bado haijaanza kumsumbua waalimu wangemuacha aendelee na masomo. na nilikuwa sifikirii kumshtaki huyu kijana lakini inaniumiza sana anapo jibu mbovu as if hawezi kuadhibiwa.
 
Last edited by a moderator:
Achana na mikesi isiyo na kichwa wala miguu. Alimbaka, hapana. Walikubaliana na wakiwa na akili timamu. Ushauri wa kuachana na kesi kama hiyo ni sahihi, hakuna utakachopata mahakamani, labda kuwapelekea pesa polisi na hakimu. Lakini alimpa mimba ama walipeana? Kumpa ina maana huyo kijana wa kiume si wa kawaida, anazo mimba anagawa kwa wasichana? Maana yangu ni hii, mimba bila kubakwa inapatikana kwa ushirikiano wa watu wawili. Yaani bintiyo alishiriki kikamilifu wakati wa kuitengeneza hiyo mimba, hakupewa, bali walipeana!
 
Eeee.... polisi wa nchi gani? Tanzania? Usiende watakutia ndani na kukubambika kesi. Acha kabisa. Watadai ulikuwa mzembe mpaka bintiyo akapata ujauzito. Usiende.
 
Ningeshauri ajisajili kama "Private Candidate" kama muda haujapita, lakini kama muda umeshapita afanye mtihani mwakani kama private candidate. Kwa sasa sheria iliyopo hairuhusu mwanafunzi (Primary and secondary school) akiwa mjamzito awepo shuleni. Hiyo haijalishi hata kama umemaliza ada yote. Binti alishafanya makosa hayo tayari, kingine cha kufanya waweza kwenda ktk vyombo vya sheria ingawa binafsi naona ni kupotezeana muda tu, kosa lilishafanyika hao. Huyo kijana wahusishwe wazazi wake kuhusu kumtunza huyo binti (akiwa kwako) kisha mtoto akishazaliwa. Vijana wakikubaliana kuoana hilo litakuwa lao sasa kwa baadae.
 
Sheria zenyewe za Bongo utapoteza muda, achana nae huyo kijana. Mwambie binti atunze mimba na mtoto. Kama ipo ipo tu one day yes.
 
Mtunze huyo binti, akijaliwa kujifungua salama na mtoto wake akikua au wakati anaendelea kunyonyesha anaweza kuendelea na masomo kama private candidate, achana na kesi ambazo zitakugarimu muda na fedha na hauwezi kubadilisha yaliyotokea, onyesha upendo kwa huyo binti, amepata mimba kwa bahati mbaya au kutokana na kukosa elimu ya uzazi, yeye kuwa na mahusiano ni haki yake na ni mahitaji muhimu ya akili na mwili, ni bahati mbaya aliyempata hafai/amemwacha solemba, kitu ambacho kinamtesa kisaikolojia pia.
Huo ndio ushauri wetu kwako.
 
Pole mkuuu waswahili walisema kua uyaone, we kiroho safi endelea kulea mwana and then mjukuu
 
Wadau mimi naishi na mtoto wa dada yangu, kwasababu dada yangu hana uwezo nilichukua jukumu la kumsomesha huyu mtoto, kwasasa yupo form four, jana kafukuzwa shule baada ya kugundulika ni mjamzito wa miezi mitano. Kwasababu sifahamu vema sheria zinazosimamia hili swala naomba kufahamu yafuatayo:-

1. Je ni sahihi huyu mtoto kufukuzwa shule hasa ukichukulia nimelipa ada mpaka siku atakapomaliza masomo yake?

2. Kijana aliyempatia uja uzito anakili kufanya hivyo ila anajibu jeuri sana kwamba nisimfuatefuate. Je ni hatua gani za kisheria naweza kumchukulia huyu kijana hasa ukichukulia huyu bint yetu ana umri wa zaidi ya miaka kumi na nane yaani ana miaka18 na miezi7 hivyo alikutana naye kimwili akiwa ana umri zaidi ya miaka18.

Bora ushukuru huyo kupewa mimba angepewa ukimwi je?

Baraka Boki (MEng, MBA from Duke university)
 
Visenti ukiwa hujapitia kwa mama muuza unakuwaga na mapointi!!!!safi sana,Ezan!fanya kama alivyokushauri visenti!
 
Mtunze huyo binti, akijaliwa kujifungua salama na mtoto wake akikua au wakati anaendelea kunyonyesha anaweza kuendelea na masomo kama private candidate, achana na kesi ambazo zitakugarimu muda na fedha na hauwezi kubadilisha yaliyotokea, onyesha upendo kwa huyo binti, amepata mimba kwa bahati mbaya au kutokana na kukosa elimu ya uzazi, yeye kuwa na mahusiano ni haki yake na ni mahitaji muhimu ya akili na mwili, ni bahati mbaya aliyempata hafai/amemwacha solemba, kitu ambacho kinamtesa kisaikolojia pia.

Mkuu unamaanisha amuache tu huyo kijana aliyempa mimba binti yake na still anajibu jeuri? Yaani hata Makonzi tu??
Mkuu Ezan mfuate huyo kijana umshikishe adabu personally, unless jiandae kuwa na mkwe asiye-behave.:glasses-nerdy:
 
Last edited by a moderator:
Ningeshauri ajisajili kama "Private Candidate" kama muda haujapita, lakini kama muda umeshapita afanye mtihani mwakani kama private candidate. Kwa sasa sheria iliyopo hairuhusu mwanafunzi (Primary and secondary school) akiwa mjamzito awepo shuleni. Hiyo haijalishi hata kama umemaliza ada yote. Binti alishafanya makosa hayo tayari, kingine cha kufanya waweza kwenda ktk vyombo vya sheria ingawa binafsi naona ni kupotezeana muda tu, kosa lilishafanyika hao. Huyo kijana wahusishwe wazazi wake kuhusu kumtunza huyo binti (akiwa kwako) kisha mtoto akishazaliwa. Vijana wakikubaliana kuoana hilo litakuwa lao sasa kwa baadae.

Why kama private candidate wakati hajafanya bado final exam? Unless you mean apospone till next year then afanye as a normal school candidate in a private school. Private candidates ni wale ambao wanarudia mtihani( I'm ready to be corrected)
 
Mfungulie kesi huyo jamaa. Usimwache hivihivi. Nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Jamaa afunguliwe kesi ya kumkatiza masomo huyo binti. Mapenzi hayawezi kuyazidi nguvu masomo. Ingekuwa kesi ya madai ningeinunua...

Mzee Tupatupa
 
Why kama private candidate wakati hajafanya bado final exam? Unless you mean apospone till next year then afanye as a normal school candidate in a private school. Private candidates ni wale ambao wanarudia mtihani( I'm ready to be corrected)
Nadhani uko sahihi, nilitaka kumaanisha hivyo.
 
Sheria akishapata mimba haijalishi kalipa ada ajalipa ni kwao na sijui ule mkakati wa kutaka kuwarudisha shule baada ya kuza ulishia wapi?
 
Back
Top Bottom