Kenyans work illegally in our country

the influx of kenyans who illegally work in our country is a big problem whereby kenyans dominate most of private school.

let them come and work ,at the end of the day your children will benefit by speaking english
 
Ngamia alimwomba mwarabu aliyekuwa kwenye hema ili ahifadhi kichwa chake tu kujikinga na baridi na upepo wa usiku jangwani. Yule mwarabu kwa wema wake akamkubalia. Ilipofika asubuhi ngamia alikuwa ndani ya hema na mwarabu alikuwa nje akipigwa na baridi.
 

Kama ulinisoma vizuri ndugu yangu Sherpherd niliongelea "WORK ETHICS" wakati najenga hoja yangu ya awali kuhusu umuhimu wa kuwakaribisha wageni waje kufanya kazi nchini. Inawezekana kabisa kama ulivyosema kozi ya unesi ya Tanzania ikawa na mtaala mzuri tu. Ila utendaji wa kazi unahitaji stadi za kazi zaidi ya hizi academic qualifications tunazozishadidia sana hapa Tanzania. Kuna mambo kama kuheshimu kazi, kujituma kazini, kujiamini, uwezo wa kuwasiliana (communication skills) na watu mbalimbali, huduma kwa wateja na muhimu zaidi ubunifu katika utendaji wa kila siku. Bahati mbaya haya mambo hayafundishwi mashuleni bali ni elimu dunia ambayo mtu anaipata kutoka kwenye jamii iliyomzunguka toka kwa wazazi, walimu, na watu wengine. Hivyo badala ya kupoteza muda kuwalaumu wageni wanaokuja nchini kufanya shughuli mbalimbali tungejifunza ni nini hasa walichonacho, ambacho sisi ama hatuna au hatukitumii ipasavyo, kinachowafanya waweze kuajiriwa nchini mbali na makwao na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi.

Umewahi kujiuliza kwa nini mahoteli mengi ya kitalii yanapenda kuwaajiri wakenya hata kwa nafasi za chini ambazo hazihitaji utaalamu mkubwa na wako tayari kuwalipa mshahara zaidi ya watanzania? Ulishawahi kufika hotelini na kugundua kuwa badala ya mpokeaji kukupokea mzigo, ambayo ni kazi yake aliyoajiriwa kuifanya, anajidai kama hajakuona? Wewe hujawahi kumuajiri fundi uashi au seremala mkakubaliana kazi na malipo na unapomsimamia ili amalize kazi kwa wakati na kiwango mlichokubaliana akakuona msumbufu na wakati mwingine kuikimbia kazi? Kuna tatizo la msingi ambalo tunatakiwa kama watanzania tujiulize ni wapi ambapo hatuendi sawasawa ili ikiwezekana tuanze kuwekeza kwa watoto wetu waje kutukomboa kwenye hili tope la "mediocrity". Ukisoma vitabu vinavyoelezea maendeleo ya nchi za Asia kama China, Malaysia, Singapore, Thailand, na nyinginezo utagundua kuwa walijifunza mambo mengi sana toka kwa wazungu na wajapani kwa lengo la kubadilika ili waige yale mambo yaliyowafanya waendelee kwa kasi. Na pia hawakusita kuwaajiri kwa wingi pale utaalamu wao ulipohitajika.

Suala la watu kuulizwa vitambulisho barabarani siwezi kuliongelea kwa undani kwani sijui masuala ya Kenya kwa undani ila kwa uzoefu wangu mchache wa kutembelea huko sijawahi kuulizwa kitambulisho barabarani. Ninachojua ni kuwa ukiwa unafanya mambo yanayotia shaka yumkini utaulizwa kitambulisho hata hapa kwetu Tanzania.
 

Ni kweli nakubaliana na wewe kwamba Watanzania tupo na excuse nyingi sana na poor katika utendaji wa kazi.Lakini nafikiri vyuo wingeboresha mitaala yao hili imwandae mwanafunzi kuwa na nidhamu katika kazi nakufanya kazi kwa bidii zote,hili wageni kufanya kazi za wazawa lipungue.Lakini kwa upande mwingine watu sio waminifu ukija kwenye suala la maadili ya kazi,watu wengi upenda kudokoa sana na maanisha mkono mrefu wanaweza kufilisi kampuni yako ndio maana makampuni mengi yanapokuja kuwekeza Tanzania wanaoutsourse watu kutoka nje,ethics katika kazi bado ni suala gumu kwa watanzania wengi.Nafikiri watu wajitume na kuwa nanidhamu katika kazi hii itajenga trust kwa waajiri shida watanzania wanapenda utajiri wa haraka haraka.Tuje kwa maada halisi watu wasio na kibali wasirusiwe kuendelea kuwepo Tanzania au kufanya kazi.
 
Their presence is not a problem,but their illegal presence matters, try to go in Kenya and work illegally u will see

Even their presence ni tatizo... In short HATUWATAKI, kwa nini wanalazimisha sisi waTZ tuwatake/kuwakubali...
 
let them come and work ,at the end of the day your children will benefit by speaking english

Akili zako naweza kuzifananisha na JK, anayebadilishana madini kwa suti...
 

Kwa hiyo tuendelee kuchukua walimu kutoka kenya na hawa wanaozalishwa na vyuo vya Tanzania tuwaache kwa sababu awajui kingereza.Uzalendo kwanza ndugu mengine baadaye.
 

Uko sahihi Mkuu !!
 
wacha kutuchanganya wewe!!!! is there any opportunity for Tanzanians to do the same in Kenya????!!!! hata ikitokea imeenda Kenya kusoma especially universities once ukimaliza immigration officers will deal with u perpendicularly hadi unavuka mpaka kuingia tz kama ni barabara au hadi unapanda ndege!!!!!!
 
Unajuanga Tatizo si kwa wa KE kuwa wengi kwa hii nchi, na wala sisi wa KE sio kwamba tunajuanga mavitu mingi. Issue ni kwa ogezeko la wajinga kwa Tz, maana sielewi ni kwa nini mTZ anangangania lichama zee kama ccm(implies ujinga bado upo nchini) halafu anashangaa eti kwa nini wakenya wanajaa hapa ni kufanya kazi professional ati, kwa sababu hamna watu wa kutosha kufanya hizi kazi
 
mbona unaandika vitu ivi ivi..
 
Nikiendelea kuchangia hi mada tym t napigwa ban, maana kuna watu wajinga cjawah kuona, wanasema watanzania ni waviv cjui blah blah.. let me tel them if u pay cheap u get the monkeys..! kama kaz inahtaj digree alaf unajir chet kuna utanzania hapo? by tha way wat is the use of English in tailoring? engeneering? nursing? hawa watz wanaowadharau watz wenzao ni full of sh\@t!! hata ivo knachogomba hapa sio wakenya kufanya kaz, ni kufanya kaz bila vibal... alaf huu upuuz umekuwa ukichagiza na viongoz wetu.. mauchwara makubwa.. hata Pinda amewah sema hvo, et mara amefiwa oh cjui nini, mbona kesi zinahairishwa jaj akiuguliwa na mtoto? au wao sio watz? mara ngap wabunge na mawazir hawapo oficn au majimbon kwao? hata uwazir tuwaajir wakenya na wahind basi... This is our Tanzania and we wl damn die for it no matter wat!! wakituona waviv wakajenge hizo shule Kenya.. wa.j.in.ga wakubwa!!
 
Ila wajiandae kurudi huko kenya, kwani 2015 sio mbali, ni swala la muda tu...
 
How about our native teachers who in streets scrambling at least to get a post while private schools are under kenyans
Wanakidhi viwango?? Kama mnawapeleka failures kwenye fani ya ualimu mnategemea nini?? Waacheni bana watusaidie cha msingi wafuate taratibu tu :bored:
 

Umenena Mkuu!! Binafsi siongezi kitu Mkuu !!
 
Watanzania lazima mfahamu kuwa mkenya au mganda kufanya kazi Tanzania SIO KOSA KISHERIA!
Muungano wa nchi za afrika mashariki zinamruhusu mwananchi wa nchi yyt katika hizi, kuishi na kufanya kazi popote pale ktk afrika mashariki.
 
Watanzania lazima mfahamu kuwa mkenya au mganda kufanya kazi Tanzania SIO KOSA KISHERIA!
Muungano wa nchi za afrika mashariki zinamruhusu mwananchi wa nchi yyt katika hizi, kuishi na kufanya kazi popote pale ktk afrika mashariki.

Tujadili kufanya kazi bila vibali. Walio wengi wanafanya kazi bila vibali na kama kuna mmoja bi boss anataka awabebe ndugu zake wote .

W tz inabidi tuwe wazalendo kwa kuwafichua watu kama hawa.
 
Tujadili kufanya kazi bila vibali. Walio wengi wanafanya kazi bila vibali na kama kuna mmoja bi boss anataka awabebe ndugu zake wote .

W tz inabidi tuwe wazalendo kwa kuwafichua watu kama hawa.


Labda hayo masuala ya vibali lkn
Suala la boss kuwabeba ndugu zake.

mbona karibu watz wengi wanalo hilo!

We angalia kwenye ofisi yyt mfano boss akiwa muhaya! Au mchaga! au muha!

Unakuta mpaka mfagiaji kabila lake!

Kama tunapenda haki, basi tuanze kusafisha kwetu kwanza kabla ya kuwaregebisha hao wageni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…