KERO Kero ya barabara kwa wakazi wa Kata ya Kimala wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wakazi wa kata ya Kimala Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa tumekuwa na kero ya Barabara ya kuingia kwenye kata yetu.

kata hii ina vijiji 4 ambavyo havina Barabara za uhakika za kupita mwaka mzima. Kwenye kipindi hiko cha mvua, Barabara huwa mbaya na mbovu na kama tukipata mgonjwa yatupasa tumbebe kwenye machela ili tumpeleke sehemu zenye huduma ya Afya kwenye kata ya Dababa ambayo ni umbali wa Kilomita 30 kutoka katani kwetu.

Changamoto hii ni kubwa kwani kwa sasa kutoka katani kwetu hadi kwenye kata ya Dabaga ambayo ina Barabara za uhakika za kutufikisha Iringa Mjini au kutufikisha Wilayani Kilolo tunatakiwa kulipa gharama ya Tsh 50,000 kwa boda boda kwani hakuna gari linaloweza kuja huku katani kwetu.

TARURA Wilaya ya Kilolo tusaidieni kutatua changamoto hii kwani wagonjwa wanalia ndani.

angalia kwenye hii video mateso tunayopata.

Your browser is not able to display this video.



Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…