DOKEZO Kero ya umeme Mbeya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sisi wakazi wa Isyesye iliyoko mkoa wa Mbeya tunashida moja na TANESCO, hatukatai kuna mgawo wa umeme lakini kuna kero moja inayotukwaza sana wananchi: Umeme umewekwa kwa zamu lakini cha kushangaza hata siku ambazo tunatakiwa kushinda na umeme wao wanakata.

Pia wakati mwingine wanarudisha umeme halafu unakuta unakaa dakika mbili tu na wanakata tena hapo haujashinda siku nzima na sisi wengine hatutegemei mishahara, kipato chetu kula yetu na watoto kusoma tunategemea huo huo umeme. Wangetufikiria kwa hili suala jamani ni kero kubwa.

Na pia kama wanakata, basi tujue wanakata moja kwa moja sio wanakata wanarudisha sekunde mbili wanakata tena ni kikwazo tunaunguza vitu jamani.
 
Ata Mimi Niko Ilomba uku tunashare line wote ya Chunya mpaka muda huu hakuna umeme.
Yani CCM mnachotufanyia kwenye umeme Mungu ndo anajua
 
Back
Top Bottom