Kero: Manispaa Morogoro punguzeni matawi ya mianzi hapo darajani

Kero: Manispaa Morogoro punguzeni matawi ya mianzi hapo darajani

Alubati

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2016
Posts
6,757
Reaction score
15,493
Katikati ya mji mita mia moja kutoka halmashauri ya manispaa ya Morogoro uelekeo wa kituo kikuu cha polisi ,kwenye daraja maarufu " daraja la shani".
Kuna miti ya mianzi ambayo imekuwa na faida ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi mara mto unapofurika.
Lakini sasa matawi yake yamekuwa na kufanya eneo hilo la daraja kuwa giza upande wa kushoto,matawi pia yanasogea katikati kwenye barabara eneo la watembea kwa miguu na kuwa kero.
Inawalazimisha watembea kwa miguu kupita kwenye njia ya magari ili kuepuka kuchomwa na matawi ambayo sasa yanaelekea kuziba barabara.
Mfanye usafi hapo msisubiri mh. Rais akose pa kupita atakapokuja kufanya kampeni uwanja wa Jamuhuri.
 
Back
Top Bottom