Kesi namba 456 (Jamhuri v JamiiForums): Kwa mara nyingine Wakili anayehusika na Kesi apata dharura! Kesi yapigwa kalenda..

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar, imetajwa tena leo Aprili 18, 2019

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Candid Nasua huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Jebra Kambole na Jeremiah Mtobesya mbele ya Hakimu Thomas Simba.

Wakili wa Jamhuri, Nasua ameiambia Mahakama kuwa shauri hilo lilikuja mbele ya Mahakama kwa ajili ya upande wa utetezi kuanza kujitetea lakini yeye sio Wakili anayehusika na shauri hilo.

Wakili anayehusika na shauri hilo amepata dharura, hivyo Wakili Nasua ameomba siku nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.

Washtakiwa wanatakiwa kuanza kujitetea baada ya kukutwa na kesi ya kujibu kwenye shauri hilo mnamo Mei 16, 2019.

Wakili wa Utetezi na Jamhuri pamoja na Hakimu wamekubaliana kuahirisha shauri hilo hadi !Aprili 18, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.

Kujua namna kesi hiyo iliyokuwa mara ya mwisho Machi 19, 2019 soma


Kujua yanayotokea kwenye kesi zote zinazohusiana na Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums na Mwanahisa mwenzake, Micke William, soma

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom