Kesi dhidi ya katiba mpya mahakama kuu

Kesi dhidi ya katiba mpya mahakama kuu

Kusema kweli ktk hili wala sijui maana nchi nyingine maamuzi ya mahakama kuu ndio ya mwihso lakini Tanzania kwetu sii lazima.. Kesi ya Mtikila kuhusu mgombea binafsi alishinda mahakamani lakini hakupewa haki hiyo..Sasa hapa unashindwa kuelewa kama tuna mihimili mitatu au kuna mmoja na mingineyo iko chini yake kama muungano wa Tanzania!
 
I had OK christmas and this made it waay better!. High Court ndiyo kimbilio la independent thinkers, we need to keep it really busy na siyo kuandamana. Te international community always looks at our High court decisions na ninajua huwa wako very careful.

Kuhusu mgombea binafsi, muungano ndiyo kikwazo kwa hiyo mahakama ilikuwa haina jinsi.
 
Ilkuwa appealed and nullified kama sikosei
 
Muungano ndio kikwazo kwa vipi mkuu nipe darasa. Je, unafikiri Libya, Egypt, Bahrain, Tunisia na Syria wangetumia mahakama zao wangeipata haki kuliko kufanya maandamano?..

Kumbuka utawala wa CCM ni wa Kidikteta hilo halina ubishi sasa inakwenda mahakamani ili utafute haki ipi ikiwa swala zima la kuunda Katiba Mpya halipo ktk katiba yetu!.ni sheria gani itatumika au mnategemea mahakama kuu itasema maadam swala hili halipo ktk katiba basi rais hana mamlaka hayo?..Nao wataulizwa kwa kutumia sheria gani?..maanake wenzetu wanayo mifano ya katiba ya mwaka 1961, 1964 na 1967.
 
Ilkuwa appealed and nullified kama sikosei
Hata sijakuelewa Muungano ndio ulifanya hivyo ama Utawala wenyewe..maana sielewi maamuzi ya rais yahusiane vipi na muungano? Hapa ndipo sikuelewa nataka kujua huo muungano ilihusika vipi ... ni ktk kutaka kuelewa mkuu wangu kesho niweze kuwa na kumbukumbu..
 
This is one case that I just can not wait to follow up minute to minute as it was just such long overdue.

Big up sana TLS pamoja na wanaharakati wengine vichwaa humo!!! Hii ndio njia ambayo serikali ilikua ikitamani tupite na swala la katiba mpya.

Hata hivyo ijulikane kwamba kwa kuwa CCM haikua na haja hata kidogo na katiba mpya, huu mgogoro wa kikatiba waliupanga makusudi na kujua wazi kwamba kesi zitafungulwa na KUWASAIDIA KUCHELEWESHA JAMBO HILI na hatimaye uchaghuzi mkuu mwingine kufanyika bila Katiba mpya.

Kwa misingi hiyo, harakati za kutafuta katiba mpya ziongezeke maradufu mwakani 2012 ili kuweka wananchi sawa kujiundia katiba baada ya kukipiga chini CCM na uongozi wake hata kabla ya uchaguzi unaofuatia.
 
Ni mwanzo mzuri,ingawa nina wasiwasi na uhuru wa mahakama zetu.
Muda utasema.
 
This is one case that I just can not wait to follow up minute to minute as it was just such long overdue.

Big up sana TLS pamoja na wanaharakati wengine vichwaa humo!!! Hii ndio njia ambayo serikali ilikua ikitamani tupite na swala la katiba mpya.

Hata hivyo ijulikane kwamba kwa kuwa CCM haikua na haja hata kidogo na katiba mpya, huu mgogoro wa kikatiba waliupanga makusudi na kujua wazi kwamba kesi zitafungulwa na KUWASAIDIA KUCHELEWESHA JAMBO HILI na hatimaye uchaghuzi mkuu mwingine kufanyika bila Katiba mpya.

Kwa misingi hiyo, harakati za kutafuta katiba mpya ziongezeke maradufu mwakani 2012 ili kuweka wananchi sawa kujiundia katiba baada ya kukipiga chini CCM na uongozi wake hata kabla ya uchaguzi unaofuatia.
Nakubaliana na wewe 100%... Katiba mpya itaandikwa na CCM mtake msitake japokuwa hiki ni kipimo kizuri sana cha katiba iliyopo.. Je, hii serikali itafanya maamuzi kama iloyafanya kwenye kesi ya mgombea binafsi - Nullify!.
 
Kesi kupinga Katiba Mpya yaiva
Monday, 26 December 2011 12:22
Fredy Azzah

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kimesema kimekamilisha mchakato wa kufungua kesi ya kikatiba, kupinga sheria ya mapitio ya katiba iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete, Novemba 29 mwaka huu.Rais wa chama hicho, Francis Stolla, aliliambia gazeti hili jana kuwa chama kinatengeneza hati ya mshtaka ambayo yatafunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, katikati ya Januari mwakani.

"Hii ni kesi ya kikatiba, haihitaji kutoa taarifa kwa Serikali. Tunatumia sheria ya haki za msingi na wajibu wa kutekeleza ya mwaka 1994," alisema alipoulizwa kama tayari walishaitaarifu Serikali kuhusu kusudio hilo.Kwa mujibu wa Stolla, kesi hiyo ni dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tumeunda kamati ya kushughulikia katiba, yenye wajumbe wanane. Kwa sasa wajumbe hao wako katika mchakato wa kuandaa hati ya mashtaka. Wakimaliza, tutateua mawakili watatu wa kuisimamia kesi hiyo mahakamani kwa niaba ya chama,” alisema Stolla.

“Kwa sababu sheria inasema ukitaka kishitaki serikali inabidi umushitaki Mwanasheria Mkuu, kwa hiyo tutafanya hivyo lakini kesi hii ni ya kikatiba na mlengwa wetu ni Bunge,” alisisitiza.

Alisema hatua ya kulishtaki inatokana na dhamana ya chombo hicho ya kutunga sheria. "Tunalishtaki kwa sababu sheria hiyo iliyoitunga ni mbovu,”alisema.

Stolla alisema sababu za kufungua shtaka hilo ni pamoja na sheria hiyo kukiuka katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Alitaja ibara zilizokiukwa kuwa ni pamoja na ile ya 18 inayowapa nafasi wananchi kutoa maoni yao na ibara ya 22, inayotaka wananchi washirikishwe kwenye masuala muhimu na yenye maslahi kwao.Kwa mujibu wa Stolla sababu nyingine ya kufungua kesi hiyo, ni sheria hiyo kukiuka taratibu za utungwaji wa sheria, ikiwa ni pamoja na kupitishwa na Bunge baada ya kusoma mara mbili, badala ya mara tatu kama inavyotakiwa kisheria.

“Mara ya kwanza walipowasilisha hati ya dharura bungeni, kelele zilipigwa kuwa iondolewe na utaratibu wa kutungwa kwa sheria hii uwe wa kawaida. Pia kutaka ule muswada uandikwe kwa lugha ya Kiswahili, mambo yale yalitekelezwa,”alisema.Alisema kuwa baada ya kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili ambayo Watanzania wengi wanaielewa, muswada ulipaswa kurudishwa kwa wananchi ili waujadili lakini jambo hilo halikufanyika.

“Siku ile wanasoma ule muswada wa Kiingereza kwa mara pili, waliusoma ule wa Kiswahili kwa mara ya kwanza lakini wakadai kuwa ni mara pili. Halafu wakaja kusoma tena mara ya pili na kuupitisha. Sheria inataka usomwe mara tatu, kwa hiyo ni wazi kuwa huu ulipitishwa baada ya kusomwa mara mbili badala ya mara tatu kama inavyotakiwa,”alifafanua Stolla.

Alisema sababu nyingine ni sheria hiyo kuwa na vipengele vinavyozuia watu au asasi nyingine nje ya tume itakayoundwa kuwaelimisha wananchi juu ya katiba.

Stolla alisema katika kifungu cha 22, sheria hiyo inaweka makosa ya jinai na adhabu kwa mtu ama taasisi, itakayofanya kampeni ya kuhamasisha juu ya katiba.

“Kwa sheria hii midahalo kama inayofanywa sasa hivi inaharamishwa, ni tume ya katiba mpya tu ndiyo itahamasisha kwa mikutano maalumu, kwa hiyo sisi tunadhani kuwa hali hiyo inanyima uhuru wa kutoa maoni,” alieleza.

Msimamo huo wa TLS unakuja siku moja tangu vyombo vya habari vimkariri Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Profesa Issa Shivji akiikosoa sheria hiyo kwa kile alichosema kuwa ni mbovu na haitazaa katiba bora.
Akichambua sheria hiyo, Profesa Shivji alikosoa kifungu cha 21 akisema kuwa kinashangaza kwani kinazuia hata watu kuikosoa sheria hiyo.

“Mimi nasema kuwa sheria hii ni mbovu, katika sheria hii, kifungu hiki kinanizuia hata kusema, sheria hii ni mbovu’. mimi sijui kulikuwa na fikra gani kuweka kifungu kama hiki, kitu kimoja tu ni kwenda mahakamani kuipinga,” alisema.

Akichambua kifungu kimoja baada ya kingine katika sheria hiyo, Profesa Shivji alisema imewatenga kabisa wananchi katika mchakato mzima wa kuandikwa kwa katiba mpya.

“Wananchi wanatakiwa kushirikishwa tangu hatua ya kwanza, kwa mchakato wa Bunge, yaani sisi wenyewe tumeshirikishwa kupitisha sheria hiyo kuhakikisha kuwa vyombo vyote vinavyohusika vinafuatwa.” Alisema Profesa Shivji.

Akitoa mfano wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Katiba, Profesa Shivji alisema haikufanya kazi yake kikamilifu hivyo kuwanyima wananchi fursa ya kutoa maoni.

Novemba 29 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitia saini muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 huku kukiwa na malumbano makali kutoka asasi za kiraia, vikiwemo vyama vya siasa, kupinga hatua hiyo kwa maelezo kwamba, mchakato huo uliendeshwa kwa mizengwe.

Hata hivyo, taarifa ya kusainiwa kwa muswada huo iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari, ilisema hatua hiyo ya Rais Kikwete, ilikamilisha safari ya kutungwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 baada ya Bunge kupitisha muswada huo uliowasilishwa na Serikali huku ikiweka wazi kuwa Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria
hiyo.

‘’ Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yeyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko hurukutoa maoni yake na Serikali itayasikiliza na kuchukua hatua zipasazo’’ ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

kutoka mwananchi
 
Hata sijakuelewa Muungano ndio ulifanya hivyo ama Utawala wenyewe..maana sielewi maamuzi ya rais yahusiane vipi na muungano? Hapa ndipo sikuelewa nataka kujua huo muungano ilihusika vipi ... ni ktk kutaka kuelewa mkuu wangu kesho niweze kuwa na kumbukumbu..
Unajua kikatiba, serikali ni ya muungano i.e URT

Kuupinga muungano ni sawa na ku- redefine territorial borders, almost an act of war.
Vyama vya siasa ni lazima viwepo bara na visiwani, just to verify their allegiance. Na ukiwa mwanachama maana yake umekubali muungano. Ndiyo maana KAMAHURU ilitakiwa iwe na wanachama bara ie CUF.

Sasa, mgombea binafsi atakuwa kiyume na matakwa ya katiba kuhusu vyama vya siasa, kuwa ni lazima viwe vya muungano.Na mtu mmoja hawezi kutambuliwa rasmi utiifu wake kwenye muungano eg. Mtikila.
 
Napata mashaka na maamuzi ya haki kutoka kwenye mahakama zetu maana nakumbuka kesi ya mgomo wa walimu mwaka 2007 ilivunja rekodi kwa maamuzi kubatilishwa usiku wa manane baada ya hukumu. Tangu kipindi kile nimekosa imani na mahakama zetu. Ukijumla na hatua ya majaji kushindwa kutoa hukumu ya haki ya mgombea binafsi huku wakijua kuwa mamlaka ya mwisho ya kutoa haki ni mahakama wao wakaurudisha mjadala bungeni kwa hoja dhaifu eti swala la mgombea binafsi nila utashi wa kisiasa na sio kisheria. Maamuzi ya hovyo kabisa.
 
Kwa style hii llengo lao linatimia، lengo la kuwa Katiba isibadilike mpaka next elections, watasingizia kesi hizo kuwa zilichelewesha mchakato
 
Hili la mgombea binafsi nadhani mpaka sasa imekula kwetu na ponea yetu iko kwny katiba mpya nadhani..
Kwa sababu mahakama ilishatuzingua kwa kukwepa jukumu lake (refer kesi ya mgombea binafsi)

Mahakama iliamuru suala lirudi bungeni wakati huko inategemea kama kuna political will.. Kitu ambacho hadi sasa sijaona political will yoyote si kwa rais wala serikali kwa ujumla kuruhusu mgombea binafsi..

Huu ni mfano sana nakumbuka vizuri mahakama kuu ilikwisha aamua kuwe na mgombea binafsi ila serikali wakakata rufaa mahakama ya rufaa chini ya jaji mkuu pamoja na wateule majaji wengine wakatudhulumu haki yetu tena kwa zengwe la wazi je leo ndo haki itatendeka kweli "I BET NOTHING WILL COME OUT OF IT"

Serikali ya tz inaweza kukubali kupoteza kesi ambayo haina maslahi nayo kwa kipindi husika na sio vinginevyo hiyo takrima unayotuambia matumizi yake yalikuwa yamekwisha pita ndo maana nasi tukajiona washindi swala la katiba hata kama ni kwa kuua chama chao hawajari ila watahakikisha wanaleta katiba inayoendana na matakwa yao na sio misingi na matakwa ya wananchi
 
Inategemea tuu jaji anafkiria nini na ni mtu wa aina gani..nafahamu kuna majaji with strong spirit na independent,bold hawawi sidelined na chochote bali their genuine intepretation of the law and facts

Tuombe Mungu huyu Judge awe huru kufanya maamuzi kwa manufaa ya nchi bila kuingiliwa na Magamba.
 
Unajua kikatiba, serikali ni ya muungano i.e URT

Kuupinga muungano ni sawa na ku- redefine territorial borders, almost an act of war.
Vyama vya siasa ni lazima viwepo bara na visiwani, just to verify their allegiance. Na ukiwa mwanachama maana yake umekubali muungano. Ndiyo maana KAMAHURU ilitakiwa iwe na wanachama bara ie CUF.

Sasa, mgombea binafsi atakuwa kiyume na matakwa ya katiba kuhusu vyama vya siasa, kuwa ni lazima viwe vya muungano.Na mtu mmoja hawezi kutambuliwa rasmi utiifu wake kwenye muungano eg. Mtikila.
Nimekuelewa kwa hiyo muundo wa Muungano ndio ulopelekea maamuzi hayo sio?...Dah ama kweli nchi yetu kizungurumkuti!
Unajua sheria zetu kusema kweli zinanishinda kabisa.. Mbona Zanzibar kuna vyama ambavyo haviko Bara?..Iweje bara tu ndio lazima tuwe na vyama pande mbili na hata tukishiriki Zanzibar hatuna ushirika ktk bunge lao unless mtu huyo ni Mzanzibar mbona sisi hatutazami asili ya mgombea?..

Sasa sababu hizi hizi zinaweza kabisa kutumika kuikwaza katiba Mpya maana huu Muungano wetu ni waki mazingara - Uchawi mtupu!
 
katiba mpya haitapatikana- kwanza sheria aliyosaini jk ni batili. Jk anapelekwa pelekwa tuu.

sheria iliyosainiwa ni tofauti na matakwa ya wananchi. Ccm ni waoga, ili ki ukweli ccm kwishney. Ije katiba mpya au isije, in any means and by all means ccm kwishney 2015 or even before 2015 gov may collapse because economy has already collapsed.

mimi nashauri kwa sasa tung'ang'anie tume ya uchaguzi ivunjwe na iundwe tume huru. Halafu 2015, tumpate rais atakae kuwa na moyo wa kuwatumikia watanzania.

jaribu kufuatilia post zangu za nyuma kuhusu tume ya uchaguzi
 
wakuu siamini kama kweli tutakuwa na katiba mpya kabla ya 2015'hiyo kesi ni ushindi mkubwa kwa ccm itaenda na itapitiliza 2015'sio idea nzuri hata kidogo kufungua kesi'tulitakiwa tulazimishe serikali kufanya tunayotaka'na kwa taarifa tu hayo ndo matokeo ya upole wetu na ujinga wetu
Kwani tunakimbilia wapi hii katiba sio ya tume ya uchaguzi.
 
Nimekuelewa kwa hiyo muundo wa Muungano ndio ulopelekea maamuzi hayo sio?...Dah ama kweli nchi yetu kizungurumkuti!
Unajua sheria zetu kusema kweli zinanishinda kabisa.. Mbona Zanzibar kuna vyama ambavyo haviko Bara?..Iweje bara tu ndio lazima tuwe na vyama pande mbili wakati na hata tukishiriki Zanzibar hatuna ushirika ktk bunge lao?..
Zanzibar ina serikali ambayo mipaka yake haihusiani na bara.
But the opposite is true when it comes to URT.
 
Huu ni mfano sana nakumbuka vizuri mahakama kuu ilikwisha aamua kuwe na mgombea binafsi ila serikali wakakata rufaa mahakama ya rufaa chini ya jaji mkuu pamoja na wateule majaji wengine wakatudhulumu haki yetu tena kwa zengwe la wazi je leo ndo haki itatendeka kweli "I BET NOTHING WILL COME OUT OF IT"

Serikali ya tz inaweza kukubali kupoteza kesi ambayo haina maslahi nayo kwa kipindi husika na sio vinginevyo hiyo takrima unayotuambia matumizi yake yalikuwa yamekwisha pita ndo maana nasi tukajiona washindi swala la katiba hata kama ni kwa kuua chama chao hawajari ila watahakikisha wanaleta katiba inayoendana na matakwa yao na sio misingi na matakwa ya wananchi

Mkuu ni kweli una kumbukumbu nzuri kuhusu kesi ya mgombea binafsi,ndio hasa kilichotokea.
 
Back
Top Bottom