Kero ya uharibifu wa noti za kitanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Ndugu Wana Jamii forums.

Siku za hivi karibuni kuna tabia inayoelekea kuzoeleka ya mateja(ita wavuta bange) kuchana tepe za noti na kuzitumia kwa ajili ya kuvutia bange au madawa mengine ya lulevya. Inasikitisha kuona kwamba wizara ya fedha, ambayo ndio wenye hakimiliki ya hizo noti wameendelea kukaa kimya kana kwamba hawajui kinachoendelea. Sidhani kwamba kuna ofisa yeyote wa wizara ya fedha ambaye hajawahi kutumia au kuona noti iliyoondolewa utepe(mkanda?)-samahani siujui jina sahihi linalotumiwa hapa-watalaamu wanaweza kutusaidia. Hizi noti zimeharibiwa sana kiasi kwamba ni nadra kukuta noti kuanzaia sh 1000 na kuendelea ambayo haijabanduliwa huo utepe wa pembeni.<img height="812" width="392">
Ili kutokomeza tatizo hili, natoa wito kwa serikali itoe agizo kwa mabenki yote kukusanya noti zote zilizobanduliwa utepe kwa muda maalumu itakaoona unafaa, na baada ya huo muda kupita noti zote zisizokuwa na utepe zichukuliwe kama noti bandia na zisikubaliwe katika malipo yoyote yale. Baada ya kufanya hivyo kutakuwa tena hakuna tatizo la noti kuharibiwa na mateja kwa kuwa wataogopa kupata hasara pindi wabanduapo utepe huo kwa kuwa hakuna mtu atayekubali kupokea hizo noti.

Kusema kweli hili tatizo mimi linanikera sana ndio maana noti zetu haziheshimiwi. Kila mwendawazimu anaweza kuzichezea kadri atakavyotaka, ikiwa ni pamoja na wale watengenezao noti bandia. Wadau wengine mnasemaje kuhusu hili tatizo?


wahusika watalishughulikia ipasavyo hilo suala asanteni. Pesa ya Tanzania.jpg Pesa ya Tanzania.jpg
 
Hili ni tatizo la beni kuu kutengenezesha noti zisizokidhi viwango!!
 
Hili ni tatizo la beni kuu kutengenezesha noti zisizokidhi viwango!!
Hawa jamaa si ndio wanaozidisha hadi order ya mzigo wenywe; akili zao zimejaa kujinufaisha tu aka kufisadi
 
Back
Top Bottom