Kero huduma kwa wateja Azam TV

Kero huduma kwa wateja Azam TV

ngonani

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2012
Posts
1,366
Reaction score
598
Kwa siku tatu mfululizo nimekuwa nikipiga Azam Customer care ili kuulizia mambo kadhaa kuhusu vifurushi vyao vipya kwa namba 0764700222. Cha kushangaza kila nipigapo naambiwa subiri utahudumiwa muda sio mrefu! Siku ya kwanza nilishika simu sikioni kwa takribani dakika 45, napigiwa wimbo mfupi na mwisho naambiwa maneno hayo hayo, hadi simu ikaloa jasho.

Kesho yake hivyo hivyo na siku zilizofuata hivyo hivyo. Hadi nikakata tamaa na kuacha kabisa kufuatilia. Swali; Je, huduma ya Customer Care Azam bado ipo au illishasitishwa? Na kama haipo kwanini wateja tusijulishwe? Na kama bado ipo kwanini inachukua zaidi ya saa moja bila kuwepo response?

Najua message itawafikia na mtatoa ufafanuzi..
 
Nimelipia king'amuzi cha Azam Tv, napiga huduma kwa wateja simu zote hazipatikani, nataka wanifungulie kifurushi cha 30,000, nilipolipia walifungua kifurushi cha kilichokuwa awali,
 
Mkuu leo Jumamosi .
Wao sio Kampuni za simu kwamba wapo kazini siku zote.
Piga Jumatatu na wapo vizuri saana tu kwenye kuhudumia wateja wao.
Nakuambia hivyo kwa uzoefu.
 
Mimi pia nimelipia cha 30000,lakini bado hawajafungua inabidi wabadilike sio mbaka tuwapigie simu bwana waweke system kwamba mteja ukishalipia tu inafunguka tokana na ulivyolipa sio mimi nianze kuangika tena kupiga simu.
 
Namba ya Azam ni 0784 108 000. Mwezi huu wa Ramadan wanafunzi ofisi zao saa 12 na kufunguliwa-Ardhi saa 3 asubuhi
 
Mimi pia nimelipia cha 30000,lakini bado hawajafungua inabidi wabadilike sio mbaka tuwapigie simu bwana waweke system kwamba mteja ukishalipia tu inafunguka tokana na ulivyolipa sio mimi nianze kuangika tena kupiga simu.

Mkuu ebu fafanua kwanza mie awali (mwezi uliopita)nililipia cha 15 sasa wamepandisha ni 20,nimelipa cha 12 na nimeunganishwa moja kwa moja bila kupiga call center,je mwezi ujao nikilipa cha 20 itakuwaje? je itanilazimu kupiga call center waniunganishe na Azam Plus?
 
King'amuzi changu cha Azam kimekata matangazo baada ya kifurushi kwisha. Majira ya saa 18:30hrs kwa kifurushi cha Azam Play Tsh.30,000. Hadi muda huu zaidi ya saa 20:20hrs hakijafungua. Akaunti yangu ni 212904379094. Nimepiga huduma kwa wateja simu zote hazipokelewi hali inayoonyesha kuwa kitengo hicho hakifanyi kazi muda wote kuhudumia wateja. Nimepata hasira nafikiria hata kukivunja king'amuzi chenyewe nirudi Startime.
 
Back
Top Bottom