Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,808
- 11,973
Kesi namba 458 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kuendesha mtandao bila kutumia Kikoa cha do.TZ na Kuzuia Upelelezi wa Polisi imeendelea leo Agosti 1, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.
Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Daisy Makakala huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala mbele ya Hakimu Huruma Shaidi.
Wakili wa Jamhuri, Daisy Makakala ameiambia Mahakama kuwa shauri hilo lilikuwa mbele ya Mahakama kwa ajili ya kusikilizwa lakini kutokana na kukosekana kwa shahidi wao wa mwisho, Tully Esther Mwambapa ambaye yupo nje ya mkoa, anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa kwa shauri hilo.
Upande wa Utetezi ulikubali kuahirisha shauri hilo lakini pia Wakili Kibatala amesema upande wa utetezi hawawezi kupinga sheria za nchi hivyo aliiomba Mahakama imtake Wakili wa Jamhuri kuleta shahidi wao huyo wa mwisho ili shauri hilo lisikilizwe na kuisha.
Shauri hili limeahirishwa tena hadi Agosti 26, 2019 huku upande wa Jamhuri ukisisitiza kuwa utajitahidi shahidi wao afike siku hiyo
Katika shauri hilo lililofunguliwa Desemba 2016 na kuanza kusikilizwa Februari 2017, tayari mashahidi zaidi ya Watatu kutoka upande wa Jamhuri wameshasikilizwa na shahidi wa mwisho kusikilizwa ilikuwa mnamo Novemba 07, 2018.
Baada ya hapo shauri limekuwa likiahirishwa huku sababu kadhaa zikitolewa na kubwa ikiwa ni kukosekana kwa shahidi.
------
Kujua mashauri yote ya JamiiForums yanavyoendelea tembelea: Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums