KERO Kero ya Maji Uyole, Nimeilipa, huduma hakuna!

KERO Kero ya Maji Uyole, Nimeilipa, huduma hakuna!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2026-05-21 at 16.55.25.jpeg

Fichua uovu: Uyole, jimbo jipya la Tulia.

Nimefanya malipo ya kuunganishiwa huduma ya maji safi tangu mwezi wa nne, lakini hadi leo sijapatiwa huduma hiyo. Kila ninapofuatilia, naambiwa vifaa bado havijapatikana, niwasubiri hadi vitakapokuja.

Kinachoniumiza ni kwamba ninatumia gharama kubwa kununua maji kila siku, ilhali mtaani ninaona mabomba yakivuja ovyo bila kurekebishwa wala kuchukuliwa hatua. Inazua maswali: je, kweli vifaa havipo, au kuna mchezo unaendelea?

Naomba suala hili lipatiwe ufumbuzi na sauti ya wananchi isikilizwe, kwani hali hii imekuwa ni mzigo mkubwa kwa maisha yetu ya kila siku.
 
Shida kubwa idara nyingi za Serekali uwajibishwaji ni mdogo na hakuna kabisa kwahiyo ni ngumu sana wahusika kufatwa majukumu yao kwa uhakika na kwa weledi. Zaidi hapo utaambiwa vifaa havijakuja toka mkoani na ukifwatilia utaambiwa vifaa havijaja kutoka ofisi ya kanda yetu mgao wetu ni mpaka mwezi wa 6.
 
Back
Top Bottom