Kenya yazuia ndege za UAE ili kulipiza kisasi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,872
Kenya imesitisha safari zote za ndege za abiria zinazoingia na kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ili kulipiza kisasi hatua ya Dubai ya kupiga marufuku safari zote za ndege za abiria kutoka Kenya kutokana na vipimo bandia ya Covid-19.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) Gilbert Kibe ameliambia gazeti la The EastAfrican siku ya Jumanne kwamba kusimamishwa huko kulianza Jumatatu usiku wa manane kwa muda wa siku saba.

Marufuku hiyo hata hivyo haiathiri safari za ndege za mizigo ambazo kwa kawaida husafirishwa na wachukuzi kama vile Kenya Airways na shirika la ndege la Emirates kutoka UEA hadi Kenya.

"Safari za ndege za abiria za ndani na nje kutoka UAE zimesitishwa kwa muda wa siku saba. Tunafanya hivi ili kujibu marufuku ya safari za ndege za abiria za Kenya kuelekea UAE," alisema Bw Kibe Jumanne.

Marufuku hiyo inajiri siku chache tu baada ya UAE kuongeza muda wa marufuku ya safari za ndege nchini Kenya baada ya kubaini kuwa wasafiri kutoka Nairobi walipimwa na kukutwa na Covid-19 baada ya kuwasili katika taifa hilo la Mashariki ya Kati, licha ya kuwa na matokeo yaliyoonyesha kwamba hawakuwa na virusi vya Covid .
 
Maumbw@ hao. Ni vizuri tumelipiza kisasi. Jambo hili liliniuma sana kuona jinsi nchi hii ya ujinga ya Kiarabu inavyoban ndege na abiria kutoka Africa wakidhani wao ni Mungu. Tit for tat is a fair game. Hata Nigeria waliban UK kwa sababu hii hii.
Usituingize kwenye migogoro yenu. Ni Kenya vs falme za kiarabu. Tanzania hatuhusiki
 
Kenya ilipozuia abiria kuingia Kenya kwa sababu hiyohiyo na Tanzania tulipolipiza kisasi wewe ni miongoni mwa watu waliomsema vibaya Sana Magufuli, Leo unahalalisha Kitendo cha Kenya kulipiza kisasi, kweli Kenya ni nchi ya watu wa hovyo Sana.
 
Ukipigana ngumu na ukuta, utaumia wewe. Hoja ya Kenya ni ya kuipuuza sana tu. UAE yenyewe angalau ilikuwa na hoja ya UVIKO-19. Sasa wao wanasema wazi ^wanalipiza kisasi!^ That's insane! It's foolish! Wanamkomoa nani?

Halafu Uhuru juzi hapa alijifanya kumshauri Anko wa Chattle eti awe gentleman. Really Mr President?
 
Nyie mtahusikaje ilhali ndege zenu hazitoki nje ya Tanzania? Ndege zenu zinapiga route za daladala hapo Tanzania.
Ndio ujue kiwango cha maendeleo hapa kwetu, kama ndege zimefikia hatua ya kuzagaa kama daladala. Pole sana. Mlaumuni Mr Uhuru amelewa madaraka. At least this year anafurushwa kutoka State House, aingie kiongozi mahiri, Dkt. WSR.
 
Sisi hatutaki ujinga wa waarabu.
 
Nyie mtahusikaje ilhali ndege zenu hazitoki nje ya Tanzania? Ndege zenu zinapiga route za daladala hapo Tanzania.
Kama hujui vitu uwe unasema ueleweshwe. Usicomment kwa mihemko.
Kwa kifupi biashara huwa inafanyika kwa nchi zote mbili, ndio maana nchi zina-sign mikabata kwa ajili ya mashirika ya ndege ya mataifa yao. Mikataba hiyo inaitwa bilateral air service agreement(BASA).
 
Kwa hivyo? What is your point? Sijakuelewa.
 
Maumbw@ hao. Ni vizuri tumelipiza kisasi. Jambo hili liliniuma sana kuona jinsi nchi hii ya ujinga ya Kiarabu inavyoban ndege na abiria kutoka Africa wakidhani wao ni Mungu. Tit for tat is a fair game. Hata Nigeria waliban UK kwa sababu hii hii.
Hicho kisasi naona kama ni kichekesho UAE wamepìga ban ndege za abiria kutoka kenya kwenda UAE this ban includes ndege zao pia zinazokuja Kenya sasa na nyie mnapiga marufuku nini tena wakati ban imeshapifwa na UAE?
 
Ndege yao ilikuja Kenya jana usiku. Hio ndio imefanya kibano wakipokee leo. Eti walisitisha ban jana baada ya siku kadhaa za ban
 
Usituingize kwenye migogoro yenu. Ni Kenya vs falme za kiarabu. Tanzania hatuhusiki
Umejiingiza mwenyewe boss. Wapi kataja Tanzania? Stop making yourself important. Tunaongelea like minded African countries like Nigeria ambazo pia zilibaniwa na zikalipiza. Not non-entities like Tanzania that barely get any flights from UAE. 🤣🤣🤣
 
Ndio ujue kiwango cha maendeleo hapa kwetu, kama ndege zimefikia hatua ya kuzagaa kama daladala. Pole sana. Mlaumuni Mr Uhuru amelewa madaraka. At least this year anafurushwa kutoka State House, aingie kiongozi mahiri, Dkt. WSR.
sasa ndege 11 ndio unasema kuzagaa? 🤣🤣
 
Back
Top Bottom