Kero za Kubaki Bachela – Maisha ya Kuazima Furaha kwa Wengine!

Friji la mtumba

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
277
Reaction score
431
Wakuu Nimerudi tena na hawa kataa ndoa, nimekaa nikaangalia maisha ya mabachela (na mimi nimewahi kuwa mmoja wao), nikagundua kuwa kubaki hujaoa kwa muda mrefu ni kama kujitesa. Maisha ni ya muda, ya kubahatisha, ya kuomba msaada kwenye kila jambo.

Kero kuu za maisha ya bachela:

1. Hakuna mtu wa karibu wa kweli: Unaugua, unahitaji mtu wa kukuangalia – unaishia kupiga simu “umepotea sana mrembo.”

2. Chakula ni kama adhabu: Unakula chipsi, wali wa mama Ntilie au unaagiza kila siku. UPUUZI

3. Uchafu wa maisha: Vyumba vya wengi vina harufu ya soksi, sahani haijaoshwa wiki mbili, sinki limejaa maji.

4. Mastress ya mapenzi: Leo unaambiwa “niko busy,” kesho “nipo kwa shangazi,” halafu unakuta anapost picha na mtu mwingine.

5. Gharama zisizo na tija: Kila weekend unaingia ‘mtego’ – outing, vocha, drinks, surprises. Mwisho wa mwezi huna savings wala maendeleo.

6. Upweke wa kweli: hii inapelekea wengi kua waraibu wa punyeto na kupelekea kukosa nguvu za kiume..

Wanaume wenzangu tuliooa, hebu tusifiane kidogo:
Haya yote sisi tumeepuka. Tuna wake halali, tunafanya tendo kwa uhuru na amani, tunajua kesho tunakula nini, na maisha yanapangwa kwa pamoja. Ni heshima, ni amani, ni maisha ya kujengeka.

KATAA NDOA WENGI HAWAPO SAWA VICHWANI
 
Kupika & Usafi hizo ni tabia kama hukufundishwa kwenu walaumu wazee wako, watu tunakaa mageto masafi muda wote na ukitaka kupika nusu saa umemaliza.
Stress za mapenzi hizo nazo ni mambo ya kujitakia ukiwa mwanaume karne hii.
Kuhusu savings mimi ambaye sijaoa nasave kukuliko.

Nenda urudi na hoja nyingine
 
Umemiss ubachela wewe.
 
Una uhakika gani kusema ww ambae hujaoa unasave kunizidi nilieoa??? Unafaham kipato changu
 
Back
Top Bottom