Kesho Naenda MAHAKAMANI, Naomba Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesho Naenda MAHAKAMANI, Naomba Msaada

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Uswe, Jul 2, 2012.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mdogo wangu alikua ameajiriwa na jamaa anaitwa richard kwenye kibanda cha tigo pesa

  amepata short katika hiyo biashara, kulingana na maelezo yake, hiyo short aliipata kutokana na network mbovu ya mtandao wa tigo

  anasema, alituma pesa kwa mtu, mtandao ukamjibu kuwa hiyo transaction haijafanikiwa, akarudia rudia badae akafanikiwa, lakini kumbe pale alipokua anajaribu afu inashindikana pesa ilikua inakwenda, sasa huyu mwenye kibanda, (aliyemuajiri dogo) amekwenda polisi na sasa kesho atapelekwa mahakani, tena kwa criminal charge


  Dogo amelala Polisi Jumamosi, Jumapili tumeweza kumuwekea dhamana lakini ilikua shughuli pevu, Kuna dalili zote za rushwa! Mazingira yanaonesha kuna mtu kapewa pesa ili amfundishe adabu dogo.

  Toka asubuhi tuko polisi, waliokuwepo wanasema hiyo issue anaishughulikia afande Nuru (ni mwanamke) afande nuru kapigiwa simu asubuhi saa mbili kasema yuko njiani anakuja, hadi saa nne hajafika, saa nne akapigiwa akasema nyie endeleeni na shughuli njooni saa saba, ilipofika saa saba akapigiwa simu akasema yupo njiani anakuja, hadi saa tisa alikua hajafika!


  Alipofika kitu cha kwanza anasema tumsubiri Richard (huyo bwana aliyeshtaki), baada ya kueleweshana na kujiridhisha kwamba dhamana kwa mtu anayetuhumiwa sio lazima anayetuhumu awepo (sio requirement ya kisheria) Afande Nuru akasema anataka huyo Richard aje ili kuepusha majungu!

  Tuliendelea kumsubiri huyo Richard hadi karibu saa kumi na moja jioni! Afande anasita kutoa dhamana kwa sababu anaogopa majungu.

  Kitu kingine cha ajabu, dogo alipokamatwa jumamosi, hakuchukuliwa hata maelezo ya awali, Kwa maelezo niliyoyapata polisi ni kwamba Richard alimpigia simu afande kwamba kuna mtu kamdhulu, afande bila ushahidi wowote wa awali, bila hata kuchukua maelezo kutoka upande wa pili akafanya maamuzi ya kumkata dogo na kumtupa rumande, Jana (baada ya kuwa dogo kuwa amelala rumande tayari) Afande Nuru ndio kachukua kamwandikisha maelezo (hiyo ilikua saa tisa mchana)

  Msaada kutoka kwenu
  1. Nilifikiri hii ni kesi ya madai lakini kama nilivosema nafikiri kuna influence ya askari mmoja, na wanafungua criminal case, Je hii ni sahihi? kama sio tufanyaje?

  2. Nitegemee nini kesho? ni wakati gani nahitaji kumhusisha mwanasheria? Je kuna mtu anaweza kusimamia hii case, kama ndio naomba aniPM

  3. Huyu mtu alikuwa anasema hasara aliyopata ni laki nne lakini alipofika polisi akabadilisha ikawa laki saba, ni wazi anadanganya, lakini pia ni wazi anatumia rushwa, Nini nifanye kuzuia influence ya pesa anayotumia?

   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Wana mkataba wa kazi? kwanza dogo ana haki ya kukataa tuhuma dhidi yake ili apewe nafasi ya kueleza ukweli ambapo mtapewa muda wa kutoa maelezo ya kweli.lakini vizuri kumtafuta wakili amtetee kwakuwa mkishinda yeye atalipa gharama za kesi na usumbufu.poleni sana!
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  1. Hapana hawana mkataba wa kazi

  2. nimeuliza naambiwa wamefanya crimanal case makusudi, eti criminal case unakua unashitakia na jamhuri kwa hiyo huyo jamaa anakua kama hausiki hivi, sasa mi sijui ina maananisha nini kisheria.

  3.Ninashukuru
   
 4. H

  Henry Philip Senior Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  fANYA FASTA UTAFUTE MWANASHERIA KWANI NIMEONA HUYO JAMAA NA AFANDE WANA MAPUNGUFU,KWANZA HAIKUCHUKULIWA MAELEZO YA AWALI, PILI ANASEMA DOGO ALIMDHURU-ALETE USHAHIDI ALIMDHURU VIPI. NAKUSHAURI TAFUTA MWANASHERIA ATAKUSHAURI NA KUKUSAIDIA VIZURI ZAIDI. DUH UNYANYASAJI KILA KONA. POLE SANA MKUU.
   
 5. U

  Uswe JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Nashukuru, kama kuna mwanasheria humu anaweza kusimamia hii kesi naomba aniPM
   
 6. nameless girl

  nameless girl JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 3,905
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  hiyo case ni ya madai na si criminal kama wasemavyo, endapo wata rise issuea ambazo unadhani si za kweli una haki zote za kuchallenge mahakama na kuthibitika mahakamami kwamba jambo wanalosema ni la kweli. kwa ufupi huyo dogo alilolifanya ni mistake na hakudhamiria. fasta saka mwanasheria kabla hawajakupotezea muda hao
   
 7. congobe

  congobe JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  pole ndugu yangu kwa matatizo,naomba nikusaidie jambo muhimu kuliko yote unapofanya money transactions kwa njia ya mitandao lazima kumbukumbu zinabaki,mwambia dogo awe mkweli kama ni kweli alihamisha fedha kama anavyodai,ili dogo atakapoanza kuhoji maswali mahakamani ana haki ya kuomba mahakama itoe kibali cha uchunguzi juu ya namna fedha zilivyohamishwa kwa mteja,hata yeye mwenyewe anaweza kupiga simu costerma care wakampatia list ya namna pesa zilihamishwa kwa mteja ,na costerma care wana uwezo wa kutoa ushahidi mahakamani,hakuna case .je dogo alimjulisha tajiri yake juu ya hilo ..ama aliwajulisha tigo pesa juu ya uhamisho huo je? tatizo lilishughulikiwaje.ukipata majibu hayo tafuta wakili ama simama mwenyewe hakuna case hapo,ila isiwe dogo kafanya janja alafu anadanganya wenda tajiri yake amefatilia tigo pesa kakuta hakuna uhamisho ulofanyika kimakosa ndo mana kamweka ndani.haitakiwi useme uongo kwa wakili ujue hilo wakili anatumia maelezo yako kushinda case
   
 8. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  Pesa zikihama kunabaki uthibitisho wa transaction ilofanyika na huwa inarudi kama feedback kwenye simu ilotumika dogo must be mkweli
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Wanaweza kwenda Tigo wakaomba statement toka kwenye hiyo line ya biashara(Tigo Pesa) baada hapo watajua kama kuna double transactions kwa no moja moja,watafanya utaratibu kwanza kuomba warudishiwe toka kwa huyo alietumiwa mara 2 ama la watajua nini cha kufanya,wanamuonea tu huyo dogo kumlaza ndani na kumpa kesi kubwa kama kaiba benki akiwa mtumishi wa benki hata mkataba hana ni uonevu mkubwa,jitahidi kupata wanasheria wakushauri anapoteza muda wake huyo bwana Richard!nasikia hasira sana ukimfanyia mtu kazi yake ila ikitokea makosa anakuruka na kukupa kesi!!poleni sana wana JF mliopatwa na mkasa
   
 10. U

  Uswe JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Alikwenda Tigo kupata msaada lakini alikwama kwa sababu yeye sio mwenye account, Tigo walimwambia hawawezi kumpa details za mteja mwingine.

  Bosi wake kakataa pia kutoa ushirikiano, sijui kama kaenda tigo mwenyewe, lakini mimi nilimuomba tupate statement ya tigo kisha tupitie hiyo statement wote, akagoma!
   
 11. congobe

  congobe JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  omba mahakama itoe order ya kuletwa ushahidi kwamba pesa zilihama ama la kutoka tigo ili weka wakili utfanikiwa
   
 12. MFYU

  MFYU JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ,nadhani ni CRIMINAL CASE! Cuz uyo mwenye TIGO,anamtuhumu kwamba dögo ameiba...THEFT!! Sasa Onus itakua kwa dogo,kuprove kwamba hakuna wizi
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Hapana, onus kwanza ipo kwanza kwa anayeshitaki (jamuhuri) kuleta ushahidi wa mambo angalau mawili: kwanza kama kuna kosa(wizi) umefanyika na pili kama mtuhumiwa ndiye aliyetenda kosa(wizi) huo - kwa yote mawili bila kuacha shaka yoyote. Baada ya hapo ndio mtuhumiwa naye ataleta ushahidi wake either kuonesha kuwa hakuna wizi uliofanyika au kama kweli wizi umefanyika, si yeye aliyefanya wizi huo au angalau kuonesha kuwa ushahidi ulioletwa na jamuhuri dhidi yake unaacha mashaka.

  Ni vema mtuhumiwa akapata usaidizi wa kitaalamu (wakili).
   
 14. k

  kiliochangu JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 1,122
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  mwanasheria kwa kesi ya vocha.au auze ng'ombe akanunue kuku. Anyway. Amka, wakushtakiwa hapo ni Tigo kwa kuwa na huduma ambazo haziko sawa. Muhusika wa kibanda nenda Tigo kawape taarifa wakulipe pesa zako kwa kosa la uzembe wao. Sheria ipo ya kulipwa> Nenda kaulize wanasheria tume ya mawasiliano watakujulisha
   
Loading...