Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa. Hakimu hajamaliza kuandika uamuzi mdogo(ruling)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Machi 13, 2018

Hata hivyo, shauri limehirishwa mpaka tarehe Aprili 09, 2018 baada ya Hakimu Simba kusema hajamaliza kuandika uamuzi mdogo (ruling) kutokana na kupata safari ya ghafla.

Siku hiyo ya kesi Hakimu Simba amesema itaanza kusikilizwa kuanzia saa 4:00 asubuhi na kuutaka upande wa Jamhuri kuja na mashahidi wao wa mwisho.

Kujua ilikotokea, soma Kesi namba 456: Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji mafuta bandarini, yaahirishwa mpaka Machi 1
https://www.jamiiforums.com/threads...-bandarini-yaahirishwa-mpaka-machi-1.1405188/
Pia soma kujua mfululizo wa Kesi za JamiiForums.com => Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums
 
Kwa hio hakimu akipata dharura huwa hajali kazi, kama na sisi tungekua tuna ahirisha majukumu ya kazi zetu kwa kisingizio cha dharura si kila kitu kingesimama?
ni kupotezeana muda tuu..

Pole sana Melo kwa kila changamoto unapitia one day yatapita haya yakibakia nyuma nawe umeendelea mbele.
 
Hizi kesi hazitakwisha leo wala kesho kwa kuwa serikali wanazitumia kama bargaining chip (hook) ya kutaka kuwapelekesha wamiliki wa mtandao pendwa wa JF!
 
Back
Top Bottom