Kenya yampongeza JK kwa hotuba yake bungeni

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,343
Reaction score
20,797
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Amina Mohamed anayetembelea nchini amempongeza JK kwa hotuba yake aliyoitoa bungeni wiki hii na hasa tamko lake la Tanzania kutojitoa katika EAC.

Bibi Amina amekuja nchini pamoja na mambo mengine kujadili uhusiano baina ya nchi zetu na pia mtafaruku uliojitokeza katika uhusiano wa nchi zilizomo katika EAC.

Wana JF:
Je hatua ya Amina kuja nchini ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia zinazochukuliwa na Kenya ili kurejesha mtengamano wa EAC?
Kwa upande wake, Kenya moja ya nchi waanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki na ambayo ilishutumiwa kushiriki kuibagua Tanzania, imemtuma waziri wake wa mambo ya nje, Amina Mohammed kwenda Tanzania na kuwa na mazungumzo na waziri mwenzie wa mambo ya nje Bernard Membe kuhusu mfarakano huo na nia ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili hizo.

Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumapili, waziri Amina Mohammed, amesema Kenya inaunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, kuhusu uamuzi wake wa kutojitoa katika Jumuia ya Afrika Mashariki, huku akisisitiza kuwa bila Tanzania hakuna Afrika Mashariki na bila Afrika Mashariki hakuna Tanzania.

"Kama unavyojua Kenya na Tanzania tumekuwa tukiijenga jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu sana, tuko na mafanikio mengi sana, kuna mambo mengi tumeyafanya, kuna njia ndefu imebakia kuna mambo mengi yasiyoweza kupimwa kati ya nchi hizi. Na tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashriki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na waendelee . Kwa Tunataka uchumi wetu uende vizuri. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana, sisi ni wale wa kwanza tuliokuwa pale kwa hiyo tunataka tufanye kile tunachoweza kuendeleza Afrika Mashariki..... Lakini tumefurahia sana sana hotuba ya Rais aliyotoa pale bungeni na tunawashukuru pia Watanzania kumuunga mkono."

Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa kindugu

Pia waziri Amina amesisitiza kuwa hakuna namna ambavyo Tanzania na Kenya zitatenganishwa, kwa namna ambavyo zimejenga maingiliano makubwa ya kijamii na kiuchumi, huku akiomba Tanzania kusaidia kusukuma ombi la Kenya la kutaka kesi ianyomkabili Rais wake, Uhuru Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi ili kumpa fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Benard Membe amesema serikali yake imefurahi kuona Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza Tanzania kwa kuinusuru jumuia ya Afrika Mashariki kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na si ya viongozi, na kuahidi kushirikiana na Kenya katika masuala mbalimbali likiwemo la kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi.

Waziri Membe amesema waziri mwenzake Amina kutoka Kenya amesema hotuba ya Rais Kikwete imewazindua kwani hawakujua kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ni kukiuka taratibu za Jumuia ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa Kenya itashirikiana kikamilifu na nchi waanzilishi halisi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Katika kuonyesha nia thabiti ya kutotoka katika Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Kikwete katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, alisema "Tanzania ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuia na kuhusika kikamilifu katika ujenzi wake."alisema.

Chini ni Link ya Habari hiyo
BBC Swahili - Habari - Kenya yaiunga mkono Tz A.Mashariki
 
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Amina Mohamed anayetembelea nchini amempongeza JK kwa hotuba yake aliyoitoa bungeni wiki hii na hasa tamko lake la Tanzania kutojitoa katika EAC.

Bibi Amina amekuja nchini pamoja na mambo mengine kujadili uhusiano baina ya nchi zetu na pia mtafaruku uliojitokeza katika uhusiano wa nchi zilizomo katika EAC.

Wana JF: Je hatua ya Amina kuja nchini ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia zinazochukuliwa na Kenya ili kurejesha mtengamano wa EAC?

Ndiyo, ndio jibu!
 
Kwa upande wake, Kenya moja ya nchi waanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki na ambayo ilishutumiwa kushiriki kuibagua Tanzania, imemtuma waziri wake wa mambo ya nje, Amina Mohammed kwenda Tanzania na kuwa na mazungumzo na waziri mwenzie wa mambo ya nje Bernard Membe kuhusu mfarakano huo na nia ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili hizo.

Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumapili, waziri Amina Mohammed, amesema Kenya inaunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, kuhusu uamuzi wake wa kutojitoa katika Jumuia ya Afrika Mashariki, huku akisisitiza kuwa bila Tanzania hakuna Afrika Mashariki na bila Afrika Mashariki hakuna Tanzania.

"Kama unavyojua Kenya na Tanzania tumekuwa tukiijenga jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu sana, tuko na mafanikio mengi sana, kuna mambo mengi tumeyafanya, kuna njia ndefu imebakia kuna mambo mengi yasiyoweza kupimwa kati ya nchi hizi. Na tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashriki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na waendelee . Kwa Tunataka uchumi wetu uende vizuri. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana, sisi ni wale wa kwanza tuliokuwa pale kwa hiyo tunataka tufanye kile tunachoweza kuendeleza Afrika Mashariki..... Lakini tumefurahia sana sana hotuba ya Rais aliyotoa pale bungeni na tunawashukuru pia Watanzania kumuunga mkono."

Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa kindugu

Pia waziri Amina amesisitiza kuwa hakuna namna ambavyo Tanzania na Kenya zitatenganishwa, kwa namna ambavyo zimejenga maingiliano makubwa ya kijamii na kiuchumi, huku akiomba Tanzania kusaidia kusukuma ombi la Kenya la kutaka kesi ianyomkabili Rais wake, Uhuru Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi ili kumpa fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Benard Membe amesema serikali yake imefurahi kuona Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza Tanzania kwa kuinusuru jumuia ya Afrika Mashariki kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na si ya viongozi, na kuahidi kushirikiana na Kenya katika masuala mbalimbali likiwemo la kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi.

Waziri Membe amesema waziri mwenzake Amina kutoka Kenya amesema hotuba ya Rais Kikwete imewazindua kwani hawakujua kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ni kukiuka taratibu za Jumuia ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa Kenya itashirikiana kikamilifu na nchi waanzilishi halisi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Katika kuonyesha nia thabiti ya kutotoka katika Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Kikwete katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, alisema "Tanzania ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuia na kuhusika kikamilifu katika ujenzi wake."alisema.

Chini ni Link ya Habari hiyo
BBC Swahili - Habari - Kenya yaiunga mkono Tz A.Mashariki
 
Rwanda wafanye hivo hivo pia kutuliza hasira za watanzania.
 
Kenya imekuwa nchi ya kwanza kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki kuipongeza Tanzania kwa hatua yake ya kutangaza bayana kwamba haiko tayari kutoka katika jumuiya hiyo kama ilivyodhaniwa.
Wasiwasi kuwa Tanzania ingejitoa kutoka jumuia ya Afrika Mashariki ulitokana na hali iliyojitokeza kwa baadhi ya nchi za jumuia hiyo kuendesha mikutano yao bila kuishirikisha Tanzania na Burundi.
Taarifa zinazohusiana
Kenya, Tanzania
Baadhi ya wanasiasa na wananchi nchini Tanzania walitaka nchi yao iachane na jumuia hiyo wakizishutumu Kenya, Rwanda na Uganda kuitenga Tanzania hata katika mikutano ya masuala yaliyohitaji maamuzi ya jumuia.
Kufuatia mfarakano huo, ulionekana kutishia uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, wiki hii alilihutubia bunge la Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, katikati ya nchi na kutangaza bayana kuwa Tanzania haitatoka katika jumuiya ya Afrika Mashariki, kwani imefanya kazi kubwa kuifufua na kuiunda upya baada ya kusambaratika mwaka 1977.
Kwa upande wake, Kenya moja ya nchi waanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki na ambayo ilishutumiwa kushiriki kuibagua Tanzania, imemtuma waziri wake wa mambo ya nje, Amina Mohammed kwenda Tanzania na kuwa na mazungumzo na waziri mwenzie wa mambo ya nje Bernard Membe kuhusu mfarakano huo na nia ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili hizo.
Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumapili, waziri Amina Mohammed, amesema Kenya inaunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, kuhusu uamuzi wake wa kutojitoa katika Jumuia ya Afrika Mashariki, huku akisisitiza kuwa bila Tanzania hakuna Afrika Mashariki na bila Afrika Mashariki hakuna Tanzania.
"Kama unavyojua Kenya na Tanzania tumekuwa tukiijenga jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu sana, tuko na mafanikio mengi sana, kuna mambo mengi tumeyafanya, kuna njia ndefu imebakia kuna mambo mengi yasiyoweza kupimwa kati ya nchi hizi. Na tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashriki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na waendelee . Kwa Tunataka uchumi wetu uende vizuri. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana, sisi ni wale wa kwanza tuliokuwa pale kwa hiyo tunataka tufanye kile tunachoweza kuendeleza Afrika Mashariki..... Lakini tumefurahia sana sana hotuba ya Rais aliyotoa pale bungeni na tunawashukuru pia Watanzania kumuunga mkono."
Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa kindugu

Pia waziri Amina amesisitiza kuwa hakuna namna ambavyo Tanzania na Kenya zitatenganishwa, kwa namna ambavyo zimejenga maingiliano makubwa ya kijamii na kiuchumi, huku akiomba Tanzania kusaidia kusukuma ombi la Kenya la kutaka kesi ianyomkabili Rais wake, Uhuru Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi ili kumpa fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.

Benard Membe,waziri wa mambo ya nje wa Tanzania
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Benard Membe amesema serikali yake imefurahi kuona Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza Tanzania kwa kuinusuru jumuia ya Afrika Mashariki kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na si ya viongozi, na kuahidi kushirikiana na Kenya katika masuala mbalimbali likiwemo la kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi.
Waziri Membe amesema waziri mwenzake Amina kutoka Kenya amesema hotuba ya Rais Kikwete imewazindua kwani hawakujua kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ni kukiuka taratibu za Jumuia ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa Kenya itashirikiana kikamilifu na nchi waanzilishi halisi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Katika kuonyesha nia thabiti ya kutotoka katika Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Kikwete katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, alisema "Tanzania ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuia na kuhusika kikamilifu katika ujenzi wake."alisema.
Rais Kikwete alitumia muda mrefu katika hotuba hiyo kuchambua masuala mbalimbali ya msingi ya uhai wa jumuia hiyo huku akisema ameshangazwa na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kuzitenga Tanzania na Burundi.BBC
 
K...,

Benard Membe amesema serikali yake imefurahi kuona Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza Tanzania kwa kuinusuru jumuia ya Afrika Mashariki kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na si ya viongozi, na kuahidi kushirikiana na Kenya katika masuala mbalimbali likiwemo la kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi

...

Amenichefua hapo kwenye red; in fact hilo ndilo lengo kuu la ziara ya Waziri Amina Mohamed, mengine ni blah blah tu.
 
Rwanda wafanye hivo hivo pia kutuliza hasira za watanzania.

Thubutu! Wale watutsi walivyo na viburi na dharau kamwe hawawezi kufanya hivyo. In fact habari zilizopo ni kwamba wanataka kurudi kwenye Muungano wa Nchi za Afrika ya Kati (Central Africa Regional Bloc). Ni mabingwa wa kuharibu mahusiano na vigeugeu balaa.
 
Kuna mambo mengi sana yametokea hapa Africa Mashariki.
1. Tulipowakea Rwanda na Burundi tuliwapokea kwa MASHAKA! Tuliogopa wasije kuleta shari zao kwetu. Tumeona Rwanda inavyomwaga sumu. Mbaya zaidi Katibu Mkuu wa EAC ni Mnyarwanda na tumeona madhara yake. Ni sumu tu.

2. Kenya wamekuwa ndumila kuwili na wanafiki sana. Wanajua ukiitenga Tanzania wao watakuwa wanahudumia Landlocked Uganda, Burudi na Rwanda.

3. Burudi hawajui kabisa nini kinaendelea EA. Utawala wao wa kibabe hivyo wanashughulika na wapinzani tu.

4. Tanzania sisi NI WASWAHILI SANA. Hatufanyi chochote lakini tunasubiriatokeo tu! Juzi Rais Kikwete analalamika HATUALIKWI! Kwani kuna nchi ya kualika wenzake? Tatizo ni uswahili. Tumebaki na Ardhi. Ajira. Wivu. Wote huo ni uswahili tu. Kwa waziri Sitta kazi yake ni nini? Tufanye kazi.
 
vizuri kwa kwenya kuitambua tanzania na kumtuma waziri wake lakini kuwe na nia ya kweli kuimalisha umoja huu.rwanda ndio kila kitu ktk mfarakano ni dhahiri hata katika kuisaidia m23.jumuia ni lazima waitazame zaidi rwanda
 
Kuna mambo mengi sana yametokea hapa Africa Mashariki.
1. Tulipowakea Rwanda na Burundi tuliwapokea kwa MASHAKA! Tuliogopa wasije kuleta shari zao kwetu. Tumeona Rwanda inavyomwaga sumu. Mbaya zaidi Katibu Mkuu wa EAC ni Mnyarwanda na tumeona madhara yake. Ni sumu tu.

2. Kenya wamekuwa ndumila kuwili na wanafiki sana. Wanajua ukiitenga Tanzania wao watakuwa wanahudumia Landlocked Uganda, Burudi na Rwanda.

3. Burudi hawajui kabisa nini kinaendelea EA. Utawala wao wa kibabe hivyo wanashughulika na wapinzani tu.

4. Tanzania sisi NI WASWAHILI SANA. Hatufanyi chochote lakini tunasubiriatokeo tu! Juzi Rais Kikwete analalamika HATUALIKWI! Kwani kuna nchi ya kualika wenzake? Tatizo ni uswahili. Tumebaki na Ardhi. Ajira. Wivu. Wote huo ni uswahili tu. Kwa waziri Sitta kazi yake ni nini? Tufanye kazi.
Hapo kwenye red nimecheka sana mkuu,
 
Waziri Membe amesema waziri mwenzake Amina kutoka Kenya amesema hotuba ya Rais Kikwete imewazindua kwani hawakujua kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ni kukiuka taratibu za Jumuia ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa Kenya itashirikiana kikamilifu na nchi waanzilishi halisi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Amateurish president (& VP)? Au kesi ya mauaji ya kimbari na ubakaji imewachanganya kiasi kwamba hawawezi kufikiri sawasawa?
 
Back
Top Bottom