Kesi dhidi ya katiba mpya mahakama kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi dhidi ya katiba mpya mahakama kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Dude, Dec 26, 2011.

 1. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Juzi nilipendekeza hapa kuwa sheria ya mchakato wa uundwaji wa katiba mpya inaweza kuwa challenged mahakama kuu kwa kukinzana na katiba.

  Leo mwananchi limeripoti na kumnukuu rais wa Tanganyika Law Society ndugu Stolla kuwa maandalizi yamekamilika kufungua kesi hiyo mahakama kuu.

  Sheria hiyo inakinzana na ibara ya 18 ya uhuru wa maoni kwa kucriminalize shughuli yoyote ya kuelimisha kuhusu katiba nje ya sheria hiyo.

  Sababu nyingine ni procedural irregularity kwa sababu kama mnavokumbuka ni kwamba muswada wa sheria hiyo ulikuwa withdrawn na ulivorudishwa ukapitishwa kana kwamba umesomwa mara ya tatu.
  Tusubiri lakini binafsi naona dalili ni njema ingawaje ground ya pili ndio ina nguvu kwa sasa nadhani kwa sababu zifuatazo.

  Hiyo ground ya kwanza mahakama inaweza kudeclare hicho kipengele void tothe extent of inconcistence na katiba na sheria yenyewe kama yenyewe ikaendelea.

  Lakini hiyo ground ya pili ikibainika na mahakama kweli procedure zilikiukwa basi sheria nzima inaweza kubatilishwa yani kuwa nullified na hivyo tukaanza mwanzo..which is what i pray for.
   
 2. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwanzo mzuri bt naingiwa na hofu kidogo kuhusu hiyo kesi, iv haki itapatikana kweli kwenye hizi mahakama zetu? labda ipelekwe ICC. Manake hiyo sheria inakiuka haki za binadamu.
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa majaji hawa wateuliwa wa magambo kweli haki itatendika bora waipeleke East Africa Court labda haki itapatikana
   
 4. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndugu ICC zinakwenda kesi za jinai za makosa ya uhalifu wa kimataifa yani international crimes..
  So kisheria tunasema ICC haina jurisdiction (mamlaka/uwezo kisheria) kupokea kesi kama hii..

  Kwa mujibu wa ibara ya 30(3) ya katiba na kwa mujibu wa basic rights and duties enforcement Act, mahakama kuu ndio sehemu muafaka ya kuanzia.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kesi ya katiba inasikilizwa na wateule wa jk haki itatendeka kweli?
  labda waje majaji wa kuazimwa kutoka nje!
   
 6. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Inategemea tuu jaji anafkiria nini na ni mtu wa aina gani..nafahamu kuna majaji with strong spirit na independent,bold hawawi sidelined na chochote bali their genuine intepretation of the law and facts
   
 7. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu ikishindikana, ndo kusema mahkama ya wananchi iingilie kati au?
   
 8. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu kuna kesi nyingi maamuzi ya mahakama yamekuwa dhidi ya serikali so tusiwe prejudiced mapema ivo,vuta subira na usikate tamaa!
   
 9. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ikishindikana hapo tunaenda court of appeal of Tanzania
   
 10. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa Tanzania yetu hii au, labda majaji watoke nchi nyingine!!
   
 11. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  From there?
   
 12. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  wakuu siamini kama kweli tutakuwa na katiba mpya kabla ya 2015'hiyo kesi ni ushindi mkubwa kwa ccm itaenda na itapitiliza 2015'sio idea nzuri hata kidogo kufungua kesi'tulitakiwa tulazimishe serikali kufanya tunayotaka'na kwa taarifa tu hayo ndo matokeo ya upole wetu na ujinga wetu
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwa majaji hahahawa! Lbd kwa miujiza ya MUNGU
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Mkuu kumbuka Jk alivyosaini ule mswada kwa mbwembwe. sasa we unadhani mahakimu wanaweza kutoa maamuzi sahihi na huru bila mkono wake? they must be remotely controlled!
   
 15. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mi naona ni disadvantage kwa JK na serikali yake kwamba watakuwa wameshindwa kuhakikisha katiba inapatikana kufikia muda huo,which means suala la katiba litakuwa limewashinda and it will imply someone else need to take over from thereon-whichever that is going to be CHADEMA,NCCR,CUF,UDP,SAUTI YA UMMA ETC I DON‘T KNOW!
   
 16. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Doesn‘t matter..unakumbuka kuhusu kesi ya takrima?
   
 17. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuliko kuwa na katiba mpya mbovu bora iwepo, Sasa ni kuhakikisha mgombea binafsi anakuwepo na 2015 kura zinalindwa usiku na mchana kwa nguvu zote ili kuhakikisha mshindi halali anapatikana
   
 18. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hili la mgombea binafsi nadhani mpaka sasa imekula kwetu na ponea yetu iko kwny katiba mpya nadhani..
  Kwa sababu mahakama ilishatuzingua kwa kukwepa jukumu lake (refer kesi ya mgombea binafsi)

  Mahakama iliamuru suala lirudi bungeni wakati huko inategemea kama kuna political will.. Kitu ambacho hadi sasa sijaona political will yoyote si kwa rais wala serikali kwa ujumla kuruhusu mgombea binafsi..
   
 19. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Tulijaribu sana kulinda kura mwaka jana lakni unajionea yaliyotokea'kumbuka tume ya uchaguzi ndio walewale'tungetumia nguvu ya maandamano na migomo'hakuna njia nyingine'kuchelewa kwetu kufikiri kutatupeleka kubaya
   
 20. h

  herimimi Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni uamzi wa busara,waharakishe kufungua,wengi tupo nyuma yao. umma utashinda.
   
Loading...