Kesi ya jinai inayomkabili Yohana Rugembe na washtakiwa 20 yaendelea Mahakamani, Mashitaka yaongezwa kufikia 11

Kesi ya jinai inayomkabili Yohana Rugembe na washtakiwa 20 yaendelea Mahakamani, Mashitaka yaongezwa kufikia 11

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Kesi ya jinai inayomkabili Katibu Mkuu Mstaafu wa BAVICHA Taifa, Yohana Kaunya Rugembe, pamoja na washtakiwa wengine 20, imeendelea leo Ijumaa, Februari 6, 2026, katika Mahakama kwa hatua ya kusomwa kwa hoja za awali.

Mashitaka 2 yameongezwa na kufanya jumla ya makosa kuwa 11.Upande wa Jamhuri wameieleza Mahakama kwamba wanatarajia kuita jumla ya mashahidi 41 na vielelezo 18.Mahakama imepanga kuanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo Februari 12,/02/2026, Tarehe 17/02/2026 na tarehe 20/02/2026 kuanzia saa tatu Asubuhi.

Ikumbukwe kwamba Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka yanayohusishwa na vurugu zilizotokea wilayani Bunda, mkoani Mara, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Tukutane Bunda kwa tarehe zilizopangwa kwa wananchi tuliokaribu na viunga vya mahakama ya Wilaya ya Bunda.

Haki haijawahi kushindwa, inacheleweshwa tu!Asante wakili Massaba kwa kufika Bunda kwa ajili ya watuhumiwa!
 
Wassira anakubali kutumika na wazanzibar ambao hawana hata uchungu na bara!!

Unafiki umelimaliza hili taifa
 
Duh

Ujinga mzigo

Sisi watanganyika ni wajinga wa kutupwa
 
Back
Top Bottom