Kesi ya Dk. Mahanga kupinga `ukihiyo’ yaahirishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Dk. Mahanga kupinga `ukihiyo’ yaahirishwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 15, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,394
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Dk. Mahanga kupinga `ukihiyo’ yaahirishwa

  Imeandikwa na Flora Mwakasala; Tarehe: 14th January 2011 @ 23:20

  MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imeahirisha kesi ya madai ya kulipwa Sh bilioni moja iliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, mpaka Februari 24 mwaka huu itakapotajwa tena.

  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Esther Mwakalinga aliahirisha kesi hiyo jana baada ya Mahanga kudai kuwa hatakuwepo mahakamani hapo kwa kuwa amesafiri kwenda Dodoma.

  Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea alifungua kesi akidai kulipwa zaidi ya Sh bilioni moja na mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli kutokana na kumtaja kwenye orodha ya mafisadi wa elimu.

  Kwa mujibu wa Jalada la kesi hiyo, Februari 7 mwaka jana Msemakweli alidaiwa kuwa aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuzindua kitabu alichokiandika ambacho
  Mahanga anadai kuchafuliwa jina lake kwa kuandika habari za uongo dhidi ya taaluma yake.

  Katika mkutano huo Msemakweli alidaiwa kutumia kikao hicho alichoitisha kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu chake cha jina la ‘Mafisadi wa Elimu Toleo la Kwanza kumchafua jina Mahanga.

  Katika ukurasa wa mbele wa kitabu hicho anadaiwa kuweka picha ya Mahanga na katika ukurasa wa 12, 13, 14 kulikuwa na picha nyingine huku kukiwa na taarifa na maelezo ya uongo ikiwa ni pamoja na kueleza jinsi Mahanga alivyoghushi vyeti vya elimu ya juu.

  Aidha katika ukurasa wa 14 katika aya ya pili na tatu kulikuwa na baadhi ya maneno yanayosomeka kama, ‘Ufisadi wa Mahanga...Pia kwenye Fedha za Umma.”

  Mbali na kudaiwa kughushi vyeti vya elimu pia Mahanga anadaiwa kuchukua fedha za umma kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kuzitumia kwa ufisadi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,394
  Trophy Points: 280
  Anayemfahamu mdaiwa amshauri aiombe mahakama iifute hiyo kesi kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi zinazozidi madai ya Tshs 100- 150 Milioni.........................Huo ni ushauri wa bwererere......mbali ya kuwa tumechoshwa na viongozi wa umma ambao hukimbilia mahakamani kutishia raia na madai ya mabilioni.........................
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je niharali kwa kesi kuahilishwa mara 24 bila sababu maalum?

  NIPASHE INARIPOTI KUWA:
  Hata hivyo, Hakimu Mwakalinga hakufafanua iwapo Dk. Mahanga yuko kikazi, au anakabiliwa au kuzuiwa na kitu gani mkoani Dodoma hata ashindwe kufika mahakamani jana, zaidi ya kuishia tu kutamka kwa kifupi kwamba, "yuko Dodoma".

  Pia hakimu huyo hakueleza alipokea kwa njia gani taarifa ya Dk. Mahanga ya kuwapo kwake Dodoma.
  Bila kufafanua mambo hayo, Hakimu Mwakalinga aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 22, mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa. Hii ni mara ya 24 kesi hiyo kuahirishwa tangu ianze kutajwa mwaka jana.
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hapo patamu.... na naomba wadau tufatilie hii kesi mpaka mwisho wake asije akaimaliza kinyemelea.... na akiamua kuifuta wananchi tufungue kesi kutaka kujua ukweli wa elimu yake...., na kama ni kweli amegushi basi ashitakiwe
   
Loading...