KESI AMBAYO HAIJAWAHI KUPATA UFUMBUZi

Zemanga zoze

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,012
1,698
imeandikwa na Abu bin seydun
Familia ya Beaumont ya watoto watatu ambao ni Jane Nartare Beaumont (alizaliwa 10 mwezi wa tisa1956), Arnna Kathleen Beaumont (Alizaliwa 11 mwezi wa kumi na moja1958), na Grant Ellis Beaumont (alizaliwa12 mwezi wa saba 1961)... Walikuwa wakiishi Adelaide South Australia walipotea mnamo tarehe 26 mwezi wa kwanza mwaka 1966 baada ya kuaga kwao kwamba wanaenda ufukweni kubarizi huku jane akichukua jukumu la kuwaangalia wadogo zake kwenye safari hio wakiwaaga wazazi wao Jim na Nancy Beaumont na kuelekea fukwe za Glenelg si mbali toka walipokuwa wakiishi mtaa wa Harding...Ufukwe ambao ulikuwa maarufu kwa watoto kutembelea na kufurahi ilihitaji safari ya dakika tano tuu kwa usafiri wa basi toka kwao mpaka ufukwe wa Glenelg na haikuwa shida kwakuwa washaenda Mara nyingi peke yao fukwe hizo na waliondoka asubuhi ya Siku hiyo .....Lakini wazazi wao walikuja kushtuka mpaka jioni watoto wao walikuwa hawajarudi na si kawaida yao wakienda ufukweni huwahi kurudi nyumbani hivyo wakatoa taarifa polisi jion hio polisi wakaanza uchunguzi kwa kuuliza watu waliokuwepo fukwe hizo........
WATOTO WAONEKANA NA KIJANA MREFU MWEUPE....... majibu yao yalikuwa hivi...kwamba waliwaona watoto hao watatu wakiwa na kijana mmoja mweupe aliyejengeka kimazoezi huku umri wa kijana ukikadiriwa kuwa miaka kati ya thelathini hivi ...huku akionekana kucheza nao na kufurahi pamoja na kijana huyo ufukweni shahidi mwingine alikuwa ni muuza duka wa fukwe hizo alipohojiwa alisema Mara ya mwisho alimuona Jane Beaumont akija dukani kwake na kununua pasties na meat pie akiwa na( A£ 1) paundi moja ya Australia....huku wazazi wakishangaa maana waliwapa hela za usafiri tuu wasingeweza kununua vitu hivyo huku muuzaji akikiri kuwajua watoto hao kutokana na kutembelea mara kwa mara fukwe hizo lakin hawakuwahi kununua vitu vya bei ghali hivyo. Polisi wakathibitisha kuna mtu aliwapa hela hio......
MUDA WA MWISHO KUONEKANA WATOTO HAO...
Alipohojiwa mtu wa kupeleka barua mtaa wa Harding yani "Postman" alikiri kuwaona watoto hao wameshikana mikono wakiwa na furaha wakirudi nyumbani kwao...baadae polisi walikiri kwamba post man alikosea muda aliowaona watoto hao ...huku wazazi wakiwaelezea watoto wao hasa Jane mkubwa wao alikuwa na aibu na muoga kwahiyo Huyo kijana inaonekana alijenga mazoea nao kupitia safari zao za nyuma ufukwen apo ikafika kipindi wakamzoea na kumuamini kutokana na taarifa ambayo Arna mdogo ake Jane alimpa mama yake Siku moja kabla ya kupotea kwao kwamba Jane amepata rafiki wa kiume ufukweni lakini mama yake hakuzingatia hilo akijua ni rafiki tuu...miezi kadhaa mbele baada ya kupotea kwa watoto hao mwanamke mmoja aliibuka na kusema aliona mwanaume akiwa na watoto watatu wakiingia kwenye nyumba ya karibu kwake iliyokuwa haitumiki halafu baadae akamuona huyo mwanaume peke yake akitoka haya hivyo polisi hawakumpeleleza sana kwanini hakutoa taarifa kwa wakati taarifa ziliendelea kumiminika zaidi ya mwaka na habari hii kuteka vyombo vingi vya habari nchini Australia pia ikawa funzo kwa wazazi kutowaachia watoto wao waende picnic bila uangalizi....
KESI YAWAVUTIA WATAALAMU WA NGUVU ZA GIZA..... Kwa kiingereza huitwa parapsychologist ambao uchunguzi wao hukusaidia kitu zaidi ya kupamba vyombo vya habari(media frenzy) kwa kuonyesha majengo kadhaa ambayo wanahisi watoto wa Beaumont wamezikwa lakini hata yalipobomolewa hakuna chochote kilichopatikana kama ushaidi,..............................
FAMILIA YA BEAUMONT YAANZA KUPOKEA BARUA.
Baada ya miaka miwili ya kulotea kwa watoto wao Walipokea barua kutoka kwa mtu aliyejifanya ndo amewateka na anataka awarudishe mikononi mwa wazazi wao lakini mwishoni ilikuja kufahamika kwamba si kweli na huyo mtu alikuwa akifanya hivyo kujifurahisha na aligundulika mwaka 1992 baada ya kuingia kwa teknologia mpya kama (haox fingerprinting) akiwa na miaka 42 na barua hizo alituma akiwa na teenager .... WAZAZI WALIONGEAJE KUHUSU WATOTO WAO.......
Jim na Nance Beaumont Waliendelea kuishi nyumbani kwao wakiamini ipo siku watoto wao watarudi nyumbani kwao mwaka jana (2016) wakiwa wanaadhimisha miaka hamsini(50)/toka kupotea kwa watoto wao walisikika wakisema haitapendeza kama watoto wao wakirudi wao wakiwa wameshakufa mbaya zaidi miaka ya karibuni wametengana kila mmoja anaishi kivyake huku wakikubali kwamba ukweli kuhusu kupotes watoto wao haujapatikana na wameamua kuzika majina ya watoto wao na kuishi maisha yao yaliyobaki mbali na vyombo vya habari mwaka jana Jim alikuwa na miaka 90 na nancy alikuwa na miaka 88.Japo kuna wauwaji wengi wameshakamatwa na kufungwa kuhisiana na upotevu wa watoto hawa lakini hakuna aliyekiri imebaki siri na imekuwa amoung "TOP TEN UNSOLVED CASES EVER"
 
Ulizaa,ukaita majina,ukalea kwa muda kisha kwa ghafla tu watoto wanapotea na huwaoni tena maishani.Unazeeka huku ukijenga taswira sasa hivi wangekuwa hivi na una imani kwamba kuna siku watatokea kwa kuwa hawakufa ukashuhudia maiti zao.
Inauma sana
 
aiseeehh!sad story bora wafe ujue wamekufa makaburi yao yapo kuliko kupotea unajipa moyo kua kesho atarudi
 
Aisee miaka mingi hiyo kuna mambo humu duniani ukiyasoma inakuwa kama unaangalia movies hayaaminiki
 
Back
Top Bottom