Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,582
Habari za majukumu waungwana,
Mimi ni mkazi wa Igoma jijini Mwanza maeneo ya St. Mary, pale kuna kituo cha daladala kisicho rasmi maarufu kama Bango la zain.
Sehemu hiyo imekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo kwani magari yaendayo / yatokayo Musoma hupita pale kwa spidi kubwa kitu kinachopelekea wavuka kwa miguu, waendesha baiskeli na pikipiki kugongwa mara kwa mara.
Wiki jana aligongwa kijana na kufa pale pale. Tukazika, jana mida ya saa nne usiku amegongwa tena kijana mwingine na kufa pale pale.Kwa yeyote mwenye ushauri tufanye nini naomba msaada wa mawazo.
Sehemu hiyo hakuna tuta, hakuna zebra na kuna kama kigenge hivi kinachofanya watu kuvuka mara kwa mara. Uongozi haujafanya lolote kuwajulisha TANROADS ili kupata suluhu ya ajali hizi.
Nawasilisha.