Kesi na. 456 (Jamhuri v JamiiForums): Hukumu yaahirishwa kwa mara ya nne

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,805
11,964
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar imeahirishwa tena leo Februari 19, 2020 hadi Aprili 02, 2020.

Hukumu hii awali ilipangwa kusikilizwa Novemba 26, 2019 ikapangwa tena kutolewa Disemba 06, 2019 na baadae ikapangwa kutolewa Januari 22, 2020 na ikapangwa kuwa lazima leo Februari 19, 2020 hukumu ingetolewa saa 6 mchana.

Kesi hiyo leo imesikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar chini ya Hakimu Huruma Shaidi kwa niaba ya Hakimu Mwandamizi Thomas Simba anayeendesha kesi hiyo.





















Katika kesi hiyo, Washtakiwa wanatuhumiwa kutotoa ushirikiano kwa Jeshi Polisi walipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom.

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Faraji Nguka huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Wakili Benedict Alex

Hakimu Simba alitakiwa kutoa hukumu ya Kesi hiyo leo baada ya Upande wa Utetezi kumaliza kujitetea, lakini uamuzi wa hukumu katika kesi hiyo umeshindikana kutolewa kutokana na kwamba Hakimu hajamaliza kuandika hukumu hiyo

Wakili Nguka amesema, “Shauri hili lilikuja mbele ya Mahakama kwa ajili ya kusikiliza hukumu lakini hukumu haijakamilika kwa hivyo tunaomba siku nyingine kwa ajili ya kesi kuja kutolewa uamuzi”

Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 19, 2020 kwa ajili ya kutajwa tena huku akisema siku ya hukumu itakuwa Aprili 02, 2020
****

Kujua ilipotokea kesi hii, tembelea Kesi Na. 456 (Jamhuri v JamiiForums): Hukumu yaahirishwa hadi Februari 19, 2020 saa sita mchana

Kujua kinachoendelea kwenye kesi zote za JamiiForums, tembelea Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

ORIGINAL CHARGE SHEET

C0D6625C-51AB-4231-9D48-F07CB56E7FDC.jpeg


AMENDED CHARGE SHEET

8E276AFB-657C-4299-A9BF-6A96D123E15D.jpeg


Charge-sheet mpya ilibadilishwa Novemba 2017 > Kesi dhidi ya JF: Mahakama ya Kisutu yabariki Jamhuri kubadilisha hati ya mashtaka! Ni kesi ile ya Oilcom - JamiiForums
 
Mtu kawasaidia kutoa taarifa za ufisadi badala ya kufatilia mjue ukweli, kuokoa mabilioni ya fedha zinazopotea mnajitahidi kuzima chanzo cha taarifa!

Kuna haki na kweli hapa Tanzania? ESCROW watu wamepiga fedha nyingi wako mitaani wanakula bata, wasemaji wawananchi wote wanabambikwa kesi mahakamani, haki iko wapi kuzima ukweli?

Watanzania ni misukule wamelala hawaoni ukweli? Watu wananunuliwa eti wamehama rushwa itaisha kwa jinsi hiyo?

Mungu tuokoe na hili jinamizi, maana wewe hulali wala hununuliwi unasimama ktk haki ili watoto wetu wawe na maadili mema!!
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa Hukumu ya kesi inayomkabili Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo kutokana na Hakimu anayeendesha shauri hilo kutohudhuria mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu leo ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye anasikiliza shauri hilo amepangiwa majukumu mengine, kesi imeahirishwa hadi Aprili 2, 2020 kwa ajili ya hukumu.

Melo yupo nje kwa dhamana na kwa mujibu wa kisheria kesi inayomkabili mshitakiwa huyo haruhusiwi kutoka nje ya mipaka bila ruhusa maalumu ya mahakama, Katika kesi hiyo mbali na Mello, mshitakiwa mwingine ni Mackie William.
(📹 via @ayotv_)
 
Natabiri pamoja nakuwa na kesi ambayo imemtesa Zaid ya miaka minne ila at last Maxence Melo atakuwa hana kesi nakuendelea na kazi yake.

Haki yake itachelewa ila ataipata mchana kweupe.

Wapo watu wanasifu ujasiri wa mtu alitoa taarifa ikasaidia kugundulika ujambazi wa mafuta.

Pia na imani Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaona kile kinaendelea na atatenda haki kwa Kijana huyu.
amen
 
TumainiEl,
Mkuu Tumaini, ufafanuzi tu kidogo wa kisheria, kesi za jinai zina stages mbalimbali, hiyo stage ya hana kesi ya kujibu, inaitwa commital procedure, kesi ya Max imeishavuka stage hiyo, alikutwa ana kesi ya kujibu na kesi imeendeshwa kwa kusikilizwa na mashahidi wakaitwa.

Hapa sasa tuko kwenye stage ya mwisho ya hukumu, stage hii haihitaji utabiri ni kuingilia uhuru wa mahakama, bali inahitaji maombi, Max kukutwa hana hatia.

P
 
Pascal Mayalla , kipi kinapelekea kesi kuchukua muda mrefu namna hii? Je, ni uwezo wa mahakama zetu mdogo? Kitengo cha kukusanya ushahidi kimeelemewa na mahitaji, au kesi zinaendeshwa huku maamuzi yakiwa tayari yameshafanyika (hukumu inatoka kabla ya kesi kusikilizwa)?

Takriban miaka minne hata kama itaamuliwa washtakiwa hawana hatia, lakini wameshaathirika kisaikolojia, kijamii na zaidi kiuchumi.

Nafikiri umependekeza jambo jema, tuendelee kuliombea hili jambo liwe na mwisho mwema.
 
The Monk,
Mkuu The Monk, kwanza swali lako hili lime ni inspire kuandika kitu kuhusu justice system yetu, kiukweli justice system yetu ina matatizo, justice delayed is justice denied, kuna yule wakili wa Arusha, Medium Mwale, amekaa mahabusu miaka 8!.

Kina Kitilya, Sio na Shose, huu ni mwaka wa 4!, kesi yenyewe ni ya banking transactions, transactions zote za bank dunia nzima, zinafanywa kwa maandishi, hivyo huo uchunguzi unaochukua miaka 4 ni uchunguzi gani?.

Tukisema serikali yetu haina uwezo, tunanyooshewa vidole kuwa tuna chuki!.

All and all, hili la mateso ya watu kukaa mahabusu vipindi virefu, litampatia sana baraka rais Magufuli, watu wanateseka bila sababu, tena tunapaswa kuzifumua sheria zetu hata kesi za manslaughter watu wapewe dhamana, kama Ditopile aliua kwa 1st degree murder na akapewa dhamana, why only him and not others?. Mtu kama Rugemalila, 75 years old, mwenye assets za billions, anaweza vipi kutoroka nchini kwa kesi ya bilioni 300 wakati anadai ma trilioni?.

Kama majizi ya EPA yalisamehewa na kutakiwa kurejesha walichokwapua bila hata kufikishwa mahakamani, iweje mwizi wa kuku afungwe miezi 6 jela?.

Wito kwa DPP: Japo ni Ushauri wa Rais kuwasamehe, Tafadhali tumia ...
Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji ...
Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever ...
P
 
Back
Top Bottom