Kesi ya ACACIA

vyovyote iwavyo!! jambo la msingi ni kwamba tumegundua kuwa mkataba wa accacia ni wa kinyinyaji na wizi. Naunga mkono juhudi za JPM hata kama tukitakiwa kulipa fidia, ni sawa tu.
Siyo kila mfungwa alitenda kosa!!
Ni mikataba wa uwizi aliyoingia Mwekezaji ACACIA na nani sijui..maana wauita mkataba wa ACACIA wakati ni mkataba wa uwekezaji umeridhiwa na pande zote yaani Serikali na wao. Acha mahaba kaka jaribu kuwa msomi na sio mwanasiasa.
 
Hiyo nia njema ya kushusha bei ya hisa za acacia London si ndio?
Nia njema ya kuhakikisha tanzania inapata inachostahili.
Wewe unaumia kushuka kwa hisa kuliko kufurahia jitihada za kutafuta kama Kuna pesa yako huwa inaibiwa.
Hakuna namna
 
Kwa sababu zoezi lilikuwa la Nia njema, na data kama zinaaminika. Bado wanaweza kufungua makontena mengine wanafanya chukua sample upya kwa kushirikiana au kwa uwepo wa acacia na SGS representative.
Yale majibu ya kwanza yatabaki kama serikali ilitaka kujilidhisha na nadhani wana haki hiyo ila haya ambayo yatafanyika mbele ya waangalizi wote ikiwezekana waongezeka muwakikishi kutoka kwa mnunuzi smelter na mwingine independent.
Kwa kufanya hivyo na kama tume yetu inauhakika acacia wakiwa wanaiba watakamatwa tu bila hata ya kwenda mahakamani.
Hii ndio suluhu ya kudumu...
Hivi ndio nilitarajia ungekuwa waleta mada za namna hii hapa Jukwaani. Wote tunamuunga mkono Mh. Rais kwa jitihada zake nzuri lakini ziwe zinazingatia natural justice. Imani ya Rais hata kabla hajachukua form ilikuwa ni sisi kuibiwa madini na wawekezaji. Basi angetafuta ukweli kupitia mikataba kama vile kubaini vipimo vinavyopunguza aina za madini na uwingi wa madini katika makinika na kuunda tume kama ya Prof Mruma ishirikiane taasisi huru za kimataifa kubaini ukweli wenye uwakilishi wa pande zote..mwekezaji na serikali. Kwa sasa serikali tu ina imetoa maoni yake bado wawekezaji wanahisi wako sahihi. Vyema tubalance story tuwashitaki na kuwaadhibi kwa haki.
 
NIMEIOKOTA SEHEMU: Kuna sababu za msingi hapa serikali ishaurike!Huyu ameshauri hivi:
Huenda uchunguzi wa madini ndani ya mchanga ukaishia kuwa swala la JPM kutafuta sifa tu na usiwe na manufaa kwa umma kwa sababu zifuatazo:

1. Acacia kama ilivyo migodi mingine Tanzania ni mali ya wawekezaji na siyo mali ya serikali maana stahili ya serikali ni asilimia 4 tu ya thamani ya madini yanayochimbwa. Serikali kufungua container za acacia na kuchukua sampuli bila kuwashirikisha acacia ni kosa.

2. Sampuli za mchanga zilizochukuliwa na kaati ya rais zimepimwa kwenye maabara bila uwakilishi wa acacia na ni kosa maana tayari acacia wamesema hawatambui huo uchunguzi na kwa hivyo serikali haiwezi kutumia matokeo ya ripoti hiyo kudai fidia mahali po pote.

3. Mikataba kama huo wa acacia inapotokea kutoelewana mahali pa kutafuta suluhu ni mahakama ya kimataifa ya usuluhishi na mahakama hiyo pia haitatambua matokeo kwenye ripoti ya kamati ya rais. Mahakama utatumia ripoti ya SGS maana inatambulika kimataifa au serikali ikikataa ripoti ya SGS mahakama itateua chombo kingine huru cha kimataifa kurudia uchunguzi wa mchanga kwenye container. Kama vipimo vya kiasi cha madini kwenye mchanga kitafanana na zile za SGS basi serikali ya Tanzania itabwagwa chini na acacia na kutakiwa kulipa gharama za kufidia kwa acacia.

4. Kuna uwezekano pia acacia wakasema mchanga kwenye container siyo wa kwao maana serikali imefungua container bila wao kuwepo na kupelekea uwezekano wa mchanga wao kutolewa na serikali kuweka mchanga mwingine.

5. Kwenye sakata hili uwezekano mkubwa ni serikali kupoteza na siyo kupata. Mikataba ya kimataifa inahitaji weledi na wala siyo mihemko ya kisiasa na ubabe wa serikali.

Mkinga mkinga

Hata mseme nini....tunachotaka ni ukweli kuhusu uchimbaji madini hapa nchini tz.

T 2017 JPM
 
vyovyote iwavyo!! jambo la msingi ni kwamba tumegundua kuwa mkataba wa accacia ni wa kinyinyaji na wizi. Naunga mkono juhudi za JPM hata kama tukitakiwa kulipa fidia, ni sawa tu.
Siyo kila mfungwa alitenda kosa!!
Mawazo kama haya yatapelekea tuwaachie hata hio 4% maana gharama za fidia nazo zitatushinda.
tutumie akili jamani
 
Nia njema ya kuhakikisha tanzania inapata inachostahili.
Wewe unaumia kushuka kwa hisa kuliko kufurahia jitihada za kutafuta kama Kuna pesa yako huwa inaibiwa.
Hakuna namna
Hio nia njema inaweza hata isifae kama misingi ya kutatua tatizo inapuuzwa. Sisi sio wakenya au useme ni wasomali kiasi kwamba hatupendi nchi inufaike na dhahabu, tunataka tusipoteze tena kwa namna ile ile ya kizamani kwa kutotimiza matakwa ya kisheria na ya kimikataba.
 
Mbona unazunguka ubuyu......nani kakwambia serikali inataka fidia,,,,,,,,,serikali ilitaka kujiridhisha ili ipate pa kuanzia sasa ushajua mipango ya serikali??????? Rais kishasema ripoti ya pili ndo itategemea nini ifanye kuhusu mikataba......kama nyerere alivunja mikataba itakua sasa isivunjike......jk tu alivunja mkataba wa reli walimpeleka wapi?????
Kwa kukusaidia hakuna muwekezaji huwa anatafuta vita na nchi alowekeza......
Sasa itaanzia wapi kama ripoti haitatambulika kimataifa? Hivi tunadhani mikataba ya kimataifa ni kama amri za Rais kwa wateule wake? Noo
 
Wangefukuza tu ii acacia,..INA gharama kubwa
Mkuu kwenye mambo ya mikataba hufukuzi tu unapoamua kumbuka mtu kasainishwa mkataba tena mkiwa na akilo timamu so ukivunja kwa sababu ya mihemko mwenzio anakimbilia mahakamani kufungua kesi ya madai....... hapo mkataba utakuwa umevunja ila mapesa utakayomlipa ni sawa na faida kma angechimba mgodi wako kwa miaka 5!!!
 
Back
Top Bottom