Kero: Wasukuma kuongea kilugha kila mahali

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
10,419
15,974
Wakuu,

Natumai asubuhi ipo murua kwenu,

Jamani kuna hii kero ya hawa ndugu zetu kutoka Shinyanga bila kusahau Mwanza na maeneo mengine ya kupenda kuongea kilugha.

Yaani wanadhani hii nchi ina kabila moja tu wao sehemu yoyote ni kuongea kisukuma kwenda mbele.

Imagine mtu umemtoa msichana mzuri out mmekaa mnapata msosi mara anapokea simu anaanza kupayuka kilugha.

Mnaudhi sana nyie jamaa.
 
Nachowapenda wasukuma wanajali sana lugha yao ya asili, nimeishi shy mno yaani wao kijijini au mjini wanatwanga tu kisukuma sio kama sisi kwetu (ujiji) ukisikika unaongea kilugha wanaanza kukucheka kua umetoka shamba, au mrundi. Mwisho wa siku watoto wanakua hawajui lugha yao ya asili na utamaduni ndo unapotea taratibu.

NB. Msukuma pure hasikilizi bongo fleva utamkuta kafunga redio kiunoni ameachia saautii kuuuubwa huku yupo ananyonga baskeli. Wanasikiliza sana wasananii wao kama Madebe,Ng'Wana shindu, etc

-R Davincio..
 
Kwani makabila mengine yamekatazwa kuongea,waache wasukuma wafurahie lugha yao,kama unaona aibu kuongea lugha ya kabila lako hadharani wengine wanaweza waache,na wanajivunia kuiongea na ndio lugha inayowaunganisha kama jamii ya wasukuma.
 
Hamna kabila linaboa kama wajaluo,imagine wamepanda basi watatu lkn utadhani basi zima ni wajaluo,kwa mfano mmoja awe amekaa mbele mwingine katikat na 3 akae mwisho basi wao huwa wanaendelea na story kama vile wapo wenyewe na ukizingatia Mungu amewajalia sauti ndio kero kbs
 
Kwani makabila mengine yamekatazwa kuongea,waache wasukuma wafurahie lugha yao,kama unaona aibu kuongea lugha ya kabila lako hadharani wengine wanaweza waache,na wanajivunia kuiongea na ndio lugha inayowaunganisha kama jamii ya wasukuma.
Watu kama hawa ndo wanakua watumwa wa lugha zisizo zao...utakuta anaona fahari kuongea kizungu ila anaona aibu kuongea lugha ya kwao huko!
 
Nachowapenda wasukuma wanajali sana lugha yao ya asili, nimeishi shy mno yaani wao kijijini au mjini wanatwanga tu kisukuma sio kama sisi kwetu (ujiji) ukisikika unaongea kilugha wanaanza kukucheka kua umetoka shamba, au mrundi. Mwisho wa siku watoto wanakua hawajui lugha yao ya asili na utamaduni ndo unapotea taratibu.

NB. Msukuma pure hasikilizi bongo fleva utamkuta kafunga redio kiunoni ameachia saautii kuuuubwa huku yupo ananyonga baskeli. Wanasikiliza sana wasananii wao kama Madebe,Ng'Wana shindu, etc

-R Davincio..
Hahaa me sio msukuma ila nmezaliwa na nimeishi usukumani, nawakubali sana wasukuma kweny kuheshimu lugha yao
 
Utajibeba kajinga wewe! Wasukuma tukikohoa vikabila vingine mnyamaze kabisaaa! Nafikri mnaona jembe linavyowaburuza, mtakoma!
Sasa kwani hili Jembe ni Msukuma? Ushamba wenu kila anayeongea Kisukuma kwenu ni Msukuma.
 
Wakuu,

Natumai asubuhi ipo murua kwenu,

Jamani kuna hii kero ya hawa ndugu zetu kutoka Shinyanga bila kusahau Mwanza na maeneo mengine ya kupenda kuongea kilugha.

Yaani wanadhani hii nchi ina kabila moja tu wao sehemu yoyote ni kuongea kisukuma kwenda mbele.

Imagine mtu umemtoa msichana mzuri out mmekaa mnapata msosi mara anapokea simu anaanza kupayuka kilugha.

Mnaudhi sana nyie jamaa.
Hiyo inaitwa proud to be msukuma....hongereni sana wasukuma kwa hilo...mmewaonesha wengi kuwa mkosa kabila ni mtumwa..sio wanao jifanya kuongea kizungu wakidhania ni usomi kumbe ni lugha ya watu kama ilivyo lugha yao..penda chako sio kupenda cha mwenzio...na kukumbusha tu sio shinyanga na mwanza tuu kuna mikoa mingine mingi tuu inayo ongea hiyo lugha na ni lugha inayo ongewa na watu wengi saaana tz...ndugu kuliko kuwa na kero au wivu kajifunze hiyo lugha ili upate kujua mengi kuhusu wasukuma na uwingi wao na ukarimu wao. Kuna asiliam kubwa sana ya watu kutoka mataifa mengine wanao ongea kisukuma kama warabu, wasomali, wahindi, wazungu kwanini wewe kama mtz usitafute kujifunza kuongea lugha ambayo ni ya pili kuongelewa hapo tz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom