DISPLEI
Member
- Oct 17, 2012
- 70
- 46
Hivi karibuni Trafic Police wanakaa sambamba na kituo cha Ubungo Kibo kuzuia magari yasipite njia ya mwendo kasi (kuelekea Ubungo). Sambamba na kituo hicho, kuna kituo cha daladala pia na bajaji zinapakia na kushusha.
kutokana na pilikapilika mahali hapo, waendesha magari kuna wakati wanalazimika kupishana kwa kusogea upande wa mwendo kasi ili kuzuia msongamano wa magari au kujihepusha kukwanguana na bajaji/daladala. Kitendo cha kukanyaga msitari wa upande wa mwendo kasi, gari inakamatwa na kuambiwa kwamba umefanya kosa la kupita njia ya mwendo kasi.
Wanakutia hofu kwamba kutokana na kosa hilo, utawekwa ndani badaye kupelekwa mahakamani na ili kukomboa gari utatakiwa kulipa TZS600,000. Wengi wanajitetea mwishowe unaambiwa ulipie makosa 3 hadi 5 (90,000 hadi 150,000) ili wakuachie. Hela hizo zinalipwa mfukoni mwao.
Vyombo husika viliangalie hili tatizo na kuondolea raia wema kero
- za kubambikiza makosa kwa nia ya kujinufaisha.
- za kuwachelewesha kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi
hawa maaskari wapo hata leo trh 07 Jul, 2020 na wanaendelea na usumbufu huo kwa raia wema. Tafadhari vyombo husika liangalieni hili kuondoa usumbufu husio wa lazima kwa waendesha magari.