Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,384
- 26,733
Ndugu zangu!
Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.
Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.
Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.
Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.
Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.
Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?
Urio yupo upande gani?
Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.
Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.
Ncha Kali.