Kero ya mitandao ya simu kugawa Number kwa mtu mwingine

Kero ya mitandao ya simu kugawa Number kwa mtu mwingine

coyyote

Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
53
Reaction score
88
Umofia kwenu wakuu.

Awali ya yote ningependa kuwapa pole kwa hili janga la Corona na tuzingatie utaratibu uliotolewa na wataalamu wa afya juu ya namna gani ya kujikinga.

Twende katika hoja yangu. Kumekuwa na utaratibu wa mitandao ya simu nchini pindi Number ikawa offline kwa kipindi fulani kama miezi mitatu kwa sababu mbalimbali either kupotea kwa hio sim card ama kusafiri nje ya nchi, wao husajili mtumiaji mpya kwa hio number na matokeo yake watu hukutafuta kwa number hio na kutokea kutoelewana anapopokea mtu mwingine wasiyemjua.

Binafsi nilisafiri nje ya nchi mwezi Novemba mwaka jana, nimerudi mwezi March katikati na bahati mbaya nilipoteza simcard yangu ya Airtel, nilipata lost report na kwenda ofisi za airtel Morocco, pasipo tarajia nikaambiwa Number yangu tayari imesajiliwa na mtu mwengine kwani haikuwa hewani kipindi kirefu, cha kufanya ni kusajili number nyingine, nilitoa malalamiko yangu kuhusu number yangu kwani ndio number ya kiofisi lakini wakasema hawana cha kunisaidia kuhusu hilo swala, na kwa moyo mgumu nikakubali matokeo.

Sasa nikasajili number nyingine mpya kwa mtandao huohuo, kero iliyojitokeza ni kwamba napata simu kila siku watu wakimtafuta mtu aitwaye Ndesi, mwingine shemeji (inaelekea ndie aliyekuwa mmiliki wa hii number mpya na pengine amepata mkasa kama wangu). Kila nikijaribu kuwaeleza wapigaji kwamba mnaemtafuta sio mmiliki tena wa hii number hawaelewi, kesho yake wanapiga tena, yani mpaka imefika hatua ya kuichukia simu yangu kwani simu ninayopata nyingi ni za watu nisiowafahamu zaidi ya ndugu na marafiki.

Sasa najiuliza, ni kwanini number hupewa mtu mwingine ndani ya kipindi kifupi sana, kwani Number zimeisha? Na kama zimeisha si mfanye grace period ya walau miezi sita number ikiwa offline ndio irudi sokoni, mbona miezi mitatu ni kidogo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
airtel ndio wana izo mambo sana.. unasajili namba mpya leo ,simu zinaanza kuingia za wamasai ata hujuan nao wakimtafuta morani mwenzao.
Ni kero sana, juzi nimepokea simu nikaanza kupigwa mabusu na mwanamme mwanzangu nilishtuka sana, nikamuuliza mzee baba vipi? akajitambulisha yeye ni Joseph wa Iringa na hii namba ni ya mchepuko wake wa Dar. Jamani tutapeana kesi imagine unanunua line kumbe ilikuwa namba ya jambazi, mara wazee wanakutrace wanakukuta si unajua huwa hawaulizi wakifika ni mateke tu mwisho wa siku unavunjwa kiuno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanzo tabia hii walikuwa nayo mtandao wa tgo siku hizi Airtel wanaboa sana . Miezi mitatu mbali kuna simcard yangu ilijilock baada ya wiki mbili nafanya process ya kurenew ishakuwa na mtu.

DUMU KUBWA
 
Umenichekesha wew dah
"Wewe baba si nilikwisha kuambia kuwa mimi nimeolewa ni mke wa mtu huku migombani, mbona huelewi unazidi kunipigia simu?" Hapo nilikuwa nampigia shemeji yangu wa kiume kumbe namba walishagawa. Ilibidi niombe samahani maana hali ilikuwa inakuw a tete.
 
"Wewe baba si nilikwisha kuambia kuwa mimi nimeolewa ni mke wa mtu huku migombani, mbona huelewi unazidi kunipigia simu?" Hapo nilikuwa nampigia shemeji yangu wa kiume kumbe namba walishagawa. Ilibidi niombe samahani maana hali ilikuwa inakuw a tete.
😂😂😂😂😂nimezid kucheka
 
Hawa airtel waligawa number yangu moja maridadi kabisa sitowasamehe

Sent from ONEPLUS 5T using Tapatalk
 
Kumbe,,,mi nilisajili halotel sijampa mtu namba naitumia kwa intanent,nashangaa napigiwa simu na namba siijui,,
Nikadhani labda wasiojulikana wana maongezi na Mimi,maana kila nikisearch jina la mpigaji sipati mrejesho,hajasoma shule yaani hakuna rekodi yeyote,
Mpaka Sasa nimeblock namba za simu karibu 100.
 
airtel ndio wana izo mambo sana.. unasajili namba mpya leo ,simu zinaanza kuingia za wamasai ata hujuan nao wakimtafuta morani mwenzao.
ha ha ha mkuu umenichekesha sana

kwakwli airtel wanaudhi yaan namba yangu pia ya zaidi ya miaka 10 wamempa mtu mwingne kisa miezi 4 tu sikuwanimetumia
dah sasa sikuwa na namna nikasajiri nyingne
kwakweli nilipata usumbufu sana kwa hao morani
halafu hawajui kutuma sms wao wanapiga tu ukikata wanapiga tu hata uwaelekeze vp hao morahawakuelewi kabisa yaani

mm AIRTEL situmii tena nimeachana nao usumbufu mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kama mtu uliacha mpunga wa kutosha kwenye Airtel money wanapita nazo kama upepo?
Mimi kero hiyo pia imenikumba voda nimesaji laini pia na m.pesa nimetumia wiki mbili tu nashangaa watu wakitaka kunitumia pesa linatoka jina jingine


Sent using IPhone X
 
Ukitaka namba yako wasimpe mtu mwingine weka MADENI TU
TIMIZA we kopa
Kama ni M PESA kopa m pawa na songesha na
Kama ni TIGO PESA we kopa NIVUSHE Tena lipa kule mwanzoni ikifika kama laki 2 hv hata ukae mwak a mzima still line yako HATAPEWA MTU MWINGINE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
airtel ndio wana izo mambo sana.. unasajili namba mpya leo ,simu zinaanza kuingia za wamasai ata hujuan nao wakimtafuta morani mwenzao.
Kweli kabisa Mkuu Airtel ndio wako hivyo
.
Mimi Nina watu wengi Sana kutok Mtwara wananipigia wanaongea kilugha, Ukiwaambia hawasikii watakuj kukupigia tena
kuna mdada wa mtwara nae nilikua nachati, Nikawa namtongoza [emoji23][emoji23]
 
Ukitaka namba yako wasimpe mtu mwingine weka MADENI TU
TIMIZA we kopa
Kama ni M PESA kopa m pawa na songesha na
Kama ni TIGO PESA we kopa NIVUSHE Tena lipa kule mwanzoni ikifika kama laki 2 hv hata ukae mwak a mzima still line yako HATAPEWA MTU MWINGINE

Sent using Jamii Forums mobile app
Njia sahihi ni kufanya porting,,namba itakuwa yako milele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom