Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums): Kwa mara nyingine tena Shahidi ashindwa kufika Mahakamani! Kesi yapigwa kalenda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,983
Kesi namba 458 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha do.TZ na Kuzuia Upelelezi wa Polisi iliendelea jana Mei 15, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Daisy Makakala huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Jebra Kambole mbele ya Hakimu Huruma Shaidi.

Wakili wa Jamhuri, Makakala aliiambia Mahakama kuwa shauri hilo lilikuwa mbele ya Mahakama kwa ajili ya kusikilizwa lakini kutokana na kukosekana kwa shahidi aliomba tarehe nyingine ya karibuni kwa ajili ya kusikilizwa kwa shauri hilo.

Sababu aliyoitoa Wakili Makakala ni kwamba shahidi aliyekuwa akisubiriwa kutoa ushahidi, Mkaribu Msaidizi wa Polisi kutoka Kitengo cha Uhalifu wa Mtandao Makao Makuu ya Polisi, Joshua Mwangasa amesafiri kikazi.

Baada ya maelezo ya Wakili wa Jamhuri, Wakili wa Utetezi Peter Kibatala aliutaka upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwani maelezo ya kuwa shahidi amesafiri si kweli. Alisema kuwa “Maisha ndio haya haya, marafiki ndio hawa hawa hivyo tunafahamu kuwa ASP Mwangasa hajasafiri.”

Alielezea kuwa kuendelea kusogezwa mbele kwa shauri hilo kila mara kuna waumiza Washtakiwa na kuzuia haki zao za msingi kwa maana hawawezi kusafiri na kuendelea na shughuli zao kwa amani

Wakili Makakala alimjibu Wakili Kibatala kuwa inawezekana anayosema yupo sahihi au haupo sahihi, lakini yeye alisema hayo kutokana na majibu ya shahidi baada ya kuwasiliana naye

Aidha, Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza pande zote mbele alieleza kuwa shauri hilo ni la siku nyingi tangu mwaka 2016 hivyo linatakiwa limalizike haraka. Pia alisema kuwa zamani mashahidi ambao ni Maaskari walikuwa wanaweza kwenda kukamatwa na kupelekwa Mahakamani yaani Mkuu wa Askari huyo anapekewa taarifa ya kumkamata

Lakini pia, itakumbukwa kuwa mara ya mwisho kwa shauri hili kusikilizwa mnamo Mei 9, 2019 upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Huruma Shahidi uliomba kuahisha shauri hilo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao

Baada ya hayo Hakimu Shaidi pamoja na Mawakili wa Upande wa Utetezi na Jamhuri walikubaliana kuahirisha shauri hilo hadi Juni 3, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom