Kesi ya huyu mrembo imefikia wapi?

Kesi ya huyu mrembo imefikia wapi?

Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti

Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’

Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa,
hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Hayo ndio maelezo yaliyotolewa leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari…. kama una comment yoyote iandike hapa chini na itatufikia.
Sasa naanza kuamini maneno ya Mzee Kenyatta (kama inavyodaiwa) kuwa "Nyerere anatawala maiti"
Na kinachonijia sasa ni je:,
- Nyerere alikuwa mzima huku akitawala maiti!?
- Wanaotutawala sasa ni wako hai na sisi ndio maiti au sote ni maiti!?


 
Hivi kwanza mkuu, miss TZ iko chini ya wizara gani?? utamaduni na michezo ama??

waziri husika mpaka sasa hajasema chochote?

Dk.+Fenella+Mukangara,+Waziri+wa+Habari,+Vijana,+Utamaduni+na+Michezo.JPG


au huyu mama fenella mukangara anaona hayamuhusu sana haya mambo?

twende kilioni zake tu mi hoooi jaman
 
Lundenga anajibu maswali magumu lea majibu mepesi na us kitoto....
 
Hana umuhimu wowote kwenye jamii, hata akiwa na miaka 40 au 50 hawezi kuwa effect tofauti yoyote kwa nchi yetu, bora wambebe waende nae huko huko.
 
Nilisikia hako kabinti kana mtoto mkubwa tu.....sasa kama nikweli kwanini Kamati ya Miss Tanzania isibadili jina na kuwa Kamati ya Mama Mrembo Tanzania....

Alostahili ushindi wa kushoto au kulia ila wa kati ni majanga tu.
 
hivi sura hii walishindwa kujua kuwa huyu ni mama mtu mzima?
Kwa faida ya wengi umri huonekana kati ya pua,mashavu mkabala na mdomo kuna mifereji kadiri unavyozidi kuelekea utu uzima mifereji hukomaa.
Kwa umri aliodanganya hakupaswa kuwa na mifereji hiyo.
Mifereji ipi?,mbona kama wote wako sawa?,
 
waka 2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani wa Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi… kashfa na hata naona wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi, huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga? Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.
Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga
‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo’ - Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ – Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga

‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’ – Lundenga
Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Hayo ndio maelezo yaliyotolewa leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari…. kama una comment yoyote iandike hapa chini na itatufikia.
Mmmm.. fix fake. Lazima kutifua mzizi. Nchi nzima tutakubali huu upuuzi? Mambo kama haya lazima kukomeshwa kila mahali.
 
Hata wewe haujasoma ukipewa kitengo tyuu una kuwa na Vyeti vyote mambo ya magumashi
 
Lundenga anajibu maswali magumu lea majibu mepesi na us kitoto....

Bado najiuliza waziri anayehusika na haya mashindano ni nani? na yeye ni boya kama lundenga ama?

>kwa sababu kama hii ishu iko ndani ya wizara yake halafu anashindwa kusema hata 'a', basi ni boya tu!
 
Hata wewe haujasoma ukipewa kitengo tyuu una kuwa na Vyeti vyote mambo ya magumashi

kaka Benny, point yako mpaka sasa bado sijaielewa.

hebu andika huku ukiwa umetulia ueleweke. too fast is harmful.
 
Last edited by a moderator:
Aiseee huyu mdada ni mkubwa sana hata uso hauna mvuto jamani kama sio miss.Mie nahisi ana miaka 30 hivi
 
Halafu m naona picha zake za siku ya shindano at lst zina mvuto ukilinganisha nahizi za press conf.anaonekana mkubwa zaidi
 
Suala lake la umri wa kichina limekuwa gumzo sana ndani ya muda mfupi!

Nimeona taarifa yake bbc swahili nako wanamzungumzia juu ya sakata lake!

Hii nchi yetu karibu kila kitu kinaendeshwa kimagumashi magumashi tu!

1512615_869880529697280_7722168114407381555_n.jpg


This face at 18yrs! is this possible??

Kumbe ndio huyu miss Tanzania!!! nasikia tu watu wakilalamika,lakini mikono yake inaonyesha sio msichana tayari ameshakuwa bi mkubwa
 
amesema mwenyewe leo ana miaka 23 hana mtoto
 
Back
Top Bottom