Kenyan Professionals More Competent than Tanzanians?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenyan Professionals More Competent than Tanzanians??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RAJ PATEL JR, Sep 30, 2010.

 1. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I came across this interesting article posted somewhere by a blogger.
  You be the judge!!


  Mkuu wa kaya pole na mihangaiko ya kampeni naona imepamba moto kweli kweli ! Uzuri ni kwamba libeneke bado linaendelea kama kawa hivyo lazima nikupongeze sana kwa hilo !

  Sasa pamoja na kwamba nchi nzima iko kwenye harakati za uchaguzi ,mambo mengine lazima yaendelee kama kawa na hivyo nimeona ni vyema nikawajulisha watanzania wenzangu nini kinachoendelea kwenye soko letu la ajira tokea tufungue milango ya soko huru julai mosi mwaka huu.

  Ikumbukwe kwamba lengo la soko huru lilikuwa ni kufungua milango ya uwekezaji na ufanyaji kazi kwenye eneo letu la Afrika Mashariki kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima na mpaka sasa makubaliano ni kwamba wananchama wa nchi 5 za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi kwenye nchi yoyote ila kwa hapa kwetu wageni lazima waombe vibali vya kufanyia kazi wanapopata kazi hapa kwa muda wa miaka 5 ijayo ambapo vitaondolewa kabisa.

  Hivyo Mkenya, Mganda,Mrundi,au Mrwanda akija hapa akipata kazi kihalali ataomba kibali uhamiaji . Ikumbukwe kuwa wenzetu Wakenya walianza ubepari zamani hivyo si ajabu ni nchi ya 2 kufanya biashara kwa wingi na Tanzania baada ya Uingereza hivyo pia tunategemea wakenya wengi wawepo kufanya kazi Tanzania lakini kwa kushindanishwa na wazalendo .

  Cha ajabu mzee ni kwamba hawa wenzetu badala ya kutumia ushindanishi unaotakiwa sokoni kwa kuangalia vigezo na uwezo wa mtu wao wameanza kutumia propaganda,mizengwe na mbinu nyingine chafu za kuwaondoa watanzania kwenye nafasi zao na kuwapa wakenya.

  Utakuta mtu anapewa kazi kwenye kampuni ya kikenya then anapigwa zengwe kuwa utendaji wake ni mbovu na kesho yake analetwa mkenya hata kama mtanzania ni mzuri kwa vigezo vyote au pia kuna kazi zinahitaji training wao hawatakupa hiyo training kwa makusudi ili ionekane huwezi kazi wamlete mkenya!

  Mbinu nyingine wanayotumia wanakupeleka training kwao Nairobi labda mwezi mzima na huku nyuma wanamleta mkenya anafanya kazi zako kisha wewe ukimaliza training unaambiwa hukufikia vigezo wanavyotaka hivyo ujiuzuru au wakufukuze kazi au watakutafutia kisa chochote tu hata cha maisha yako binafsi yasiyohusiana na kazi yako halafu unatishiwa kuwa watakufukuza au ujiuzuru nwenyewe! Kisha wanaenda uhamiaji kumwombea kibali mkenya wao wakitoa sababu kuwa mtanzania waliyemweka ameshindwa kufikia vigezo wananvyotaka!

  Wadau hizi ni baadhi ya mbinu tu wanazotumia hawa wenzetu kunyakua kazi wa watanzania kwa nguvu ! Kuna mifano mingi na watu wengi wameathirika na hizi mbinu chafu za wakenya hivyo naona muda muafaka umefika wa mamlaka husika kufanyia kazi hili jambo!

  Tunaelewa kuwa Kenya maisha ni magumu sana ndo maana wanakimbilia huku kutafuata kazi wakati hakuna watanzania waliofanikiwa kupata kazi Kenya kwa kuomba tu kwenye makampuni ya Kikenya ukiacha wanaopelekwa na makampuni nya kimataifa yaliyopo Tanzania . Hii ni kwasababu Wakenya wana dharau sana (Kenyans are very arrogant) kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki na wanajiona wao wanajua kila kitu. Hii imesababisha hata wao kwa wao wabaguane kimakabila hivyo kampuni ya Mkikuyu huwezi kumkuta Mjaluo au Mkamba ! hiki ndo chanzo cha wao kuuana mwaka juzi baada ya uchaguzi wao maake kule kwao wanaishi kwa mbinu za msituni (survival of the fittest) .

  Hata hapa kwetu wafanyakazi wengi walio chini ya mabosi wakenya wanadharauliwa na kunyanyaswa kisa ni watanzania hata kama wana uwezo kuwazidi hao wakenya !

  WATANZANIA TUFANYEJE

  Ningependa kuwashauri wadau wanapokutana na hali hii wasikae kimya na kusubiri mungu awasaidie . wajue kwamba huu ni mpango maalum ambao wenzetu wamekuja hapa kupokonya ajira za watanzania hivyo tuchukue hatua madhubuti ambazo ni pamoja nazifuatazo:

  -hakikisha kila unapofanya kitu kizuri ofisini kwako bosi wako anajua .Hii itakusaidia sana wakati wa kureview performance yako kazini . wenzetu wanaijua sana kuitumia mbinu hii inayoitwa corporate politics! Akifanya jambo dogo tu lazima amwambie bosi wake hivyo kujilinda pakitokea tatizo baadaye.

  Watanzania tusikae kimya kusubiri bosi wako aone mwenyewe kuwa wewe unafanya kazi vizuri sana ! mfuate bosi mweleze mafanikio yako kazini na sio kujificha bosi akipita koridoni oooh utakula wa chuya !

  Pili tuhakikishe tunazijua sheria za kazi vizuri na sio kutishiwa tishiwa tu na hawa wakenya wakati nchi ni yetu bwana ! tujenge utamaduni wa kusoma haki zenu ndani ya sheria ya kazi ili likitokea jambo tuweze kujitetea ipasavyo. Japokuwa sheria zenyewe zina mapungufu kwa mfano mwajiri anapewa uhuru wa kuchagua akurudishe kazini au akuachishe kazi na kukulipa mshahara wa miezi 12 tu ! sheria ibadilishwe hii !

  Tatu tujifunze bargaining skills wakati wa kuomba kazi maake utakuta wengi wetu mishahara ni midogo sana kwani wakati wa kuomba kazi tunamwachia mwajiri ajipangie mshahara wa kukulipa matokeo yake hata ukimpeleka mahakamani atakulipa vijisenti vya miezi 12 na kukufukuza kazi huku nafasi yako akipewa Mkenya na kulipwa kama expatriate.

  Nne tungependa vyombo vinavyohusika na kutoa vibali vya kazi kwa wageni (hasa wizara ya mambo ya ndani, wizara ya kazi na professional bodies ) vijiridhishe kweli hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi ambayo kibali kinaombwa. Hivi kweli jamani hatuna wahasibu wa kutosha mpaka Mkenya aje awe management account (mhasibu wa ndani) au financial controller (mhasibu mkuu ) hapa Tanzania wakati NBAA wanatoa CPA mara 2 kwa mwaka ! hawa vijana wanaomaliza hizi qualification watafanya kazi gani sasa ? Tuachane na njaa za muda na utamaduni wa kuabudu wageni ! Tuamini wazalendo na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi .

  Tano watanzania tubadilike tujenge attitude ya kujituma kazini maake soko la kibepari ndo linavyotaka ! ukiwa mvivu kazini wakenya watazidi kuja na kuchukua nafasi zetu nasisi tutaishia kulalamika tu ! hivi sasa mabenki makubwa 3 madirector wao ni Wakenya ! mshahara wa director mmoja tu unatosha kuwalipa watanzania zaidi ya 20 wa ngazi za chini na hapo bado hujazungumzia wenzao waliowaleta toka Kenya na vitu wanavyonunua kwa makampuni yaliyo Nairobi hata kama kuna makampuni ya Tanzania yanazalisha kitu hicho hicho maake bosi ndo mwamuzi !

  Naomba kuwakilisha

  Mdau aliyetendwa na wakenya !!
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..may be Kenyans have better communication skills.

  ..but when it comes to technical knowledge I dont see any difference btn Tanzanians and Kenyans.

  ..actually I think Tanzanians are better in scientific fields than their Kenyan counterparts.

  ..we definatelly need to revamp our education system. the decision to have Swahili as a medium of instructions has come to hurt us in this era of free trade and open markets. I bet u, mchuuzi wa sokoni Kenya anazungumza kingereza kizuri kuliko mhitimu wa sekondari za kata za Tanzania. sasa ktk soko huria ambako waajiri ni investors toka nchi za magharibi unafikiri wa-Tanzania stand any chance?
   
 3. C

  Chamkoroma Senior Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu jambo hili limekuwa nikilio cha siku nyingi sn, kimenifanya kutoa article ile iliyosema kwanini serikali yetu isitangaze kiingeleza kufundishwa toka std hadi chuo kikuu? ninaishi nje kwa muda ss, nimewaona wa key wakihangaika nakupata kazi kirahisi japo si wote wanafanya kazi nzuri sn, lkn lugha imewaweka mahali bora kidogo, nikamuuliza mkubwa mmoja wa sirikali yetu akasema tutaharibu utamaduni wetu, lkn wanawapeleka wanawao nje kusoma kwa ghalama ya sirikali, lkn mkulima toka mkete anabaki nakisawhili akitaka ajila anaambiwa hawezi kujieleza mbele ya kadamnasi ya kiingereza, jamani tumetendewa mambo ambayo yatatugarimu siku nyingi sn hadi kutoka katiak utumwa huu, nawaamia kuwa hakuna hata mwanajeshi mmoja anayefundiswa namna ya kuchunga au kukamua maziwa ya ng'ombe au mbuzi bali mafunzo yakukabiliana na maadui, leo sirikali yetu inatufundisha naman ya kukaa chumbani na lugha ya mama wakati wanasema Globalization is innevitable, let's open our vacancies even to other EACs hii ni ni ubadhilifu ma nguvu kazi, lazima sirikali ingeanza kutufundisha namna ya kupaamnana siyo kutupamabanisha na waliotayari kupambana.
   
 4. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Tanzanians are very competent when they want to work. Kinachotuharibia ni attitude to work. Hii ni moja ya athari za ufisadi. Wengi wanategemea kufanya kazi kidogo kwa manufaa makubwa, by hooks and crooks. Afanane na fulani aliyepata kazi Banki kuu etc. Mwisho wake wengi wanapoajiriwa mipango mikubwa ni kutengeneza pesa haraka na kustarehe.

  Nilizungumza na mjasiriamali MTANZANIA ambaye amewekeza kwenye sekta ya utalii baada ya kukaa kwenye hoteli yake kwa wiki moja na kumuona dada wa reception sio Mtanzania. Aliniomba nisubiri kwa siku tatu. Yule dada anaingia kazini saa 10 usiku, anatoka saa 6 usiku. Kwa masaa yote hayo hakai chini. Anatembelea kila sehemu na ufanisi ni mzuri. Karibu kila mgeni anamuachia tip kwa hiari yake, jinsi anavyohudumia vizuri.

  Baada ya siku tatu aliniita tukazungumza. Sikuwa na la kusema tena. Aliniambia kuwa kwa miaka mitano alikuwa mzalendo sana akaajiri Watanzania. Kwa wastani alikuwa anapata complaints sio chini ya tano kwa siku from unsatisfied customers. By then alikuwa ameajiri vijana wanne wa reception wakibadilishana kwa zamu. Baadhi ya matukio yaliyokuwa yanamsumbua kutoka kwa hawa vijana wetu ni kama yafuatayo; kupangisha vyumba "short time' hata kama vimepangishwa; vitabu vya stakabadhi kupotea, matukio ya wizi vyumbani yasiyoelezeka, malumbano baina ya wafanyakazi wenyewe na watu wa nje (eg. mtu kufuatwa na girlfriend au boyfriend wake na kugombana kazini), nk.

  Tangu alipoajiri waK wawili badala ya hao wanne, hayo yote yalikoma.

  TUFANYEJE KUBADILI HII WORK ATTITUDE ZA WATZ???
   
 5. M

  Msharika JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mweni nimekuboonyezea thanx. Hiyo ni kweli , ufisadi umearibu hari ya kazi
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kweli mtu akawa professional halafu akawa incompetent?.......sijaelewa vizuri hapa
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Kenyans are better polished and they seriously take their duties unlike us in TZ who prefer lip-service to real work.

  Even in this quotation you can see analytical skills are very flimsy................How do you gauge yourself?
   
 8. D

  Dina JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  By calling a spade a spade and not a big spoon, kuna baadhi ya maeneo ambayo waTZ inabidi tujirekebishe kwenye utendaji wetu wa kazi. Some people take for granted kuwa kazi wanazo tayari and the kazi belongs to them, without putting any effort ya kumpa mwajiri sababu ya kuendelea kumuacha kazini. Mtu anaingia kazini kachelewa, akichelewa kutoka anadai overtime! Anafanya kazi masaa yote akiangalia saa, kuwa muda utaisha saa ngapi ili aondoke. Ikija kwenye suala la customer service ndio kabisa tunakosa hata la kuongelea. Ni mara ngapi tunaenda kwenye huduma mahali ukakuta receptionist anaendelea kuongea na simu kana kwamba mbele yake hajaona mtu anayesubiri huduma yake! The list can go on and on ....cha msingi nasi tunatakiwa tufanye kazi kweli kweli vinginevyo tutakesha tukifikiria kupambana na hao wageni tukaacha kufanya ya msingi!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mbona kichwa cha habari kushoto?

  Nway, ishu hii inaenda sambamba na sera ya CCM ya kuabudu wageni (ingawa it is a prven FACT kwamba in most cases hawana input yeyote kwa uchumi wetu, YES NASEMA KWA KINYWA KIPANA), kukuwadia rasilimali kwa wageni badala ya kuzitumia kuwaendeleza wazalendo na kukumbatia ufisadi kila angle.Wahenga wanasema ukitaka kumuua nyoka mtwange kichwani, sasa tutaua ndege 12 kwa jiwe moja tukiwaondoa hawa magullible zombies CCM Oktoba 31. Fursa ndio hiyo ipo kwetu, kufanya ajizi ni kuandika maumivu.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  Mween,

  ..mara nyingi watu wanapokuwa nyumbani wanabweteka kidogo.

  ..vilevile mtu anapokuwa ugenini, hata kama siyo mwaminifu. atakuwa muoga kidogo kujihusisha na wizi.

  ..mara nyingi wageni wanakuwa wachapa kazi zaidi kuliko wenyeji.

  ..nendeni nchi za nje muone wa-Tanzania wanavyosifika kwa uchapa kazi.

  ..wapimeni wa-Tanzania walioko Kenya, vs wa-Kenya wanaofanya kazi Tanzania. nina hakika mtapata picha tofauti kabisa.

  .
   
 11. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Absolutely!
  Depending on how you define a pro.
  You can have a lousy attorney, incompetent physician, a mediocre accountant, and so on.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna lolote ni Ulimbukeni mtupu, Hata ndoa zetu wanaume na wanawake zetu wana prefer foreigners iwe hata Mkenya ni mbora kuliko Mtanzania. Hizi ndio athari za Utumwa wa fikra, wakenya hawana lolote bora kuliko sisi kwani nao ni maskini kama sisi. Wangeweza kujenga kwao kwanza kuliko kuja tafuta kazi Tanzania. Professional wana invent na sio kutafuta ajira wakijua qualification ni lugha ya kigeni. Wakenya wote wanajua hili na wanatudharau kwa sababu hiyo.

  Siku zote immigrant huja kutafuta maisha bora yaliko iwe Marekani kuvamiwa na Wahindi au Mexican, Wachina kujaa Canada na kadhalika. Hii haina maana yeyote zaidi ya ubora wa maisha sehemu wanakokimbilia. Na tukubali kwamba sisi bado washamba na malimbukeni tunababaikia sana Kiingereza cha kuchovya kama mr. Patel hapa.
   
 13. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  You need Kool Aid:hand:
   
 14. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona tunawaangalia Wakenya pekee yao? Kuna Wahindi (Wadosi) kibao kwenye hizi kampuni kibao za wale tunaowaita watanzania wenye asili ya Asia. Hawa huwaleta wafanyakazi wao karibu wote hata walinzi kutoka india wasiojua hicho Kingereza achilia mbali kiswahili. (mifano ni mingi sana ila nenda Funcity Kigamboni utashangaa ya Musa, nenda kwa Manji quality,KTM nk)

  Wahindi ndio hawafai kabisa na huyo Raj Ratel ndiye nyoka wa kwanza, hawa ni wabaguzi sana acha suala la kutudharau. Binafsi naona sisi watz tuna matatizo makubwa lakini lawama nyingi lazima zibebwe na watawala wetu ambao kila kitu zaidi ya maslahi yao binafsi kiko hands off!!!!

  Hapa hakuna suala la lugha ya kiingereza ila ni watawala wetu kutokujua vipaumbele vyetu, wakati Nyerere na Mzee Karume walikuwa wakipigania ku- export Kahawa, Pamba, karafuu, Chai, mkonge nk., leo watawala wetu wanahangaika na ku-import kuanzia chupi za mitumba, makocha wa mpira, walinzi wa mageti, watafiti wa kilimo kwanza na madini, walimu wazee kutoka marekani nk .

  Wewe jiulize hicho kiswahili chetu kinachopendwa dunia nzima kinatusaidiaJe? je kuna fedha za kigeni zinaingia kupitia kiswahili? je tumeisha ona umuhimu wa ku-export waalimu wa kiswahili au watangazaji wa radio kwenye radio za kimataifa? Wakenya ndio wanaotawala katika idhaa za kiswahili dunia nzima licha ya kiswahili kuwa cha kubabaishia. Ndio wanaofundisha Kiswahili huko ughaibuni na si muda mrefu watakuja hata kutufundisha hapa kwetu!

  Sijui sisi tumelogwa na nani?
   
 15. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisikia akili fupi basi ndiyo hii.

  Sasa mbona hujamtaja Reginald Mengi aliyewajaza Wahindi na Wakenya kule IPP Media? Mbona huzungumzii Mkono aliyewajaza Wazungu na Wahindi?

  Jitu kutwa liko JF, muda wa kufanyakazi utaupata wapi?

  Nani kakudanganya Kiswahili kinapendwa dunia nzima? Kama siyo ushahidi wa akili fupi ni kitu gani? :A S 13:
   
 16. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kujidanganya Mukandara. Wahindi (software engineers na IT gurus) wanaenda Marekani kwa sababu kuna demand kwa ajili yao. Mbona huoni wote wakikimbilia Switzerland ama Sweden kwenye maisha mazuri bora zaidi kuliko hata Marekani? Hivyo hivyo hao Wamexican, kwani huko Marekani wanapata kazi zile ambazo Wamarekani wengi hawataki kuzifanya kwa moyo, yaani what is called dirty jobs.

  Hivyo hivyo Wakenya wanapokuja hapa ni kwa sababu washaona udhaifu wa Watanzania. Mtu anatoka chuo kikuu hata kuandika barua ya kuomba kazi mpaka aka-google. Kuongea kwa kujieleza kuhusu profession yake ni almost zero. Wewe angalia watu wanavyotoa hoja kwenye ukumbi huu, unaweza ukajua yupi aliyepoteza miaka 4 pale UDSM pamoja na fedha za walipa kodi na yupi kidogo anaweza kufaa. :hand:
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,433
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Haya mawazo ni mazuri na yamejaa ukweli mtupu!! Nashangaa wanaona eti kiingereza ndio tatizo! Hebu tujiulize: Kuna vi-nchi vidogo kama Norway, Sweden na Finland wana maendeleo makubwa kabisa kabisa na hawatumii kiingereza kama Tanzania! Hapo mna la kusema...?
   
 18. K

  Kashishi JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 1,101
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mia kwa mia ndugu yangu. Na pamoja na ulalamishi wetu wote juu ya Wa-Kenya lazima tukubali wenzetu wako juu katika soko la kazi. Jambo la kwanza ni mawasiliano (communication skills) na kujiamini (confidence) katika kujieleza na utendaji wa kazi. Na katika enzi hizi za ubepari wa sekta binafsi, hizo ndio vigezo vikubwa mwajiri anavyoangalia anapofanya usahili (interview). Na hata kama Mtanzania ana qualification za kutosha mathalani shahada ya CPA bado unakuta anaanguka kwenye usahili, kwa kushindwa kwenye vigezo nilivyo vitaja.

  Kitu kingine kinachotuangusha ni cofidence kazini jambo ambalo linatufanya kutokuwa creative katika post zetu. Hii ni ile hali kushindwa kuwa techinical /creative na kushindwa kufanya maamuzi ya haraka (yaani ku-solve issues) katika mtitiriko wa kazi za kila siku. Tuna tabia ya ku-delegate kila kitu ngazi za juu zaidi kwa maamuzi zaidi, na kufanya kuonekana kupwaya katika position zetu. Na hili ni tatizo kubwa hata Mawizarani mwetu (Na hata Mawaziri wanasubiria kila kitu Rais ndio a-solve) na hata kwenye ofisi za umma. Kila kitu tumezoea kesho.

  Kuna mengi ya kuelezaa lakini imefika mahali serikali ianze kuboresha mfumo wetu wa elimu. Kwa kweli haujitoshelezi kum-tayarisha M-Tanzania kwenda kupanda katika sehemu za Ushindani wa Kimataifa. Na kama hivyo si sivyo na tujiulize ni kwa nini Wakubwa wote wa nchi watoto wao wanasoma nje halafu wanarudi nyumbani kwenda kupata nafasi zehemu ambazo ni nono ki-maslahi. Unapoona unauliza mtoto wa darasa la 7 au fomu 2 swali na anatazama chini akishindwa kujieleza au kwa sababu hana confidece yake mwenyewe au lugha ndio haipandi, basi ujue kuna tatizo kubwa kabisa katika mfumo wa elimu. Na pengine matarajio yake ndio haya tunayo yalalamikia hapa tukifika kwenye ushindani wa soko la kazi kama hii ya issue ya EAC.
   
 19. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na hii generalization. More competent to properly perform which specific job(s)? Mbona kuna hao Watz wanaodaiwa ni incompetent wengi tu wameajiriwa Kenya - vyuo vikuu, kwenye mashirika ya simu, nk.
   
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Khe khe khe khe lugha imekuwa issue. Tatizo ni serikali ya kifisadi iliyojaa Mafisadi ambao wanafikiria kujificha kwenye jumuiya kwa kuwaalika mafisadi wenzao. Hakuna uzalendo kwa sababu wao wamechota cha kutosha na wanafikiri walichokomba kitawatosha wao wenyewe na wajukuu pamoja na vitukuu hadi kiama. Uhamiaji wanatoa vibali kwa rupia wakishirikiana na wizara ya kazi etc.

  Siku atakayoingia mzalendo ndio kifo cha EAC. Kwanini tunabebeshwa mzigo wa Manyang'au? Nchi hii itajengwa na Watanzania na sio wageni au kutegemea misaada koko.
   
Loading...