Kenya yanufaika na Mt Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya yanufaika na Mt Kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by idumu, Jun 15, 2009.

 1. idumu

  idumu Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani watz mko wapi?? Kenya imekuwa ikitumia mlima kilimanjaro kwa manufaa ya nchi hiyo Mfano Kwas sasa wanautanganza Mt kiliamnjaro kupitia DSTV kwenye mashindano ya FIFA CONFEDERATION CUP yaliyoanza Tar 14 June 2009, kwa kutoa tangazo:
  Mt kilimanjaro - " MASAI KENYA"

  Wizara ya Utalii mpo?? MBONA MMELALA.
  ndg Rais JK WAAMSHE HAWA MAWAZIRI wanatuangusha
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  WANA JF,
  Habari hii ina ukweli kiasi gani?
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wakenya hawakuanza leo kufaidika na mlima Kilimanjaro. Wameanza miaka mingi nenda rudi. Sisi bado tunaupiga usingizi wa pono!
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wao ni wabunifu na wachacharikaji kwenye biashara hasa hii ya utalii.
  Kwa vile mlima huo unaonekana pia Kenya, tunategemea nini wakati tunadengua na kung'ang'ania kodi na ada kubwa?
   
 5. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hahaha,
  hahaha,
  ni kweli kenya inanufaika sana na mlima kilimanjaro,na mara nyingi hata ukienda nchi za watu huko wanajua mlima kilimajaro upo kenya sio tz...
  tatizo letu sisi wa tz tumekaa mkao wa 10%...waziri wa utalii hadi ale cha juu a.k.a 10% dio utaona anashupalia ishu ya utalii..ukiona yupo kimya ujue kachungulia kaona hamna cha juu,ndo maana haoni haja ya kukomaa na kutangaza mlima huo..
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  As long as Wakenya hawajiingizi katika deceptive ads za kusema Mlima Kilimanjaro uko kwao, wakiwa wabunifu kuvutia watalii kwao hatuwezi kuwakataza.It is not like wako Afrika Kusini ambako mlima hata hauonekani, mlima unaonekana kwao, sasa kama na sisi tunataka kufaidika tuwaambie watalii tuna "international" airport KIA pamoja na vivutio vingine vya watalii.

  Lakini hatuwezi kuwakataza kutumia mlima unaoonekana kwao -na slopes zimeingia mpaka kwao- kwa ukwasi tu.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jun 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi hayo maoni hapo juu kwamba hatuwezi kuwakataza kutangaza mlima wetu ni ya watz kweli au? I cant believe it! Kwa mawazo Ndio maana hawa jamaa wanapeta bila wasiwasi wowote. Nasikia hata mbuga ya Serengeti wanadai iko kwao. What stupid Kenyans! Huu si ubunifu ni utapeli! Ukisikia jirani yako anadai mke wako ndiye mkewe utajisikiaje? Au ndio notion kwamba mali ya umma haina uchungu?
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ninaomarafiki wengi raia wa Kenya huku ugaibuni, hawasiti kunieleza hata mimi kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya na Tanzania. Kunasiku tulibishana sana mpaka tukaingia google map ndo wakakubali. Hata hivyo hitimisho lao lilikuwa ni ukiwa Kenya unauona mlima wote. So, Kenya wanaamini kuwa mlima ule tuna-share.
   
 9. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unajua ni kwa nini kenya wanafanikia sana kwenye sekta ya utalii? na ni kwa juhudi za nani? ni za wananchi wenyewe wako busy kuitangaza nchi yao kila pembe ya dunia.
  ukitaka kujua ni kwa nini wanatuzidi kete wenzatu tembeleeni hapa mjione wenyewe.https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/30869-tuitangaze-tanzania-yetu-kwenye-mitandao.html

  nilipo anzisha thread (tuitangaze tanzania kwenye mtandao) waliifungua watu 19 tu.ikimaanisha hakuna mtu mwenye muda wakuitangaza nchi yake.
   
  Last edited: Jun 15, 2009
 10. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  We endelea kumsubiria Waziri wa utalii aitangaze tanzania watati wewe mwenyewe unaweza kuitangaza.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jun 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mlima kuonekana kwao sio kitu. Basi wangetangaza unaonekana kwao kuliko uko kwao. Sio uchakarikaji ni ujinga! Hakuna nchi inayong'ang'ania kusema sehemu fulani ya nchi ni ya kwake wakati sio hivyo. Ndio maana wanagombana na waganda juu ya kasehemu kadogo ambako watu mia hamsini wakisimama hawaenei.
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kabla hujajua wanatangaza nini huwezi kushabikia tu.Vipi kama wanatangaza "slopes of Mount Kilimanjaro" kwa watu ambao hawawezi kupanda mlima lakini wanataka kupiga picha kutoka katika slopes za mlima zilizopo Kenya? Tukumbuke pale ulipo mlima Kilimanjaro ukivuka mpaka kuingia kenya ni mbuga za Wanyama za Tsavo, sasa mnataka katika brochures za Tsavo West National Park wasiweke backdrop ya Mlima Kilimanjaro? Backdrop ambayo ni kweli ukienda Tsavo National Park unaiona?

  [​IMG]

  Badala ya kulalamika tufanye kazi ya kuueleza ulimwengu kwamba mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya. Ni rahisi kutafuta mchawi wa kumlalamikia zaidi ya kutafuta chanzo cha kweli cha matatizo kinachotuhusu sisi wenyewe.

  Ni rahisi kusema Wakenya wanautangaza mlima kama wao zaidi ya kujenga mahoteli ya kimataifa, yenye wafanyakazi wa kiwango cha kimataifa na kuwaleta watalii moja kwa moja kutoka kwao.

  Tuache ulalamishi na tufanye kazi. Na mpaka tutakapoona ushahidi wa tangazo linalosema "Mlima Kilimanjaro upo Kenya" or something to that misleading effect, tutakosa hekima kuwashutumu. Na Wakenya wana haki ya kutangaza utalii wa kupiga picha mlima Kilimanjaro kutoka slopes zake zilizopo Kenya, kwani mlima uko mpakani.
   
  Last edited: Jun 15, 2009
 13. I

  Ipole JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na wanachotangaza wao sio mlima upo kwao wanachosema njoo Kenya uone Kilimanjaro
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Na hiyo haina ubaya!
  Watanzania tuache visingizio tuchape kazi.
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sawa sawa,

  Which is a bit tricky.kwa sababu wanaweza kukuleta mpaka Kenya, ukaingia mbugani, wakakupeleka mpaka karibu ma mlima upande wa Kenya, ukapiga picha na kurudi kwenu.

  Na hata kama unataka kupanda mlima wana arrange kukufanyia shughuli zote za border crossing unaingia Tanzania kiulaini, pengine bila hata kujua kuwa umeingia nchi nyingine.

  Kama Wakenya ambao mlima hauko kwao wanaweza kufanya hivi, sisi wenye mlima tunashindwa nini kufanya biashara hii vizuri sana? Tatizo letu si Wakenya, ni umadhubuti wetu kibiashara.Sisis tulitakiwa tuufanyishe mlima biashara ya utalii kwa kiasi kikubwa (peak kama ilipo peak ya kilimanjaro) na Wakenya wapate slopes za biashara hii, kama vile mlima ulivyokuwa umefika kwao katika slopes tu.Badala yake tunalalamika Wakenya wanatuzidi.

  Hebu tuone mfano mmoja wa random kutoka Tsavo West tuone kama wanadai mlima upo Kenya.Ingawa hawajakuwa wakweli kabisa kwa ku disclose mlima hauko Kenya, hawakudanganya na kusema mlima uko Kenya, wanasema tu njoo uone mlima Kilimanjaro.

  Ni kama vile leo ma tour guides wa Zanzibar wakianzisha safari za Mombasa bila kudai kwamba Mombasa ipo Zanzibar wala kuwaambia watalii kuwa Mombasa ipo Kenya. Itakuwa sio full disclosure, lakini pia itakuwa si uongo.


  Tsavo West & East National Park: Wildlife Safaris|Mt.kilimanjaro Tours|Beach Safari
   
Loading...