Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,411
- 7,306
NIMEIOKOTA SEHEMU: Kuna sababu za msingi hapa serikali ishaurike!Huyu ameshauri hivi:
Huenda uchunguzi wa madini ndani ya mchanga ukaishia kuwa swala la JPM kutafuta sifa tu na usiwe na manufaa kwa umma kwa sababu zifuatazo:
1. Acacia kama ilivyo migodi mingine Tanzania ni mali ya wawekezaji na siyo mali ya serikali maana stahili ya serikali ni asilimia 4 tu ya thamani ya madini yanayochimbwa. Serikali kufungua container za acacia na kuchukua sampuli bila kuwashirikisha acacia ni kosa.
2. Sampuli za mchanga zilizochukuliwa na kaati ya rais zimepimwa kwenye maabara bila uwakilishi wa acacia na ni kosa maana tayari acacia wamesema hawatambui huo uchunguzi na kwa hivyo serikali haiwezi kutumia matokeo ya ripoti hiyo kudai fidia mahali po pote.
3. Mikataba kama huo wa acacia inapotokea kutoelewana mahali pa kutafuta suluhu ni mahakama ya kimataifa ya usuluhishi na mahakama hiyo pia haitatambua matokeo kwenye ripoti ya kamati ya rais. Mahakama utatumia ripoti ya SGS maana inatambulika kimataifa au serikali ikikataa ripoti ya SGS mahakama itateua chombo kingine huru cha kimataifa kurudia uchunguzi wa mchanga kwenye container. Kama vipimo vya kiasi cha madini kwenye mchanga kitafanana na zile za SGS basi serikali ya Tanzania itabwagwa chini na acacia na kutakiwa kulipa gharama za kufidia kwa acacia.
4. Kuna uwezekano pia acacia wakasema mchanga kwenye container siyo wa kwao maana serikali imefungua container bila wao kuwepo na kupelekea uwezekano wa mchanga wao kutolewa na serikali kuweka mchanga mwingine.
5. Kwenye sakata hili uwezekano mkubwa ni serikali kupoteza na siyo kupata. Mikataba ya kimataifa inahitaji weledi na wala siyo mihemko ya kisiasa na ubabe wa serikali.
Mkinga mkinga