Wakili wa Jamhuri akwamisha kuendelea kwa Kesi ya JamiiForums

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,745
11,872
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar, imekwama tena kuendelea na utetezi, Septemba 24, 2019

Sababu iliyokwamisha kesi kuendelea ni kutokana na Wakili wa upande wa Jamhuri aliyekabidhiwa shauri hilo kushindwa kufika Mahakamani kutokana na kupata udhuru

Hakimu ameomba taratibu zote kukamilishwa ili mpaka Oktoba 15 kesi iwe imekwisha kwasababu imeshaenda kwa muda mrefu. Baada ya kusema hayo aliahirishwa kesi mpaka Oktoba 7

Kesi hii inasikilizwa chini ya Hakimu, Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Candid Nasua na upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala

Aidha, katika shauri hilo Washtakiwa wanatuhumiwa kutotoa ushirikiano kwa Polisi walipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika taarifa kuhusu Oilcom

zaidi, soma;


 
Upelelezi haujakamika... Katika karne hii TZ upelelezi unatakiwa ujikamilishe wenye.
 
Kama kuna jambo linanipaga shida sana kuelewa kuhusiana na RUSHWA au kupigwa VITA rushwa nchi hi basi ni juu ya vita inayopata JF, mfano ni hi case; nilidhani vyombo vya dola hasa police, Takukuru and may be TISS wangeifanya JF kua moja kati ya sources zao za information but badala yake inapigwa vita. Najiulizaga sana kuhusu kesi hi na swala la hiyo habari ya huko bandarini, anyway, labda tutafika huko tuendako siku moja
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom