Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 312
- 286
Habari mdau wa kilimo!
Je, umewahi kuskia semi maarufu ya "ukiitiwa fursa basi wewe ndio fursa" ama " dili limekua dirisha"? Semi hizi na zinginezo zimekua maarufu kutokana na tapeli mbalimbali walizo/wanazofanyiwa wakulima na wafugaji. Hapa chini tutakupa mifano hai kwa uzoefu toka mkoani Shinyanga.
Bidhaa feki tofauti na makubaliano ya wateja
Jina la Kampuni: Mkarama Ent. Co LTD
Hawa mabwana, walikuja huku Shinyanga na kujinasibu kuwa wanatoa elimu bure ya ujasiliamali, kilimo na ufugaji.
Katika wilaya mojawapo humu Shinyanga walitoa elimu na kuahidi kuleta vifaranga kwa bei ya offer ya Tshs. 1000( vifaranga wa Bovan( kuku wa Mayai).
Wananchi wakateleza na offer.....mwisho wa siku "dili likawa dirisha" kama msemo wetu maarufu. Vifaranga walioletwa ni Vijogoo wa kuku wa mayai ambavyo kwa Dar huuzwa 200-300@ 20000 boksi la vifaranga 102!
Mauzo ya machapisho yenye elimu potoshi.
Hiki ni kilio kingine kwa upande wa wajasiliamali( wakulima na wafugaji wakijumuishwa).
Machapisho mengi ya hawa waandaa semina yana taarifa potoshi mathalani utoaji wa chanjo, uandaaji wa lishe na matunzo kwa ujumla ya mifugo. Vitabu vingi maandishi yake na "Google" hayana uhalisia! Serikali tunaomba mliangalie hili kwa ukaribu. Kwa elimu hizi, wakulima na wafugaji hupata hasara kubwa ya ama kutopata bidhaa bora ama kudumaza mifugo na hata vifo. Vitabu huuzwa kwa bei rafiki tu 3000/5000 ila elimu aipatayo mkulima/mfugaji ni bomu la maisha.
Uuzwaji wa rangi za barafu kama mbolea za maji/booster!
Mdau unashangaa! Hili si jambo geni katika tasnia nzima ya kilimo cha bustani huku vijijini. Wafanyabiashara wasiowaaminifu wametuweza sisi wakulima wadogo tusio na elimu ya kilimo. Bidhaa hizi huuzwa haswa haswa katika minada nakadharika.
Uuzwaji wa dawa na viuwatilifu "mfu"(vilivyokwisha muda wake)
Wafanya biashara wasio waaminifu kwa kujua kua watanzania hawana taratibu ya kusoma vipeperushi wala vifungashio vya dawa. Wamekua na taratibu ya kuuza bidhaa zilizoisha muda wake. Na kwa ubaya zaidi bidhaa zingine zimeandikwa kwa lugha ya malkia hivyo ni ngumu kwa mkulima mswahili mwenzangu kusoma na kuelewa. Serikali toeni macho katika hili.
Wakulima na wafugaji tufumbue macho. Tutafute taarifa katika vyanzo sahihi na kujiridhisha kabla ya kuingia kichwa kichwa. Tusiwe fursa.