Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,928
- 828,569
PICHA HII ILIPIGWA JANUARY MWAKA 2010.
,, Wa kwanza kulia (waliokaa) ni Prof.Idris Mtulia, aliyekua Mbunge wa Rufiji. Anayemfuatia ni Prof.Mark Mwandosya
wakati huo akiwa Waziri wa maji na umwagiliaji. Anayemfuatia ni aliyekua mkuu wa wilaya hiyo Bw. Kassim Majaliwa.
Prof.Mwandosya akiwa Waziri alitembelea Rufiji katika ziara ya kikazi. Majaliwa akiwa mkuu wa wilaya akampokea, na Prof.Mtulia kama Mbunge mwenyeji akashiriki ziara hiyo. Hapa wanavuka kwa Mtumbwi mto Rufiji eneo la Mtanza.
Oktoba mwaka huo Majaliwa aligombea Ubunge Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi na kushinda. Katika Baraza la Mawaziri mwaka 2010 Akateuliwa Kuwa Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu). Miaka mitano baadae akawa Waziri Mkuu.
FUNZO:
Hakuna ajuaye hatma ya maisha yetu ila Mungu pekee. Usimdharau yeyote kwani hakuna ajuaye kesho. Ukiwa na cheo au madaraka makubwa kazini usiwadharau walio chini yako, huenda kesho wakawa maboss zako.
Potifa alikua mkuu wa gereza kule Misri , akamuona Yusufu kama kijakazi aliyejaribu kumbaka mke wake, akamtupa gerezani. Lakini baadae Yusufu akawa Waziri Mkuu na Potifa akawa anatii na kutekeleza maagizo ya Yusufu.
Wakati Majaliwa akiwa DC Rufiji, alikua anaripoti kwa RC Pwani Magesa Mulongo na Waziri wa TAMISEMI Stephen Wassira . Leo wote wawili hawapo tena serikalini.
Majaliwa alipoteuliwa Naibu Waziri TAMISEMI alikua anaripoti kwa Kepteni George Mkuchika. Leo mzee Mkuchika ndiye anayeripoti kwa Majaliwa.
Maisha ni mzunguko. Ukifanikiwa usijae kiburi ukadhani ndio mwisho wa safari. Al-Bashir alikua na madaraka makubwa na pesa nyingi. Lakini leo ni mfungwa. Anakula, kulala na kuamka kwa amri. Hana tena hiyari ya maisha yake.
Na pia ukikosa leo usikate tamaa ukadhani Mungu amekuacha. Bado lipo tumaini. Anayekudharau kwa sababu ni 'Housegirl' kesho unaweza kuolewa na Rais ukawa first lady na akakuheshimu.
Kesho yako ni fumbo
Wana wa Israel walipowekwa mateka kule Babeli, Esta na mjomba wake Mordekai walikua watumwa. Esta akachukuliwa na Hegai kuwa kijakazi kwenye nyumba ya Mfalme.
Hegai alikua kama ' Afisa Utumishi' kwenye kasri la mfalme Ahasuero . Vijakazi wote wa mfalme waliripoti kwake akiwemo Esta. Lakini baadae Esta akawa Malkia , na Hegai akawa anaripoti kwake. Life is circle.
Hakuna aliyejua kiongozi mwenye ulinzi mkubwa na fedha nyingi kama Gadafi siku moja angeweza kujificha kwenye mtaro wa maji taka kama mwizi wa kuku.
Usijivune kwa kufanikiwa leo, na usivunjike moyo kwa kufeli leo. Winston Churchill aliwahi kusema " Success is not final, and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
Mungu pekee ndiye ajuaye hatma yetu atuwezeshe kuishi kwa akili... niwatakie baraka za Bwana
Imenakiliwa..!