Kesi ya kina Mramba: Serikali itashindwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kina Mramba: Serikali itashindwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Aug 16, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Endapo kilichoambatanishwa ndiyo mashtaka dhidi yao basi tujue kazi ipo mbele yetu. Serikali itadaiwa mabilioni na tutakuwa tumechezea akili za watu na kupoteza heshima ya taifa!

  Viva, GoT, Viva wanasheria wetu mnaofungua mashtaka ya namna hii.

  Safari ni ndefu sana!

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa na kwa ajili ya uchaguzi 2010.

  Kesi itaisha baada ya hapo.

  Wenye akili wameshanielewa
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  FP,

  Wasiwasi wangu ni kuwa taifa hili linakoelekea si kuzuri kabisa. Kitakachotokea after 2010 si cha kutamani kutokea.

  Kuna mchezo unaoelekea kutokea ambao kamwe sitamani utokee... Believe me or not!
   
 4. Ex Spy

  Ex Spy Senior Member

  #4
  Aug 16, 2009
  Joined: Jan 15, 2007
  Messages: 139
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Tanzania: Shamba la bibi.

  Tutaendelea kuvurugwa tu akili, masikini Taifa langu
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mchezo gani Mkuu Invisible?
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Can I reserve my comment? Thanks...
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Mbona kesi zote ni hivyo hivyo? Wengine tulishasema mapema kuwa kesi hizi zimeandaliwa kushindwa. Watu walitaka mazingaombwe wamefanyiwa sasa wakiona mtu anakatwa kipande halafu anaunganishwa mwishoni mwa onesho kwanini wasishangilie tu!?
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Aug 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Wengine tulisemaga zamani kuhusu perception vs. reality. Hakuna ambacho sijakitarajia kwenye hizi kesi zinazohusu "vigogo mafisadi"...
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Invisible Mkuu huwa unanitisha sana. Huwa unadondoa na kudonoa vitu ambavyo baadae vinakuwa kweli. Sasa hii inanitisha sana. Nakumbuka siku umedondoa kidogo tu kuhusu wizi wa mabilioni NBC na kweli ikaja kuwa wazi, na hakuna kinachofanyika. I hope nchi yetu haitaingia kwenye uchinjachinja, ingawa that is what i see coming (kama 2010 itakuwa ovyo)!
   
 11. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,118
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Labda ufafanuzi wa kwanini kesi itafeli ungesaidia kidogo mkuu!
   
 12. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,206
  Likes Received: 3,620
  Trophy Points: 280
  Ingawa kwa sheria za TZ kesi iliyopo mahakamani haipaswi kujadiliwa kwa lolote lile;lkn huu utapeli wa kisiasa za serikali ya JK kwa watz ni too much mkuu Kang!

  Kesi waliyofunguliwa akina Mramba kwa msingi wa sheria zetu ni kesi hewa hasa walipofunguliwa mashtaka ya "kitoto ya matumizi mabaya ya madaraka yao"!

  Ieleweke kuwa kwa sheria za tz waziri wa fedha HANA MAMLAKA ya kusamehe kodi hadi anapopata baraka za baraza la Mawaziri,kwa hiyo Mramba aliruhusiwa kusamehe kodi na Rais na baraza lote la mawaziri likimjumuisha Rais wa sasa JK ambaye kipindi hicho alikuwa waziri wa Mambo ya Nje!

  Na kama kweli JK anataka kuwashikisha adabu akina Mramba kwa misingi ya utawala bora hasa kwa vile walikataa ushauri wa baraza la mawaziri basi awafungulie mashtaka mazito ya ulaji rushwa na wala sio mashtaka haya danganya toto ya matumizi mabaya ya ofisi!

  Anyways,kama tu Shafi Adam kwenye kitabu chake cha KULI aliposema"yana mwisho haya"na ipo siku watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka halali kwa yale waliyotufanyia!
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,643
  Likes Received: 21,854
  Trophy Points: 280
  Wakuu tumeshalia sana kuhusu huu utapeli wa kisiasa unaondelea hapa nchini. Hawa watu wataendelea kutuzuga na kutumaliza na sisi tumebaki kutumbua macho.
  TUCHUKUE HATUA GANI SASA? maana hata tukilia na kutoa machozi ya damu, jamaa ni wagumu.
   
 14. r

  rkili Member

  #14
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunashukuru ntie wenye taaluma ya sheria kuliona hilo, ila ni bora kuelezea wasiwasi wako ktk hili nasi mbumbumbu wa sheria tukaliona, hakika hata wengine waweza changia lakini hawalioni tatizo kama nilivyo mm
   
 15. r

  rkili Member

  #15
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunashukuru ntie wenye taaluma ya sheria kuliona hilo, ila ni bora kuelezea wasiwasi wako ktk hili nasi mbumbumbu wa sheria tukaliona, hakika hata wengine waweza changia lakini hawalioni tatizo kama nilivyo mm
  pizzaman
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ninyi mnauona upande Serikali (washitaki) tu. Tatizo kubwa naliona upande wa MAHAKAMA zetu hata kama serikali ingejitahidi vipi kwa upande wa ushahidi. Mahakama zetu zimeoza NJE NDANI.
   
 17. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kuandika juu ya wizi mdogo kubeba adhabu kubwa na wizi mkubwa kubeba adhabu ndogo au kuishia kuachiwa tu: www.jamiiforums.com/habari mchanganyiko/25827 mwizi wa kuku kuuawa ni halali kwa taratibu za tanzania

  "Nimefuatilia kesi mbalimbali za matukio ya wizi, na ufuatao ni muhtasari mfupi wa mtiririko:

  Ukiiba billion 40 - hakuna kesi, hakuna anayekufuatilia, unakuwa free man. Rejea suala la Kagoda.

  Ukiiba kati ya billion 3 - 20 Utafunguliwa kesi ambayo baadae utaachiwa kwa kukosa ushahidi au kukiukwa taratibu au itachukua muda mrefu hadi inasahaulika. Fuatilia kesi za Mramba na wenzake uone mwisho wake, rejea pia kesi ya ile nyumba ya balozi Italia na ya Nalaila Kiula.

  Ukiiba kati ya million 100 - 2.9 billion Utafunguliwa kesi na kuna uwezekano wa kufungwa kwa kifungo kisichozidi miaka mitano. Rejea kesi kama ya Kasusura.

  Ukiiba kati ya Million 10 - 100 kuwa na uhakika asilimia 85 wa kufungwa. Hizi ndizo kesi nyingi zilizo mikoani na wilayani.

  Ukiiba chini ya million 10 likely utapata adhabu kubwa zaidi maana mara nyingi hela hii ni kidogo ukianza kuhonga.

  Unaweza kuona basi kuwa kadri unavyoiba kidogo ndivyo adhabu inavyoongezeka. The lesser yo steal the more severe the penalty and vice versa. Hivyo kwa kosa dogo kama la kuiba kuku basi adhabu kali ni kuuawa!!

  Hata katika rushwa wanasema eti rushwa ndogondogo ni mbaya sana kuliko rushwa kubwakubwa - logically therefore wanachosema ni kwamba rushwa ndogo ibebe adhabu kubwa na rushwa kubwa ibebe adhabu ndogo".


  Hivyo kwa akina mramba kuachiwa sioni ajabu
   
  Last edited: Aug 17, 2009
 18. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ccm wanafanya ulaghai tu. Hakuna kesi hapo lazima washinde hao.
   
 19. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mwenye macho haambiwi Tazama...
  Tangu siku ya kwanza kesi hii ipoletwa kwa pilato ... niliandika hapa kwamba haitakuwa ya ushindi kwa serikali na kama ikija kuwa na ushindi kwa serikali , litakuwa jambo jema maana itaweka precedent ya hali ya juu itakayokuja kumgusa hata Mkulu maana yatakuja kuibuka mambo kama kutotimiza wajibu kikamlifu serikalini...
  Kesi yeoye in issue mbili.
  1. precedent kwa maana ya decided cases
  2. Sheria inavyosema bila ambiguity yeyoye ile.

  Hivyo yangu macho na ninawaombea mafanikio mema ili washinde na waiweke hiyo precedent ambayo tunaisubiria kwa hamu ya kufungwa kwa kutotomiza wajibu au kufungwa kwa kutofuata ushauri wa baraza la mawaziri...
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kesi hizi zilikuwa na malengo maalum.

  1. Kurudisha imani kwa wahisani ili misaada isikatwe.

  2. Kuwatuliza wananchi wenye hasira dhidi ya watawala kwa kisingizio " Sheria iachwe ichukue mkondo wake"

  Hata washitakiwa wenyewe wameishahakikishiwa kuwa hafungwi mtu wasiwe na wasiwasi Ili mradi serikali ya CCM ipo madarakani basi watalindwa.

  Kuhusu tufanye nini hakuna la kufanya jamaa wameshika kotekote kwenye makali wameshika nchani kwa glove na kuachia katikati na kwenye mpini wameushika imara ili tukidanganyika na kushika makali yaliyoachwa wazi wanaanchia ncha na kuvuta kwa nguvu. Cha kufanya ni kuchukua jiwe na kupiga kwa nguvu kwenye glove ili ncha ipenye. Na hii itafanyika kwa njia moja tu, nayo ni kuwakosesha usingizi. Katiba ibadilishwe, Tume huru ya uchaguzi ila haya hayaji kwa kuongea huku ukiwa ndani unakula udaga na kauzu. Mfano mzuri Kenya.
   
Loading...