Kesi ya ACACIA

Kesi ya ACACIA

vyovyote iwavyo!! jambo la msingi ni kwamba tumegundua kuwa mkataba wa accacia ni wa kinyinyaji na wizi. Naunga mkono juhudi za JPM hata kama tukitakiwa kulipa fidia, ni sawa tu.
Siyo kila mfungwa alitenda kosa!!

Yaani ndo umegundua leo wakati wagonga meza na wapyuyukaji wa ccm kwa ujinga wao walihakikisha tunafika hapa tulipo!
 
vyovyote iwavyo!! jambo la msingi ni kwamba tumegundua kuwa mkataba wa accacia ni wa kinyinyaji na wizi. Naunga mkono juhudi za JPM hata kama tukitakiwa kulipa fidia, ni sawa tu.
Siyo kila mfungwa alitenda kosa!!
Hapo umeona juhudi gani?Unaweza ukawa unasukuma ukuta na jasho likakutoka kweli kweli ila mwisho wa siku work done = 0
 
Tatzoa la mkulu anapenda misifa ya kjnga sana
 
Hata msichana wa Kazi za nyumbani anapoacha Kazi na kurudi kwako usipomkagua kwenye begi lake LA nguo unaweza ukagundua ameondoka na chupi za mkeo au za watoto wako. Eti makonteina ya madini ya accacia yaondoke yasikaguliwe wala kuchunguzwa kwa kuwa eti wana mikataba, kama si ulofa ni nini? Hii nchi bhana ina majuha wengi tena wanajifanya wasomi. Wamesoma kwa ajili ya kuwatumikia na kuwathamini mabwana zao wazungu siyo kwa ajili ya maendeleo yao na ya nchi yao. Ulofa mtupu
 
MDAs haitoi fursa kwa mwekezaji kuwa dishonest! Kesi imefungwa, safari imefika mwisho wa reli (Mabamba).
 
NIMEIOKOTA SEHEMU: Kuna sababu za msingi hapa serikali ishaurike!Huyu ameshauri hivi:
Huenda uchunguzi wa madini ndani ya mchanga ukaishia kuwa swala la JPM kutafuta sifa tu na usiwe na manufaa kwa umma kwa sababu zifuatazo:

1. Acacia kama ilivyo migodi mingine Tanzania ni mali ya wawekezaji na siyo mali ya serikali maana stahili ya serikali ni asilimia 4 tu ya thamani ya madini yanayochimbwa. Serikali kufungua container za acacia na kuchukua sampuli bila kuwashirikisha acacia ni kosa.

2. Sampuli za mchanga zilizochukuliwa na kaati ya rais zimepimwa kwenye maabara bila uwakilishi wa acacia na ni kosa maana tayari acacia wamesema hawatambui huo uchunguzi na kwa hivyo serikali haiwezi kutumia matokeo ya ripoti hiyo kudai fidia mahali po pote.

3. Mikataba kama huo wa acacia inapotokea kutoelewana mahali pa kutafuta suluhu ni mahakama ya kimataifa ya usuluhishi na mahakama hiyo pia haitatambua matokeo kwenye ripoti ya kamati ya rais. Mahakama utatumia ripoti ya SGS maana inatambulika kimataifa au serikali ikikataa ripoti ya SGS mahakama itateua chombo kingine huru cha kimataifa kurudia uchunguzi wa mchanga kwenye container. Kama vipimo vya kiasi cha madini kwenye mchanga kitafanana na zile za SGS basi serikali ya Tanzania itabwagwa chini na acacia na kutakiwa kulipa gharama za kufidia kwa acacia.

4. Kuna uwezekano pia acacia wakasema mchanga kwenye container siyo wa kwao maana serikali imefungua container bila wao kuwepo na kupelekea uwezekano wa mchanga wao kutolewa na serikali kuweka mchanga mwingine.

5. Kwenye sakata hili uwezekano mkubwa ni serikali kupoteza na siyo kupata. Mikataba ya kimataifa inahitaji weledi na wala siyo mihemko ya kisiasa na ubabe wa serikali.

Mkinga mkinga

Asante mkuu kwa kulisema hilo wengine tuliongea humu tukaitwa majina yote mabaya pamoja na kuambiwa kua sisi sio wazalendo, wataalam wa vita wote duniani wanakubaliana katika jambo kubwa moja ambalo nikwamba kabla hujaingia vitani ni lazima uwatumie intel kumsoma adui pamoja na kumjua nguvu alionayo na ukiona kama kama atakushinda hapo ndio unaangalia nini cha kuchagua war of necessary au war of choice, sasa hii waliotuingiza ni vita ya kuchagua haikua ya lazima kwakua sisi ndio tunaenda kuathirika,,,,,,
busara bilistahili kutumika na pia nasisitiza walioiuza ardhi yetu pamoja na madini yetu bado wapo hai wnakula mabilioni yao kiulaini.....
ilikuaje akina chenge watengeneze mikataba ya namna ile? kuna nini hapo limefichwa? ilikuaje mkapa akubalie na awape baraka zake kama mkuu wa nchi? hapo kuna mengi yamefichika.......
nasisitiza hii vita tumechokoza pabaya ni tofauti na kuteua na kutengua watumishi wa umma......

busara ilitakiwa kutumika intel yetu ilitakiwa izame kimya kimya na kuona madhara yake au faida zake kabla ya kufanya maamuzi hayo as if tunaishi katika kisiwa ambacho kimejitenga na ushirikiano wa imataifa pamoja na mikataba mbalimbali ambayo serikali yetu imeridhia na kusaini.....
sasa tusubiri nini kitatokea....

nasisitiza kua wayahudi hua wanafanya mambo yao kimya kimya na kuwa attack enemies wao by surprise misri pamoja na warabu woote wanajua nini kilitokea katika ile vita ya warabu na waisrael, muyahudi alishinda vita hiyo tokea siku ya kwanza......
Peter munk ni mlezi na co founder wa zionist na mosad ana blood line ya Theodore herz amabae alipewa jukumu la kuilinda na kui hifadhi ramani ya nchin yao ya ahadi na ndio chanzo cha wao kuwapinga umoja wa mataifa baada ya kutaka kuwapeleka uganda then wakatumia mbinu na fitna za kila aina kurudi kwao mnamo mwaka 1949.
wayahudi wana amini katika umiliki wa madini na mafuta kama chanzo cha kuimiliki na kuitawala dunia.
hao akina roman abramovic na akina putin wote ni wayahudi na senior CIA officers hua hawafanyi maamuzi bila kuuliza msimamo wa tel aviv katika jambo hilo..
nasisitiza tumekurupuka na sasa tusubiri hukumu yetu.
 
Hii serikali ya ccm ni hatari saaaaana yaani walikula wakiwa gizani for many years, hivi sasa baada ya madini kuwa yanakaribia kuisha ndo wanakuja hadharani kujifanya kuwa wana huruma kwa wananchi!?

Tatizo walilitengeneza wenyewe, baada ya kuona kuwa wamefaidika vya kutosha ndo wanakuja kuomba support ya vipofu kuwa wawekezaji wanatuibia.

Mimi naamini kuwa kila anayesupport haya anayoyafanya JPM nayeye alifaidika na huu wizi uliofanywa kwa hisani ya ccm na wabunge wake!!!!!
 
sawa mtumwa wa ACACIA usiejitambua na genge lenu ombeni na kusali kwa nguvu ili ndoto yenu ya kuona tanzania inashindwa itimie
Wabunge wa upinzani walitoka nje Kipindi hizi sheria zinapitishwa ,mkawaona hawana akili, leo mnasema wamenunuliwa. Msiejitambua ni nyinyi tena hata huyo anayejifanya mzalendo No1 alikuwemo kwenye baraza, ni mnafiki tu
 
Yan asilimia nne?Mkapa amechangia sana kuliangamiza taifa hili
Hata kikwete naye ni wale wale maana alitoa asilimia tatu kuja nne,,,kweli nne useme ndio umelisaidia taifa kweli?hata mtoto mdogo kwa asilimia hizo anajua tunadhulumika
 
NIMEIOKOTA SEHEMU: Kuna sababu za msingi hapa serikali ishaurike!Huyu ameshauri hivi:
Huenda uchunguzi wa madini ndani ya mchanga ukaishia kuwa swala la JPM kutafuta sifa tu na usiwe na manufaa kwa umma kwa sababu zifuatazo:

1. Acacia kama ilivyo migodi mingine Tanzania ni mali ya wawekezaji na siyo mali ya serikali maana stahili ya serikali ni asilimia 4 tu ya thamani ya madini yanayochimbwa. Serikali kufungua container za acacia na kuchukua sampuli bila kuwashirikisha acacia ni kosa.

2. Sampuli za mchanga zilizochukuliwa na kaati ya rais zimepimwa kwenye maabara bila uwakilishi wa acacia na ni kosa maana tayari acacia wamesema hawatambui huo uchunguzi na kwa hivyo serikali haiwezi kutumia matokeo ya ripoti hiyo kudai fidia mahali po pote.

3. Mikataba kama huo wa acacia inapotokea kutoelewana mahali pa kutafuta suluhu ni mahakama ya kimataifa ya usuluhishi na mahakama hiyo pia haitatambua matokeo kwenye ripoti ya kamati ya rais. Mahakama utatumia ripoti ya SGS maana inatambulika kimataifa au serikali ikikataa ripoti ya SGS mahakama itateua chombo kingine huru cha kimataifa kurudia uchunguzi wa mchanga kwenye container. Kama vipimo vya kiasi cha madini kwenye mchanga kitafanana na zile za SGS basi serikali ya Tanzania itabwagwa chini na acacia na kutakiwa kulipa gharama za kufidia kwa acacia.

4. Kuna uwezekano pia acacia wakasema mchanga kwenye container siyo wa kwao maana serikali imefungua container bila wao kuwepo na kupelekea uwezekano wa mchanga wao kutolewa na serikali kuweka mchanga mwingine.

5. Kwenye sakata hili uwezekano mkubwa ni serikali kupoteza na siyo kupata. Mikataba ya kimataifa inahitaji weledi na wala siyo mihemko ya kisiasa na ubabe wa serikali.

Mkinga mkinga
Yote ndio kama hivyo yametokea. Ushauri gani unatoa kwa SERIKALI yetu?
 
Umeongea swala kubwa sana
Kuhusu kufungua serikali imekosea bila kuwashirikisha jamaa maana watasema serikali ilianua ongeza kiwango chao wenyewe
Wakibisha tutafungua wakiwepo,,,,,na swala la kusema watakataa kuwa sio kontena zao amaa tutafurahi,,maana wooote utakua wetu huo mchanga/maknkia
 
Hivi wewe ni Mtanzania Kweli??????????? Inasikitisha Sana
Hii hasara ndio mmeijua leo?

Huu uchungu ndio mnausikia leo?

Leo ndio mmkekuwa watanzania?

Wakati wapinzani wakihoji mambo haya si mlikuwa mkiwapinga?

Uchungu ni baada ya Magu kuongea na si Zitto wala Lissu?

Msitufanye wajinga bora mkaomba radhi kwa hii hasara mlitusababishia.
 
Back
Top Bottom