G
Wasitake kuzuga eti walikuwa hawajui, badala yake walifanya makusudi, na hii isiwapumbaze hapo wameuma na wamekuja kupulizia. Hapo ni kujaribu kuwazubaisha, inatakiwa uongozi wa TZ uwe madhubuti na kuendelea na mipango madhubuti ya miundo mbinu na ushirikiano wa kiuchumi na DRC.
Kuna mtu humu anaweza kunambia siye hua tunauza kitu gani Kenya?
Huyu hana lolote katumwa na bosi wake aje kuiomba tanzania impugie debe asije akapelekwa kwenda kunyea debe
Kuna mambo mengi sana
yametokea hapa Africa Mashariki.
1. Tulipowakea Rwanda na Burundi tuliwapokea kwa MASHAKA! Tuliogopa
wasije kuleta shari zao kwetu. Tumeona Rwanda inavyomwaga sumu. Mbaya
zaidi Katibu Mkuu wa EAC ni Mnyarwanda na tumeona madhara yake. Ni sumu
tu.
2. Kenya wamekuwa ndumila kuwili na wanafiki sana. Wanajua ukiitenga
Tanzania wao watakuwa wanahudumia Landlocked Uganda, Burudi na Rwanda.
3. Burudi hawajui kabisa nini kinaendelea EA. Utawala wao wa kibabe
hivyo wanashughulika na wapinzani tu.
4. Tanzania sisi NI WASWAHILI SANA. Hatufanyi chochote lakini
tunasubiriatokeo tu! Juzi Rais Kikwete analalamika HATUALIKWI! Kwani
kuna nchi ya kualika wenzake? Tatizo ni uswahili. Tumebaki na Ardhi.
Ajira. Wivu. Wote huo ni uswahili tu. Kwa waziri Sitta kazi yake ni
nini? Tufanye kazi.
Kitu from Mwananchi hiki!...it is important to do as suggested...mleta uzi!Please avoid plagiarism by acknowledging the source. Haya umeyapatakwenye gazeti au matandaoni?