Mheshimiwa Dilunga,
Nashukuru kwa ku-react juu ya maoni yangu kuhusu kesi ya Mramba, Yona, na Mgonja.
Nilichofafanua ni utaratibu unaotumika kupata kibali ili waziri aingie ktk mkataba na taasisi yoyote tunayotaka ifanye kazi fulani. Kama Mramba, Yona na Mgonja waliandaa Cabinet Paper na ikakubaliwa, waliyotekeleza baadaye ni maamuzi ya Rais.
Naelewa kwamba DPP haagizwi na Rais au chombo chochote. Lakini DPP haamui mambo mazito kama kuwapeleka kortini watu mashuhuri kama ex-ministers na permanent secretaries,bila kushauriana na uongozi wa serikali. Kwa maoni yangu, ni lazima Rais alikubaliana na DPP juu ya kuendelea na kesi hii.
Jambo moja ningetaka kufafanua zaidi ni kwamba siwatetei hawa watuhumiwa. Kama kuna ushahidi kwamba walipokea rushwa kabla ya kuandaa Cabinet Paper, basi hilo ni kosa. Lakini ijulikane kwamba sheria ya manunuzi pamoja na sheria ya uchimbaji, zote zinaweza kuwekwa kando kwa maelezo yanayoainishwa katika Waraka wa Cabinet na Rais akikubali, basi utekelezaji unaanza.
Umemalizia kwa kusema tawala zetu zilivurunda. Sijui ni tawala zipi za nchi hii ambazo hazijavurunda. Tunawasubiri kizazi kipya mtuokoe.