Kero Nyumba za kupanga

Kero Nyumba za kupanga

Mwanakulipata

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2018
Posts
718
Reaction score
1,203
Huu ni uzi Maalumu wa kuweka kero ambazo umekutana nazo kwenye nyumba za kupanga,

Mimi bhna kuna nyumba hiyo nilikaa mama mwenye nyumba ni mtu wa Tanga sijui ni wema ama ujamaa umezidi, baada ya kuhamia kama wiki moja kupita nashangaa nalazimishwa kula kwa mwenye nyumba, siku nyingine usiku nimetoka chuo nipo geto nagongewa mlango naambiwa kuna hotpot ya chakula apa...ikabidi nimuulize vizuri yule mama akasema wao wamezoea hivo kwamba mpangaji nikama familia yao nikasema huu mtego

Basi bhna ujamaa ukaendelea weee ikafika stage nikinunua kiroba cha unga ama mchele anatumwa mtoto na jagi “mama kasema anaomba unga/mchele” nikasema haya ndo malipo[emoji23][emoji23]

Kidogo kidogo hizi buku mbili naombwa sanaa..tena kumnyima mmama ishu ko unajikuta unatoa tu afu hazirudi[emoji26]..

Mwanangu umepika nini?.. Naomba hiyo mboga kidogo nile hapa...

Mama ikafika stage nikipita na maziwa au chochote kile anataka tugawane..

Sasa kubwa kuliko nilitoka kununua taulo zuri nikalifua...jioni nalianua binti yake ambae ameolewa anakaa hapo hapo akanipokonya nikajua masihara litarudi nashangaa baadae usiku namwambia nigee taulo nataka niingie ndani...“taulo lako baba nanilii amejifutia bahati mbaya apa labda nikununulie jingine" nikajua tayari nishapigwa[emoji23][emoji23][emoji23]

Loh! Yule mama alikuwa kichefu chefu..nilijuta kukaa pale wapangaji waliopo wakaniambia akikuzoea huyo atakuomba kila kitu
 
Nyumba za kupanga kama nyumba za kupanga.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom