Kesi dhidi ya Mbowe: Ushahidi wa Luteni Denis Urio ni muhimu sana

Hebu acheni kumislead watu, hawa watuhumiwa walishafutwa na JWTZ wakati wanakamatwa, harafu hii kesi bado inaendelea na Mbowe inaweza ikamfunga vilevile kwa makosa anayoshitakiwa nayo. Wasingekuwa na ushahidi na kesi iliyosimama wasingeanza kusikiliza kesi, wangeipiga kalenda tu wakisema upelelezi haujakamilika, indefinitely!
Sasa mashahidi ndio hao wakina king, haiwaijui hata PGO mmmh labda.
 
Hii kesi inaleta misuguano isiyo ya lazima kati ya Jeshi la police vs JWTZ, Chadema VS serikali, Chadema vs Police, CCM vs JWTZ.

Fikiria moja ya mashahidi kwa upande wa utetesi wakawa wanajeshi kutoka huko ngerengere, je nini kitatokea baada ya kuwa wametoa ushahidi wao kuwatetea waliokuwa wenzao??? Serikali haioni tatizo kwenye hili??
 
Je huyu Moses hana ndugu kama wapo waliwai kutangaza kupotea kwake, kifo chake? Kuna taarifa yoyote kutoka kwenye familia yake toka hii kesi ianze au kabla ya kesi kuanza?
Wakati wa mwendazake mbona ilikuwa ishu ya kawaida kutoweka Wala haikuhitaji kuripoti maana hata ukiripoti haisaidii.
 
Ndo mnavyojidanganya hapo ufipa? Kweli mmekosa akili nyie watu!

Inaelekea una umri mdogo sana! Uliza komando Tamimu alifanywaje na vyombo vya dola mwaka 1981 baada ya kuongoza jaribio la kutaka kumpindua nyerere?

Tanzania kwenye kudeal na wahalifu haijalishi wewe Nani wanakupa dozi tu!
Itashangaza kama MNYETISHAJI hatapanda kizimbani atujuze anayoyajua.
 
Swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???

Mkuu acha ujinga bana wewe ni mkubwa kuliko ulichouliza hapa.
 
Jeshi letu nalo ni la ovyo kweli. Unaachaje makomandoo wanaofundishwa kwa gharama kubwa wakasumbuliwe na hawa vinyamkera Polisi. Na hao makomandoo kuliko kukamatwa namna hiyo unakufa na mtu aisee. Unless mambo yote ni fictictious.

Endelea kupiga masta kwa picha za kuchora kwa penseli.
 
Acheni huu UPUMBAVU ndio maana mnaishi kwenye makwapa ya watawala sababu mna uwezo duni wakufikiri issue sio mtu kufungwa inatakiwa mtu afungwe kwa kesi ya kweli sio ule UPUMBAF mnafanya

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app

Nani aaminike sasa,polisi au mbowe anayelewa na kuanguka kisha kudai kavunjwa mguu na wasiojulikana kutoka ccm???

Matapeli wanapokutana chukua jembe ukalime.
 
Ila mama samia anaimgia kwenye mzego, wakifauli huu huu mtego nakuhakikishia utawala wake utayba kwa kiasi kikubwa sana
 
Ndugu zangu!

Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.

Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.

Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.

Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.

Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.

Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?

Urio yupo upande gani?

Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.

Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.

Ncha Kali.
Siro siku zake zinahesabika
 
Alikuwa upande wa watuhumiwa ila kichapo kimemgeuza shahidi wa jamhuri.
 
Hii kesi ikiendelea ni aibu kwa serikali na ikifutwa na DPP ni aibu kwa serikali. Aibu haikwepeki kwa serikali kwa njia yoyote ile, yani kunyoa au kusuka hawapendezi.

Pili, swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???.

NOTE THAT: Luteni Denis Urio ni bado mkufunzi jeshini, yupo active kama mwanajeshi wa JWTZ na hajasimamishwa kazi bado, na ndio police waliosema wameshamtupa baada ya kumalizana nae kumtekenya TAZARA POLICE STATION.

Tatu, swala la usalama wa washtakiwa na mashahidi kwa hatua ya hii kesi ilipofikia, hatua gani zimechukuliwa kuwa hakikishia wana usalama huko mahabusu walipo hifadhiwa na pindi wanapo safirishwa kwenda mahakamani?

Tumeona wakisafirishwa kwa gari bovu lililogoma kuwaka mahakamani, je ikitokea msafara wao nje ya mahakama au barabarani kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumiminiwa mzigo wa risasi ili kuficha aibu, hilo jambo litachukua taswira gani mbele ya dunia?

Swali la kizushi;

CDF wetu angekua ndio yule mwamba wa Guinea, bwana Kanali Mamady Doumbouya angekubaliana na mwenendo huu wa kuvunja katiba, kulinajisi jeshi la nchi kwa kuwateka Makomandoo na kuwafanya waliofanywa (Kupigwa, Kuteswa na Kuchomwa bisibisi za makalioni)?
Kwanza kumtesa kumpiga mtu kumlazimisha aseme kile ambacho hakikuwepo ni ukiukaji wa haki za binadamu, pili Polisiccm kwenda kuwapiga Asikari wa jwtz ni udhalilishaji mkubwa wa jwtz na watanzania kwa ujumla hasa ukizingatia hakukuwepo na Ugaidi wowote ule zaidi ya DC Sabaya kutengeneza mazingira ya kumtesa mbowe kwa lengo la kumfurahisha Magufuli kipindi hicho, Lt Urio aliombwa na mbowe amtafutie walinzi wa kawaida Yaani makomando wasitaafu kwa lengo la kujilinda dhidi ya hujuma za DC Sabaya ambaye kipindi kile alikuwa ni DC dikiteta Hatari, kipindi anawasiliana na Lt urio ambaye kiukoo ni ndugu yake mbowe alidukuliwa mawasiliano yake na ndiyo maana Lt urio na yeye alikamatwa na kuletwa Tazara kuteswa kudhalilishwa na Polisiccm ingawa sasa kingai na mahita waliomtesa wamemnunua aweze kuwa upande wao wakizani watanzania ni wajinga kiasi hicho, hii kesi yaweza kuwa ndiyo kioo cha kutambua madhara ya kutengeneza kesi za kubambikiwa pasipo kutafakari kabla
 
Ndugu zangu!

Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.

Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.

Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.

Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.

Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.

Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?

Urio yupo upande gani?

Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.

Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.

Ncha Kali.
Kupitia hii kesi watanzania wamejifunza vingi ikiwemo Polisiccm kuwatesa jwtz kienyeji kisha huyo huyo aliyeteswa kupigwa anakuja kuwa shahidi mahakamani , njaa mbaya Lt Urio anajidhalilisha na kulidhalilisha jwtz, kwa mateso aliyofanyiwa alipaswa awe amejiuzulu kazi na pengine hata kujinyonga kwa Aibu ya kupigwa kuteswa na Polisiccm ingawa sasa amejitoa fahamu anatoa ushahidi wa mchongo ambao unaenda kumletea Aibu zaidi badala ya faida
 
Back
Top Bottom