Kenya Yajitosa Sakata la Ulimboka

Kenya Yajitosa Sakata la Ulimboka

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
SUALA la Joshua Mulundi anayetuhumiwa kumteka Dk Steven Ulimboka, katika Misitu ya Pande, limechukua sura mpya baada ya ubalozi wa Kenya nchini kuamua kumchunguza, ili kubaini kama kweli ni raia wake au la.

Balozi wa Kenya nchini, Mtindo Mutiso aliliambia gazeti hili juzi kuwa amesikia taarifa za Mulundi akidai kuwa ni raia wa Kenya, lakini kama nchi, itahitaji kujiridhisha kabla haijajiingiza kumsaidia kwa lolote. Mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa haijulikani yuko mahabusu
gani baada ya kuhamishwa kutoka Gereza la Keko jijini Dar es Salaam kutokana na ufuatiliaji wa vyombo vya habari, amenukuliwa mara kadhaa na baadhi ya magezeti (siyo Mwananchi) kwamba hatendewi haki.

Pamoja na madai mengine, Mulundi amekuwa akitaka Ulimboka apelekwe mahabusu ili amtambue kama kweli alihusika kumteka, ili haki dhidi yake itendeke haraka. Dk Ulimboka alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba muda kuzungumzia ukweli kuhusu tukio hilo bado na kwamba hajawahi kuitwa, ili akutanishwe na mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo, uongozi wa Magereza nchini ulisema kwamba hauwezi kumsaidia mtuhumiwa huyo kwa lolote, badala yake ulimtaka aandike barua ya malalamiko na kumkabidhi mpelelezi wa kesi yake, ili ayafikishe mahakamani kwa hatua zaidi. Juzi Balozi Mutiso alisema kwamba kutokana na suala hilo kuendelea kuwa na utata hasa kuhusu uraia wa mtuhumiwa huyo, aliamua kutuma ujumbe
kwenda Gereza la Ukonga ambako alielezwa kwamba mtuhumiwa huyo anapatikana, lakini hakufanikiwa kumwona.

"Mimi nilituma kijana wangu leo pale gereza la Ukonga, lakini alipofika huko akaelezwa hayupo, eti afuatilie vizuri chanzo chake cha taarifa hizo mahali alipopelekwa. Nikaamua kukupigia simu (gazeti) ili tusaidiane kujua mahali alipo," alisema Mutiso.

Mutiso alisema kutokana na hatua hiyo ameamua kufuatilia ili kujua madai ya mtuhumiwa huyo kuwa raia wa Kenya kabla hajajihusisha zaidi na suala hilo. "Taratibu za kibalozi inapotokea jambo kama hilo, ni lazima awepo mtu au ndugu atakayemtambua kuwa Mkenya, au kupata vyeti vyake vya uraia.

Lakini hatujapatiwa vyeti hivyo. Kwa hivyo tunataka kuthibitisha kwanza kama ni Mkenya halafu tuhusike zaidi katika suala hulo," alisema Mutiso. Mutiso alisema leo atafanya uamuzi wa kufika mwenyewe katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa ama kuandika barua ya kutaka uthibitisho wa uraia
wa Mulundi.

"Jumatatu (leo) ndiyo nitawasiliana na wizara ili nifahamu kijana huyo yupo katika gereza gani," alisema
Mutiso.
 
Serikali inajipaka matope, sijui na yule aliyemuua mwangosi anafanyiwa unyama kama anaofanyiwa huyu raia wa kenya?
 
Serikali ya Kenya, mnamuacha tu huyu raia wenu, mikononi mwa majasusi?
 
Nahisi hawa wakenya wameanza kujiosha baada ya kusikia hii isshue imeshafika seneti ya US na UNHRC. Sasa chuzi linaanza kukolea viungo taraaaatibu.
 
Katika mambo ya Diplomasia ya kimataifa ni jambo la kawaida kwa nchi (Ubalozi) kufuatilia raia wake.

Wanataka kujua ni raia wao au la na kuona namna ya kumsaidia.

Hili sio tukio la kwanza kufuatiliwa na nchi. Hata majambazi au wahalifu wakubwa wananufaika na utaratibu wa nchi kufuatilia hatma ya raia wake.
 
Inghondi & co wanachekelea kwa pembeni wanakiiangalia movie inavyoendeleaje
 
Kwani serikali ya Tanzania,haikupeleka taarifa kamili kwenye ubalozi wa Kenya tangu awali?
 
Katika mambo ya Diplomasia ya kimataifa ni jambo la kawaida kwa nchi (Ubalozi) kufuatilia raia wake.

Wanataka kujua ni raia wao au la na kuona namna ya kumsaidia.

Mama Porojo unataka kutuaminisha kuwa Kenya ndiyo wamejua leo kuwa raia wao anahusishwa? Mbona hata vyombo vingi vya habari vilishalisema hilo kitambo? Hawa watawala walitaka kufichiana makosa, sasa limewavundia pabaya.
 
Huyo si mkenya wala nini, hawa jamaa wanatuzuga. Juzi juzi hapa niliona picha ya huyo anayedaiwa kumteka dk. ulimboka katika gazeti la Mwananchi huo mwili wake na dk. Ulimboka ni vitu viwili tofauti , Kwa mtu anayefikiria sawa sawa huyo jamaa hawezi kumteka ulimboka akiwa peke yake, kama ndo hivyo mbona hatujasikia amewataja wenzake alioshirikiana nao?

Wale waliotajwa na gazeti la Mwanahalisi mbona hatujasikia hata mmoja ameitwa kuhojiwa?

Watanzania tusiwe majuha hawa jamaa wanazuga ili upepo upite kama walivyozoea.
 
Muda ukifika hakuna atae jificha yote yata be open,najivunia kuzungukwa na mwenyez na yote atanionyesha kabla roho yangu haijatoka.
 
Anateswa bila kosa,waliohusika wanapeta tu mtaani
 
Nahisi hawa wakenya wameanza kujiosha baada ya kusikia hii isshue imeshafika seneti ya US na UNHRC. Sasa chuzi linaanza kukolea viungo taraaaatibu.

hakuna anayeweza kuamini kama yule Mkenya ndiye muhusika wa utekaji
nafikiri wametumia umafia wao na hela zao za kifisadi kutufanya tuamini hivyo
 
Mahakamani wanasema upelelezi unaendelea,ila kumwita Dr amtambue mbaya wake imekuwa ngumu,ni upelelezi wa aina gani huo? Kesi kama hizi ni changa la macho tuu.Nawashauri wakina Kijo Bisimba waweke kumbukumbu ya matukio ya kesi kama hizi ili serikali ya 2016 ipewe dondoo zake na libeneke litaanza upya. Sio mbali sana na hakika kitaeleweka tuu.
 
Serikali za kiafrika zimezoea kulindana hata kwenye dhambi zilizodhahiri.OLE WAO KWANI SIKU YAO INAKUJA miti yote itakuwa inateleza.
 
Kosa analo si alikiri mwenyewe tena akaona aanzie church ..kama walimpa na wakamhaidi kibano kidogo imekula kwake
 
Back
Top Bottom