Kesho Rais kikwete kuhutubia taifa...

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Kesho kikwete atahutubia taifa katika sherehe za kuhitimisha mbio za mwenge zitakazo fanyika uwanja wa uhuru jijini dar es salaam.
katika sherehe hizo mwenge utakabidhiwa kwa rais halafu naye ataukabidhi kwa kikosi maalum kitakachoenda kuupandisha kwenye mlima kilimanjaro.
watoto wa halaiki zaidi ya 600 ambao watapamba sherehe hizo. mia
 
umeitoa wapi hii habari tafadhali, we bado ni kuku wa kienyeji humu jamvini.
 
Mimi nakumbuka alipokuwa anahutubia wazee wa CCM wa Dar es Salaam katikati ya mwezi, alisema amelazimika kutoa hotuba ile wakati ule kwa kuwa mwishoni mwa mwezi hatakuwa na nafasi, kwani atakuwa yupo Bujumbura! Au alijua akiwadanganya wazee hakuna atakayejali?
 
alshabab hawashambulii tena mikusanyiko? au ccm wao hawashambuliiwi na alshabab
 
Ni jambo zuri kuwa hata baada ya kusaini mswada kuwa sheria ya kuunda team ya kukusanya maoni, amekubali pia kusikiliza maoni na kuuboresha (through which system usiulize yeye ni Rais atawezesha) kukidhi matarajio ya wananchi.

Ukweli huu sasa lazima uanze na maoni yote yaliyomezani kwake bila kusubiri kuwasilishwa tena upya (urasimu) na matokeo yasikike lililokubaliwa na lililokataliwa na sababu zake. Yaani tuokoe muda na tuache asonge mbele, na Jk atakumbukwa kwa hili. Kwahiyo, katika hotuba yake kesho ayatolee majibu hayo ambayo yako mezani kwake ili kuthibitisha dhamira ya walichokubaliana na CDM.

Pia aeleze utaratibu utakaotumika hadi kufanya maboresho. Hii itawapa imani wananchi wengine na vyama kama NCCR waliokata tamaa kushiriki kutoa maoni ya kuboresha muswada ambao sasa ni sheria.
 
Chadema walikataa kutoa maoni yao bungeni (walilidharau bunge) wameamua kukimbilia kwa rais(ambaye walisema hawamtambui), rais alisema atasaini mswada lakini ameamua ku u-edit kwa matakwa ya chadema (amedharau bunge). Nini hatima yake?, nadhani hautasainiwa mwaka huu mpaka mawazo mapaya ya chadema yakajadiliwe na kuridhiwa na bunge la sivyo JK atakuwa ameingia choo cha MP wa kike.....................
Ni jambo zuri kuwa hata baada ya kusaini mswada kuwa sheria ya kuunda team ya kukusanya maoni, amekubali pia kusikiliza maoni na kuuboresha (through which system usiulize yeye ni Rais atawezesha) kukidhi matarajio ya wananchi.

Ukweli huu sasa lazima uanze na maoni yote yaliyomezani kwake bila kusubiri kuwasilishwa tena upya (urasimu) na matokeo yasikike lililokubaliwa na lililokataliwa na sababu zake. Yaani tuokoe muda na tuache asonge mbele, na Jk atakumbukwa kwa hili. Kwahiyo, katika hotuba yake kesho ayatolee majibu hayo ambayo yako mezani kwake ili kuthibitisha dhamira ya walichokubaliana na CDM.

Pia aeleze utaratibu utakaotumika hadi kufanya maboresho. Hii itawapa imani wananchi wengine na vyama kama NCCR waliokata tamaa kushiriki kutoa maoni ya kuboresha muswada ambao sasa ni sheria.
 
Tumeshachoshwa na hotuba zake zilizojaa usanii na huku akikataa kukutana na waandishi wa habari wamuulize maswali live hata kwa masaa mawili au zaidi.
 
Huu uzuzu tuliokuwanao watz unatokana na huo mwenge. Sijaona tija ya mwenge tangu kuasisiwa kwake zaidi ya hasara kwa taifa kupoteza nguvu kazi ya vijana wa leo dhidi gonjwa hatari la "UKIMWI" .

mwenge ni ulozi maalum ulioasisiwa na hayati jk nyenyere kwa ajili ya kutu- log off watz ili tutawalike. Ni mtazamo wangu tu!
 
Back
Top Bottom