Kero ya askari mbezi - ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero ya askari mbezi - ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 19, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa ni saa 2 usiku , mabasi ya mikoani na nchi jirani ndio yanaingia kwa wiki sana , nipo eneo la mbezi , hapa mbezi wahamiaji wengi huwa wanapenda kushukia huko kwa sababu ya fujo kwenye standi kuu ya mabasi ubungo , kuna wahamiaji haramu na wale ambao ni halali

  Mara basi likisimama basi taxi nyingi sana huwa zinapaki pembeni kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri kwa watu mbali mbali , kati ya hizi taxi , zipo ambazo askari polisi wa kituo kikuu cha mbezi wanazijua kazi zao ni kutafuta wahamiaji mpaka wanapokaa ili waweze kuwasiliana na askari wa kituoni kwa chochote .

  Gari ndio hilo limesimama wasomali wanashuka kwenye basi Kampala Coach , Taxi inasimama kwa mbele , wale wasomali wanapanda ile taxi ya mbele , Dereva wa taxi anaendesha hiyo taxi kufika mbele kidogo tu mara gari ya polisi imeziba njia wasomali analazimishwa kushuka kwenye gari waingie kwenye gari ya polisi .

  Wanapanda gari ya polisi , sasa gari ya polisi haiendi kutuoni kama inavyotakakiwa wanaenda msitu mmoja maeneo ya mbezi au msitu mwingine ambao uko karibu na chuo kikuu cha dar es salaam eneo la golani .

  Wakifika huko wanalazimishwa kutoa pesa , yule dereva wa taxi pamoja na askari polisi wanasaidiana kuwasachi wale wasomali kila sehemu ya mwili , askari wengine pembeni wako na silaha zao , msomali akiwa mbishi basi kupigwa kwa vitako vya silaha zile au makofi .

  Baada ya hapo kama wameshachukuwa pesa zote ndio wanawaacha huru kuwasiliana na ndugu zao ambao wako nchini ili waje kuwachukuwa lakini hapo hapo wana kesi mkoni ya kuingia nchini kwa njia haramu kwahiyo wanaogopa kudai haki zao kama wakijaribu basi wanaweza kubanwa na hizo kesi zao .

  Pamoja na kuna askari wengine huwa wanashiriki vitendo hivi haswa wale askari ambao wameachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu na matatizo mengine , wengi walioachishwa kazi utawakuta kona , Rombo , Stop over pamoja na Ubungo Mataa .

  Hii ni hali halisi eneo la mbezi mpaka ubungo , huu ni usumbufu wanaupata sana wanaposhuka kwenye mabasi na vyombo vingine vya usalama toka nchi jirani , sasa imekuwa kama kazi kwa sababu hata madereva wa taxi nao wanashirikiana na askari kuendesha vitendo hivi

  Wahusika wa masuala ya usalama wa maeneo hayo naamini watashugulikia kero hii kwa sababu nimeshaandika , naomba wafuatilie zaidi .

  Sasa Naenda Kupumzika Kesho nitawaletea kisa kingine cha serikali ya Ubungo Mataa
   
 2. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Leo Shy umetupa kisa live . Big up!
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  shy upo active sana
  ni shame kwa vyombo vyetu vya usalama kunyanyasa wageni hata kama ni wahamiaji haramu. kuna taratibu zake za kuwashughulikia na si kama wafanyavyo
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Balaa kubwa hilo.
   
Loading...