KERO: Umeme wa kununua kwa zamu na nyumba za kupanga ni janga

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
11,015
16,447
Wakuu, nimepita sehemu hii jioni kuna ugomvi mkubwa kisa ni zamu za umeme, kiukweli hizi luku ni nzuri kama wapangaji wako wachache na wanaelewana vinginevyo ni majanga.

Hivi haiwezekani kila mpangaji akawa na mita yake kama vile switch?

Mabachela inakula kwao zaidi wanaotoka asubuhi kurudi usiku hasa wale wasio na vifaa vingi vya umeme lakini kwenye malipo wanalipa sawa, ukute anawasha taa tu ghetto akirudi.

Vipi una ushuhuda wowote kwenye hili?
 
Me niliwahi walaza giza wapangaji wenzangu Mbagala.

LUKU ilikua moja hafu vyumba vipo vinne, kwahiyo kila ukiisha ananunua mmoja wa Elfu 10. Wengi tulikua tunaishi simple mi sikua na friji wala jiko ni pasi, kuchaji simu na TV kidogo tu nikirudi jioni.

Aisee, siku hiyo asubuhi naenda mishemishe ndio nikaambiwa umeme umebaki kidogo sana na ni zamu yako, nikasema poa nikirudi nitarekebisha sahivi nina haraka (kumbe sikua na hela Nina kama Buku ya kufika mihangaikoni tu).

Aisee siku ya kufa nyani huwezi amini sikupata ata mia, wakati wa kurudi mfanyakazi mwenzangu akanipa lift hadi Rangi 3 mi nikamiza na ngoko hadi Kongowe. Mida ya saa 4 usiku nakuta nyumba giza.

Watu walilala giza nadhani walinitukana sana usiku kucha. Kesho asubuhi saa 11 nishaondoka ata sikuoga maana bafu la nje wangeniona.

Mida ya Asubuhi nikaotea buku 5 nikamrushia mtoto wa jirani aniwekee kwenye LUKU hafu jioni nikaja nikatia wa buku 10 mwingine. Ila nikapita kila nyumba nikaomba radhi kwa jana niliwaambia tu ukweli.
 
Wakuu, nimepita sehemu hii jioni kuna ugomvi mkubwa kisa ni zamu za umeme, kiukweli hizi luku ni nzuri Kama wapangaji wako wachache na wanaelewana vinginevyo ni majanga..hivi haiwezekani kila mpangaji akawa na mita yake Kama vile switch?

Mabachela inakula kwao zaidi wanaotoka asubuhi kurudi usiku hasa wale wasio na vifaa vingi vya umeme lakini kwenye malipo wanalipa sawa..ukute anawasha taa tu geto akirudi..
Vipi una ushuhuda wowote kwenye hili?
Tatizo siyo wapangaji ama nini. Nyie hamumjui adui wa walalahoi Tz kuwa ni Tanesco yenyewe!

Ukitaka kumuwekea 'mita' kila mpangaji (separation meter), utakadiriwa gharama ya kuvuta umeme upya ya Tsh 320,000/= kwa kila mita, bila kuelewa kwamba mita ndiyo chanzo chao cha mapato cha shirika, hata wangelitoa kwa gharama ya chini ama bure gharama zao za uunganishaji zingerudi tu!

Sasa kama una wapangaji let say wanne, mwenye nyumba muziki huo utauweza?

Ki ukweli ilitakiwa kila mpangaji angelikuwa na mita yake, wala huo ujima wa kishenzi usingelikuwepo, maana kamwe binadamu hamuwezi kulingana matumizi ya kitu chochote, kuna watu hapo lazima wanyonywe.

Hiyo ni kero ya miaka nenda rudi katika jamii ya watu wa kipato cha chini, lakini shirika la umeme ama viongozi walishashindwa kuliona hilo kama ni kero kubwa sana ya msingi kwa jamii, wapo tu kupiga siasa na kufikiria upigaji.
 
Back
Top Bottom